Ikiwa watalipwa vyeti feki, nimekusudia kuishitaki Serikali

✓ Hapa unatetea nini hasa?

Je una maana ya kwamba kusoma kwa kutumia Jina la mtu mwingine si kosa so long as wewe ndiye uliyekuwa darasani?

Iko hivi;

1. Kusoma au kufanya shughuli fulani kwa kutumia Jina la mtu mwingine, kwa sheria za Tanzania hilo ni kosa..

2. Kusoma au kufanya shughuli fulani kwa kutumia vyeti au utambulisho (identification) ya mtu mwingine, kwa sheria za Tanzania ni kosa..

3. Kurudia rudia shule kwa kubadili badili majina badala ya kufuata utaratibu wa kisheria uliowekwa kufanya vile ambao ni kurudia mtihani (Resitting Examinations) aidha ya Chuo ama FTNA au CSEE au ACSEE nk, kupitia MEMKWA au QT, kwa sheria za Tanzania ni kosa...

## Sasa Mwigulu Nchemba yuko kwenye kundi gani katika hayo matatu?

✓ Kwa hili la wanaoitwa vyeti feki. Hebu tujiulize maswali kadhaa.

1. Kwanza tukubaliane kuwa, hakuna anayesema ni sawa tu kuajiri watu wasio na sifa stahiki kushika nafasi au nyadhifa fulani ktk utumishi wa umma..

2. Lakini, kwanini hawa watu waliopita ktk michakato halali ya kiserikali ya kuajiriwa wakahesabika kuwa wame - qualify lakini ghafla leo wanaonekana hawana sifa kwa kuitwa kila Jina baya i.e "wenye vyeti feki" au "wenye elimu ndogo" au "wezi..?" Kosa liko wapi..?

## Kwa maoni yangu mimi, nasema hawa watu wameonewa, wamenyanyaswa na kudhalilishwa sana...

## Kama ni makosa, yapo kwenye mifumo ya uhakiki na utambuzi ya kiserikali..
 
kunge kuwa na Uchunguzi mkali ungewaacha je kina bashite?na watu kibao tu waliokuwa na ukaribu na wakubwa?!!mbona jeshini na polisi hawakugusa?na huko ndiko walipo wengi sana
Wewe umefikishwa mahakamani. Ukakiri kwamba ulifanya kosa unalotuhumiwa kufanya. Utetezi wako: 'Mbona na fulani alifanya kosa hilo hilo?' Unategemea Mahakama ikuachie kwa utetezii huo?
 
unaishitaki vip wakat tanzania hakuna separation of power???
 
Why do you have to cheat the process bro!!??
huo nimetoa mfano,kuonyesha kuwa wale wa vyeti fake,sio kuwa hawakuwa compitent,na taaluma zao bali ni mfumo wa ovyo uliokuwepo na kuwapa mwanya wa kufanya udanganyifu wa vyeti vya kidato cha nne na sita.Ndio maana kwa sasa kuna ugumu sana wa kufoji vyeti kutokana na utaratibu uliopo wa uhakiki.
 
Wewe umefikishwa mahakamani. Ukakiri kwamba ulifanya kosa unalotuhumiwa kufanya. Utetezi wako: 'Mbona na fulani alifanya kosa hilo hilo?' Unategemea Mahakama ikuachie kwa utetezii huo?
wala mfano wako hauhusiani kabisa na nilichokiandika!!kama kweli serikali imeamua kukomesha kitu double standard inatoka wapi?!inshu ilikuwa kuondoa vyeti fake serikalini,kwanini baadhi ya watu waliachwa,harafu Rais anaulizwa anasema eti anayoangalia ni utendaji kazi sio vyeti!!hao waliokuwa ni madkatari ,walimu,hawakuwa na utendaji mzuri?!!hadi wengine walikaribia kustafu?!
 
Wenye vyet feki wamefundisha mpaka ma profesa je na wao wanaelimu feki nadhan serikali iko sahihi kuwalipa na pia serikali ilikosea kuwatoa maana kama tunapima maarifa n uwezo wa mtu wako sahihi ila kama cheti ndio uwezo wa mtu na sio maarifa bas kazi tunayo ndio maana Elimu yetu imefika hapa mtu ana dvn 1 n GPA kubwa halafu maarifa hana au hajui kitu
 
Endapo Serikali itawalipa hao vyeti feki, nimekusudia kuipeleka mahamani Serikali.
Ni jambo jema, lakini mimi ningekushauri uanze na hawa wahuni wanaotuibia Dodoma.

Mtu anakwenda kikazi Dodoma, posho ya kujikimu analipwa, halafu analipwa tena posho ya vikao anavyokaa kufanya kazi iliyompeleka huko!

Jingine, mbunge toka Pemba ambaye jimbo lake halina hata eneo la km za mraba 6 kumlipa posho ya mafuta lita 1,000 kwa mwezi ni uharamia.

Anza na hawa, nakuhakikishia utapata uungwaji mkono hata na majaji watakaosimamia hiyo kesi.
 
Wewe ndio unajiona muelewa sana, [emoji2]
Umekiri kabisa umefoji cheti cha form four kama unadhani hicho cheti hakina umuhimu licha ya kusoma kozi zote hizo kwanini ulifoji?? Kwanini usingeenda QT ukapata cheti chako kihalali???

Acheni kutetea wizi, mnalazimisha tuikubali forgery!!!

Shame!
 
Kwa kuongezea kuna baadhi ya Wafanyakazi hawakuguswa kabisa wakiwemo police, wanajeshi, askari magereza etc. Pili kama kulikuwa na tatizo kwenye ufanyaji kazi wao kwa nini hawakuondolewa mapema kwa sababu ya utendaji mbaya? Mfano mtu ni dereva au mhudumu ni lazima awe na cheti cha Form IV?
 
Walikuwa wanalipwa pesa wasizostahili zilitoka kwenye kodi zetu. Ni frauds.
Hakuna fraud. Walikuwa wanalipwa kwa kazi waliyofanya. Siyo cheti kilichokuwa kinalipwa.

Wangapi wana vyeti na hawawezi kazi??
 
Sasa hapo watajitambulisha kwa hayo majina feki au majina yao halali? [emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]. Kazi kweli kweli
 
Na wwe nenda kaforgi alafu utetezi wako Mahakamani uwe huo, eti mbona fulani nae aligushi lakini hawajamkamata!!? Utakuja kunishukuruu siku moja!!
 
Walikuwa wanalipwa pesa wasizostahili zilitoka kwenye kodi zetu. Ni frauds.
Wabongo wengi hawajui kua frauds ni very serious offense! Alafu Mara nyingi fraud ni chain, na siyo Mtu mmoja!!
 
JAMANI PESA WANALIPWA NA MIFUKO YA KIJAMII SIYO SERIKALI KUU(HAZINA)....

Kwa sababu walikuwa wanakatwa kipindi kile wanalipwa na serikali hivyo hadi hivi sasa jasho lao lipo mikononi mwa raia fulani (social security funds)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…