Ikiwa watalipwa vyeti feki, nimekusudia kuishitaki Serikali

Ikiwa watalipwa vyeti feki, nimekusudia kuishitaki Serikali

mwigulu nchemba alisoma Ilboru mm nilikuwa naye ijapo nilimtangulia kwa mbali sana na labda tujadili ukitumia majina ambayo siyo yako lkn ni wewe ndo uliyesoma au kaa darasani ni kosa.huenda alirudia shule akaamua kubadili majina na kwa enzi hizo ilikuwa ni kawaida.hapo kosa liko wapi?
✓ Hapa unatetea nini hasa?

Je una maana ya kwamba kusoma kwa kutumia Jina la mtu mwingine si kosa so long as wewe ndiye uliyekuwa darasani?

Iko hivi;

1. Kusoma au kufanya shughuli fulani kwa kutumia Jina la mtu mwingine, kwa sheria za Tanzania hilo ni kosa..

2. Kusoma au kufanya shughuli fulani kwa kutumia vyeti au utambulisho (identification) ya mtu mwingine, kwa sheria za Tanzania ni kosa..

3. Kurudia rudia shule kwa kubadili badili majina badala ya kufuata utaratibu wa kisheria uliowekwa kufanya vile ambao ni kurudia mtihani (Resitting Examinations) aidha ya Chuo ama FTNA au CSEE au ACSEE nk, kupitia MEMKWA au QT, kwa sheria za Tanzania ni kosa...

## Sasa Mwigulu Nchemba yuko kwenye kundi gani katika hayo matatu?

✓ Kwa hili la wanaoitwa vyeti feki. Hebu tujiulize maswali kadhaa.

1. Kwanza tukubaliane kuwa, hakuna anayesema ni sawa tu kuajiri watu wasio na sifa stahiki kushika nafasi au nyadhifa fulani ktk utumishi wa umma..

2. Lakini, kwanini hawa watu waliopita ktk michakato halali ya kiserikali ya kuajiriwa wakahesabika kuwa wame - qualify lakini ghafla leo wanaonekana hawana sifa kwa kuitwa kila Jina baya i.e "wenye vyeti feki" au "wenye elimu ndogo" au "wezi..?" Kosa liko wapi..?

## Kwa maoni yangu mimi, nasema hawa watu wameonewa, wamenyanyaswa na kudhalilishwa sana...

## Kama ni makosa, yapo kwenye mifumo ya uhakiki na utambuzi ya kiserikali..
 
kunge kuwa na Uchunguzi mkali ungewaacha je kina bashite?na watu kibao tu waliokuwa na ukaribu na wakubwa?!!mbona jeshini na polisi hawakugusa?na huko ndiko walipo wengi sana
Wewe umefikishwa mahakamani. Ukakiri kwamba ulifanya kosa unalotuhumiwa kufanya. Utetezi wako: 'Mbona na fulani alifanya kosa hilo hilo?' Unategemea Mahakama ikuachie kwa utetezii huo?
 
Langu ni hilo!

Vyeti feki, ni wahujumu nchi kama ilivyo Kwa mafisadi na wezi wengine!

Wameisababishia Serikali hasara kubwa, Kwa elimu yao ndogo, wamesababisha vifo vya wananchi Kwa kutoa huduma chini ya kiwango.

Endapo Serikali itawalipa hao vyeti feki, nimekusudia kuipeleka mahamani Serikali.

Itajulikana ikiwa Serikalini kuna wanufaika wa malipo haya chini ya mwamvuli wa wafoji vyeti.
unaishitaki vip wakat tanzania hakuna separation of power???
 
Why do you have to cheat the process bro!!??
huo nimetoa mfano,kuonyesha kuwa wale wa vyeti fake,sio kuwa hawakuwa compitent,na taaluma zao bali ni mfumo wa ovyo uliokuwepo na kuwapa mwanya wa kufanya udanganyifu wa vyeti vya kidato cha nne na sita.Ndio maana kwa sasa kuna ugumu sana wa kufoji vyeti kutokana na utaratibu uliopo wa uhakiki.
 
Wewe umefikishwa mahakamani. Ukakiri kwamba ulifanya kosa unalotuhumiwa kufanya. Utetezi wako: 'Mbona na fulani alifanya kosa hilo hilo?' Unategemea Mahakama ikuachie kwa utetezii huo?
wala mfano wako hauhusiani kabisa na nilichokiandika!!kama kweli serikali imeamua kukomesha kitu double standard inatoka wapi?!inshu ilikuwa kuondoa vyeti fake serikalini,kwanini baadhi ya watu waliachwa,harafu Rais anaulizwa anasema eti anayoangalia ni utendaji kazi sio vyeti!!hao waliokuwa ni madkatari ,walimu,hawakuwa na utendaji mzuri?!!hadi wengine walikaribia kustafu?!
 
Wenye vyet feki wamefundisha mpaka ma profesa je na wao wanaelimu feki nadhan serikali iko sahihi kuwalipa na pia serikali ilikosea kuwatoa maana kama tunapima maarifa n uwezo wa mtu wako sahihi ila kama cheti ndio uwezo wa mtu na sio maarifa bas kazi tunayo ndio maana Elimu yetu imefika hapa mtu ana dvn 1 n GPA kubwa halafu maarifa hana au hajui kitu
 
Endapo Serikali itawalipa hao vyeti feki, nimekusudia kuipeleka mahamani Serikali.
Ni jambo jema, lakini mimi ningekushauri uanze na hawa wahuni wanaotuibia Dodoma.

Mtu anakwenda kikazi Dodoma, posho ya kujikimu analipwa, halafu analipwa tena posho ya vikao anavyokaa kufanya kazi iliyompeleka huko!

Jingine, mbunge toka Pemba ambaye jimbo lake halina hata eneo la km za mraba 6 kumlipa posho ya mafuta lita 1,000 kwa mwezi ni uharamia.

Anza na hawa, nakuhakikishia utapata uungwaji mkono hata na majaji watakaosimamia hiyo kesi.
 
mashitaka gani?ni nani mwenye kosa kati ya serikali na hao vyeti feki.pia tunatakiwa kuwa makini kwa jambo hili nadhani wengi hawajaelewa kiini cha vyeti feki.sijajua wengi wanalitafsiri kwa namna ipi hili jambo.huenda jambo hili linahitaji mjadala mpana ili kuwa na ile kitu inayoitwa common understanding.mfano mm nilimaliza darasa la saba na jamaa mmoja ambaye hakufaulu kwenda kidato cha kwanza enzi hizo tulikuwa tunasema hakuchagulakini akajiunga na chuo cha RMA kwa maana ya rural medical assistant.alivyomaliza aliajiriwa na baada ya miaka mitatu akaenda kusoma CO yaani clinical officer na hatimaye AMO.assistant medical officer.Serikali ilitoa mwongozo baadaye kuwa pia walipaswa kujiendeleza kwa maana ya kuwa na elimu ya sekondari.akafoji cheti cha kidato cha nne na akaondolewa kwenye ajira.je mtu huyo hakuwa competent kama watu wengi humu wanavyojiaminisha?ukiangalia wengi walikumbwa ktk mtego huu kwa ajili ya cheti cha kidato cha nne tu.tujadili.
Wewe ndio unajiona muelewa sana, [emoji2]
Umekiri kabisa umefoji cheti cha form four kama unadhani hicho cheti hakina umuhimu licha ya kusoma kozi zote hizo kwanini ulifoji?? Kwanini usingeenda QT ukapata cheti chako kihalali???

Acheni kutetea wizi, mnalazimisha tuikubali forgery!!!

Shame!
 
Anzia hapa kwanza. Ni nani aliwaingiza kazini? Huyo ndiye mwenye hatia wala siyo walio foji vyeti.

La pili Kumbuka aliyeanzisha zoezi Mwendazake naye alikuwa na PhD feki iliyopelekea kuuawa kwa Ben Saanane ambaye alikuwa anahoji uhalali wake.

Tatu zoezi lilikuwa batili kwa vile lilichaguwa watu wa kuwatoa. Kwa mfano Daudi Bashite aliendelea kuwa RC Dar es Salaam kwa kutumia cheti cha Paul Makonda. Said Bagaile aliendelea kuwa Waziri wa Utalii kwa kutumia cheti cha Hamis Kigwanggalla, Lameck Madelu aliendelea kuwa Waziri wa Sheria kwa kutumia cheti cha Mwigulu Nchemba.

Hizi double standard za Magufuli ndizo Mungu hapendi, na ndiyo maana Magufuli amekufa licha ya kuiba kura zote za 2020 na kuweka wabunge wake.
Kwa kuongezea kuna baadhi ya Wafanyakazi hawakuguswa kabisa wakiwemo police, wanajeshi, askari magereza etc. Pili kama kulikuwa na tatizo kwenye ufanyaji kazi wao kwa nini hawakuondolewa mapema kwa sababu ya utendaji mbaya? Mfano mtu ni dereva au mhudumu ni lazima awe na cheti cha Form IV?
 
Walikuwa wanalipwa pesa wasizostahili zilitoka kwenye kodi zetu. Ni frauds.
Hakuna fraud. Walikuwa wanalipwa kwa kazi waliyofanya. Siyo cheti kilichokuwa kinalipwa.

Wangapi wana vyeti na hawawezi kazi??
 
Inaonekana hata hujui chanzo cha tatizo lilikuwa ni wapi?!! Yaani mimi nimetumia cheti cha mtu cha elimu ya kidato cha nne, nikakitumia nikasomea kidato cha sita, nikafaulu, nikaingia chuo kikuu kusomea udaktari, nikapiga miaka yangu sita, nikafaulu vizuri, nikapiga masters yangu, nikapata kazi ya kutibu wagonjwa hapo utasemaje nimesababisha vifo kwa watu?

Inshu kubwa haikuwa vyeti vya taaluma bali ni cheti cha kidato cha nne na hizo pesa wanazolipwa sio za Serikali ni michango yao waliyochangia kwenye mifuko ya jamii.
Sasa hapo watajitambulisha kwa hayo majina feki au majina yao halali? [emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]. Kazi kweli kweli
 
Kwa kuongezea kuna baadhi ya Wafanyakazi hawakuguswa kabisa wakiwemo police, wanajeshi, askari magereza etc. Pili kama kulikuwa na tatizo kwenye ufanyaji kazi wao kwa nini hawakuondolewa mapema kwa sababu ya utendaji mbaya? Mfano mtu ni dereva au mhudumu ni lazima awe na cheti cha Form IV?
Na wwe nenda kaforgi alafu utetezi wako Mahakamani uwe huo, eti mbona fulani nae aligushi lakini hawajamkamata!!? Utakuja kunishukuruu siku moja!!
 
Walikuwa wanalipwa pesa wasizostahili zilitoka kwenye kodi zetu. Ni frauds.
Wabongo wengi hawajui kua frauds ni very serious offense! Alafu Mara nyingi fraud ni chain, na siyo Mtu mmoja!!
 
JAMANI PESA WANALIPWA NA MIFUKO YA KIJAMII SIYO SERIKALI KUU(HAZINA)....

Kwa sababu walikuwa wanakatwa kipindi kile wanalipwa na serikali hivyo hadi hivi sasa jasho lao lipo mikononi mwa raia fulani (social security funds)
 
Back
Top Bottom