The Palm Beach
JF-Expert Member
- Dec 30, 2015
- 1,967
- 4,267
✓ Hapa unatetea nini hasa?mwigulu nchemba alisoma Ilboru mm nilikuwa naye ijapo nilimtangulia kwa mbali sana na labda tujadili ukitumia majina ambayo siyo yako lkn ni wewe ndo uliyesoma au kaa darasani ni kosa.huenda alirudia shule akaamua kubadili majina na kwa enzi hizo ilikuwa ni kawaida.hapo kosa liko wapi?
Je una maana ya kwamba kusoma kwa kutumia Jina la mtu mwingine si kosa so long as wewe ndiye uliyekuwa darasani?
Iko hivi;
1. Kusoma au kufanya shughuli fulani kwa kutumia Jina la mtu mwingine, kwa sheria za Tanzania hilo ni kosa..
2. Kusoma au kufanya shughuli fulani kwa kutumia vyeti au utambulisho (identification) ya mtu mwingine, kwa sheria za Tanzania ni kosa..
3. Kurudia rudia shule kwa kubadili badili majina badala ya kufuata utaratibu wa kisheria uliowekwa kufanya vile ambao ni kurudia mtihani (Resitting Examinations) aidha ya Chuo ama FTNA au CSEE au ACSEE nk, kupitia MEMKWA au QT, kwa sheria za Tanzania ni kosa...
## Sasa Mwigulu Nchemba yuko kwenye kundi gani katika hayo matatu?
✓ Kwa hili la wanaoitwa vyeti feki. Hebu tujiulize maswali kadhaa.
1. Kwanza tukubaliane kuwa, hakuna anayesema ni sawa tu kuajiri watu wasio na sifa stahiki kushika nafasi au nyadhifa fulani ktk utumishi wa umma..
2. Lakini, kwanini hawa watu waliopita ktk michakato halali ya kiserikali ya kuajiriwa wakahesabika kuwa wame - qualify lakini ghafla leo wanaonekana hawana sifa kwa kuitwa kila Jina baya i.e "wenye vyeti feki" au "wenye elimu ndogo" au "wezi..?" Kosa liko wapi..?
## Kwa maoni yangu mimi, nasema hawa watu wameonewa, wamenyanyaswa na kudhalilishwa sana...
## Kama ni makosa, yapo kwenye mifumo ya uhakiki na utambuzi ya kiserikali..