Ikiwezekana, Bunge lianze na mswada wa dharura kujadili Katiba Mpya; hii Katiba ya sasa kitendo cha Makamu kutambuliwa kuwa mrithi ni hatari

Mi naangalia tu hizi senema.
Eti muheshimiwa rais Samia Suluhu tafadhalini jamani.
Majaliwa angetosha vizuri tu hapo.
 
Binafsi napendekeza hiyo nafasi ya makamu ifutwe kabisa, in case of any emergency judge mkuu au spika anashika nchi kwa siku chache then tunarudi kwenye uchaguzi.
 
Hahahah haya mambo haya 😂😂😂 niliwahi kusikia Mwamunyange alitolewa kwenye cheo mana alikuwa mfuasi wa babu wa Monduli, ila kuhusu tamaa mm nadhan yeyote anaweza kuwa na tamaa bila kuangalia cheo chake mfano kipindi cha Nyerere kuvamia Uganda ili kumtoa idd amini hvy kisheria n Uganda ilikuwa chini ya Tz lakin hatukuonyesha tamaa hizo 🤔🤔🤔
 
Acha utabiri wa tunguli
Acha roho ya husda.
Katiba siku zote ilikuwepo na mlikuwa mnaiona kwanini hamkuleta hiyo mada?
Samia kaukapata udambwi udambwi mnaanza kuteseka[emoji1][emoji1][emoji1]
Uraisi wa kuangukia sio?! Lakini wazo langu ni kumlinda Rais dhidi ya fitna na hila. Makamu angekuwa Rais wa mpito tukingoja uchaguzi mwingine na ikiwezekana na yeye ashiriki.
 
Hofu inatoka wapi?
je unakumbuka hili neno na nafasi ya uMakamu ilileta maloloso sana wakati wa Vyama vingi, na hasa kutokuelewana na ndipo wakamtoa Rais atokaye Zanzibar asiwe Makamu kwani ingeleta matatizo km hivi leo. Tulivyoungana na Zanzibar Mh Karume alikuwa Makamu na angekuwa hai kabla ya Mh J Nyerere ingebidi aje atawale mpaka huku.

Mtego huu umemkuta Mh Mama Samia naona sasa waZanzibar watanyamaza mambo ya muungano kwani wapo wengi sasa hapo juu, Hussein Mwinyi na makamu Mwanasheria Othman, je watauvunja Muungano

MY TAKE ikionekana km kuna njama imefanyika kumtoa Rais ili Makamu achukue mara moja haitakubalika kwani kuna TISS na UWT
 
Uraisi wa kuangukia sio?! Lakini wazo langu ni kumlinda Rais dhidi ya fitna na hila. Makamu angekuwa Rais wa mpito tukingoja uchaguzi mwingine na ikiwezekana na yeye ashiriki.
Katiba imeandikwa kabla hujazaliwa hakuna kitu kimetokea leo dola kashika Mwanamke wa shoka mnaanza ufukunyuku,
Poleni sana ngoma ndio kwaaanza inaanza.
 
Uraisi wa kuangukia sio?! Lakini wazo langu ni kumlinda Rais dhidi ya fitna na hila. Makamu angekuwa Rais wa mpito tukingoja uchaguzi mwingine na ikiwezekana na yeye ashiriki.
Muache amepata ubwete
Yule mwanachama mwenzetu wa Uwabata ale kuku kwa mrija[emoji1787][emoji1787]
 
Kinawatenga vipi wananchi ilhali kura wanapigiwa wote-Rais na Makamu wa Rais. Au ndio ile mnapiga kura kama unaaccept terms and conditions kwenye Internet!
 

Ninahisi ana maoni kwamba,mara nyingi kwenye uchaguzi mkuu huwa tunampigia kura Rais,mgombea mwenza wake mara nyingi huwa hawaumizi watu vichwa kwa kuwa wanaamini atafanya kazi chini ya Rais aliepigiwa kura...mawazo yake nilivoyasoma ni kuwa huyu makamu anakuwa Rais gafla wakati watu kisaikolojia hawakujishugulisha na kujua sifa zake wakati anagombea na Rais,kwa hiyo mtoa mada anahisi tunapata Rais ambae hatukumchagua

maoni yangu mimi...huo utaratibu wa kikatiba unaousemea wewe,watunga katiba hii ni kama walikuwa wanawaza kuwa hata Rais ikitokea akafariki,hawezi kufariki mwanzoni mwa mhula namna hii, waliamini Rais lazima avute vuteee ikiwezekana walau hata miezi michache kabla ya mhula wake kuisha ndiyo anaweza kufa, kwetu limetokea mwanzoni kabisaaa, ni mhula mzima wa miaka mitano
 
Acha mikwara mbuzi wewe. Amwulize vipi mwenyekiti wake wakati unatumia fake ID?
 
Hata ukishindia kashata na maji ya kandoro unaweza kulidhika vilevile.

Njaaa inakutafuna
 
Hofu inatoka wapi?
je unakumbuka hili neno na nafasi ya uMakamu ilileta maloloso sana wakati wa Vyama vingi, na hasa kutokuelewana na ndipo wakamtoa Rais atokaye Zanzibar asiwe Makamu kwani ingeleta matatizo km hivi leo.

Tulivyoungana na Zanzibar Mh Karume alikuwa Makamu na angekuwa hai kabla ya Mh J Nyerere ingebidi aje atawale mpaka huku.

Mtego huu umemkuta Mh Mama Samia naona sasa waZanzibar watanyamaza mambo ya muungano kwani wapo wengi sasa hapo juu, Hussein Mwinyi na makamu Mwanasheria Othman, je watauvunja Muungano.

MY TAKE ikionekana km kuna njama imefanyika kumtoa Rais ili Makamu achukue mara moja haitakubalika kwani kuna TISS na UWT
 
Vipi kama kwenye uchaguzi akashinda mwanamke tena.?
 
Ni ngumu sana kuelewa maana ya sheria hii. Kama cheo cha juu kama Makamu wa Rais kinaweza kuwa cha uteuzi tu, inakuwaje chaguzi zirudiwe kwa nafasi za chini kama udiwani na ubunge??

Kama chama kinaweza kupewa jukumu la kuteua makamu wa Rais wa nchi - basi chama hicho pia kinaweza kuteua mbunge na diwani!

Tuache kuchezea fedha zinazopatikana kwa jasho kwa kufanya chaguzi za marudio kwa madiwani na wabunge, sawa na tulivokwenda kufanya uchaguzi mpya wa Rais!! Kama hili linakataliwa hasa na CCM, basi lengo lilikuwa ni kuweka mazingira ya kuwa na udhibiti wa Bunge na wabunge na halmashauri. Nia hii ni ovu na kifo cha JPM kimefungua fikra!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…