kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
Siku 4 baada ya kijana Hamza kusababisha mauaji ya wapendwa wetu pale Selander Bridge nilikwenda Airport kuwapokea jamaa zangu kutoka Ulaya. Tukiwa kwenye gari langu kuelekea Mikocheni, njiani kwenye barabara ya Nyerere tukaona vibanda vingi vichafuvichafu njia nzima kutoka Airport hadi Vingunguti vya watu wanaouza chai na supu.
Wageni wangu wakaniukiza vile vibanda kandokando ya barabara ya kutoka airport ni vya akina Nani? Wanajulikana wote wanaofanya kazi kwenye vibanda vile?
Je, viongozi wenu na wageni muhimu wanaofika nchini kupitia airport hii wanatumia barabara hii pia au Kuna barabara nyingine? Kama ni hii mnawalinda vipi na snipers wanaoweza kutumia vibanda hivi kuwalenga? Mimi sikuwa na majibu sahihi kwa maswali Yao.
Siasa uchwara zinatufanya tuone ni sawa machinga kufanya kazi popote kwa aina yoyote. Siasa uchwara haziwaoni machinga wanaochafua mazingira, wanaojenga vibanda hata barabara ya airport lango kuu la nchi, njia za waenda kwa miguu, njia za maji na mitaro ya majitaka, mbele ya maduka ya wanaolipa Kodi na chini ya nyaya za umeme wa msongo mkubwa.
Iko siku vibanda hivi vichafu vitageuka maficho ya magaidi. Tuvute muda TU.