Iko wapi Tanzania yangu? Ipo wapi CCM yangu; wapo wapi wazee wangu wenye dhamana ya chama na nchi yangu?

Iko wapi Tanzania yangu? Ipo wapi CCM yangu; wapo wapi wazee wangu wenye dhamana ya chama na nchi yangu?

Wenye ni nzuri ndio wako hatarini kwa sasa. Wanaosifia tu ndio wako salama.
Duh Inasikitisha, mimi nina imani ya kuwa maneno ya Hayati Nyerere yanaonyesha yana ukweli. Upinzani wa dhati utatokea ndani ya CCM. The only way nj kuwaonyesha wanaoweza kuthubutu kuwa kuna watu nyuma yao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wenye ni nzuri ndio wako hatarini kwa sasa. Wanaosifia tu ndio wako salama.
Duh Inasikitisha, mimi nina imani ya kuwa maneno ya Hayati Nyerere yanaonyesha yana ukweli. Upinzani wa dhati utatokea ndani ya CCM. The only way nj kuwaonyesha wanaoweza kuthubutu kuwa kuna watu nyuma yao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna dawa zaidi ya wazee hao kuanzisha mchakato wa kuwawezesha viongozi ndani ya ccm, kuja na mbinu za kulinda chama na nchi.

Dhuluma nyingi zina fanyika, leo amefariki Mzee shante akiwa mahabusu, uchunguzi haujakamilika, kama mtu ana kesi na ushahidi upo, huo upelelezi unaochukua miaka ni wa vipi. Chama na nchi zinaendeshwa kiajabu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
IKO WAPI TANZANIA YANGU; IKO WAPI CCM YANGU: WAKO WAPI WAZEE WANGU WENYE DHAMANA YA CHAMA NA NCHI YANGU.

Ndugu Watanzania na wanajamvi, nawaombea kila la kheri wakati huu mgumu. Mola atatupa neema zake na tutavuka hili janga tukiwa salama wa afya.

Ninaleta uzi huu nikiwa na majonzi na wasiwasi na chama changu au chama kikongwe nchini, kinavyo tetereka na huku wale walezi na washauri, waliopewa jukumu na Mungu wako kimya na wala hawajaribu kufanya wajibu wao.

Watanzania tusijidanganye, kutetereka au anguko la CCM, litakuwa na effect kubwa sana kwa nchi na wananchi.

Je, tatizo la hizi ishara mbaya ndani ya chama changu, lina sababishwa na nini?

Mimi sio mwandishi mahiri, na wala sio fani yangu. I am a very good Administrator but not a Writer; nitajaribu kueleza maoni yangu, ubovu uliopo ndani ya chama changu.

Tokea enzi na enzi, vyama vikubwa ustawi wao sio mali au wingi wa wanachama, bali ni siasa safi, uongozi wenye busara, uadilifu, na muhimu zaidi WALEZI WAZOEFU NA WASIO NA TAMAA. CCM ilikuwa na sifa nyingi kama hizi na Zaidi. Mfano mzuri ni vyama vya upinzani Uingereza au USA, vinaweza visishike dola kwa miaka zaidi ya 10-20, lakini bado vina nguvu, sauti na vinazidi kukuwa.

Kama Rais wangu asemavyo: MSEMA KWELI NI KIPENZI CHA MUNGU. Ukweli ni kuwa walezi wetu kama akina Mwinyi, Mkapa, Kikwete, Malecela, Msuya, kinana, nk. wamekuwa na dosari nyingi sana, ambazo zimemuwezesha Rais Magufuli kukiteka chama na kukibadilisha kuwa tofauti na asili ya chama. Huwezi kubadilisha mwenendo au siasa za chama bila ya ridha ya chama, na chama sio wale wachache wanaounga lolote MK atakacho, ila ni wale watakaojadiliana naye na kuja na mbinu vumbuzi na zenye tija na manufaa kwa chama nchi na Africa. Nitazungumzia baadhi ya hawa walezi wachama na kwa machache:

1. MZEE MWINYI: Heshima kwako Mzee wangu, Mungu akupe afya na maisha marefu. Mzee wetu ukweli ni kuwa wewe ndiye aliyetokea kuwa janga kubwa la CCM leo, sijui ni uzee, Alhamdulilah imani yako ni kubwa sana, na unajua dini vizuri sana. Lakini kwa sasa uyafanyayo ni maovu sana kwa dhamana ya chama na kwa umma uliyopewa na Mola wetu. Mzee wetu, wewe kama Babu yetu, leo uko tayari kukaa kimya huku unayaona maovu yakifanywa ndani ya chama, Babu unajua fika ya kuwa mwanao atapata alichoandikiwa na Mola wake, na ambacho hakuandikiwa hatakipata.

Kama ameandikiwa kuwa Rais wa Zanzibar, ataupata huo urais bila ya uvumba wala ubani, lakini CCM wala Magufuli hawawezi kumpa Hussein kila ambacho Mola hakukiridhia. Babu mwanao Hussein, ni kijana mzuri, mwenye hekima na heshima, anapendwa na sifa zake binafsi ndizo zitakazo mpitisha kuwa na cheo chochote hapa duniani. Mzee wetu, tunakusihi ujirudi na kufanya wajibu wako kama Quran ilivyokufundisha.

2. MZEE MKAPA: Heshima kwako Mzee wangu, Mungu akupe afya na maisha marefu.

Mzee wangu, mimi ni mfuasi wako wa kisiasa na nilipenda sana namna ulivyoirudisha Tanzania kwenye ulimwengu wa biashara, you did very well during your tenure. Mheshimiwa kuna taabu sana kuhusu hii awamu ya 5, kila mtu anakuona wewe ndio the strongest kati ya walezi wote walio hai leo, tena mwenye uwezo wa kumshauri Rais wetu anapohitaji ushauri, japokuwa inasemekana ni Rais asiyependa kushauriwa na asiye na shukrani.

Inasemekana kuwa hata simu zenu mara nyingi hazipokelewi. Mzee wangu, wewe bado unapendwa na kuheshimiwa na wengi sana, na neno lako bado lina uzito mkubwa sana. Mzee wangu, una power kubwa sana kumshinda kiongozi yoyote hapa nchini, na wananchi wanakuangalia wewe ufanyavyo.

Tafadhali sana jitahidi na wazee wenzako kuja na mbinu ya kurudisha chama chetu kwenye mistari na misingi yake. Hivi kinavyokwenda ni ileile staili ya Marehemu Rais Moi na KANU, na leo tunaiona KANU ilipo. Unalo jukumu kubwa sana, na USIJIFICHE KWENYE GLASS. Your legacy highly depends on hii awamu ya 5.

This will be on you Sir

3. MZEE KIKWETE: Heshima kwako Mzee wangu, Mungu akupe afya na maisha marefu. Duh kaka yangu kipenzi Pole sana tena sana, Lilahi kila ninaposwali ninakuombea Allah akukinge na macho na midomo ya wanyonge, Maanake kila zuri lifanywalo na awamu hii ya 5 linasheherekewa kama la kwao peke yao, lakina kila baya au lenye maumivu linakuwa lako kaka yangu, na Ukweli ni kuwa yenye maumivu ni mengi sana awamu hii.

Chama chetu kinaendeshwa kichokorachokora, vijana wamepewa dhaman bila ya kuwekewa check n balance, wanafanya watakavyo, Sheikh ukienda Magerezani kila Mkoa waliobambikizwa makesi ni wengi sana, tena kwa jina la Rais, na Rais hana habari nazo. Kuna viongozi wanamtumia Rais vibaya sana. Awamu hii imekuwa awamu ya visasi, na hilo sasa limerudi nyumbani. Chama kinavurugwa kuwabambikia kesi viongozi na kuwaadhibu. Rushwa ni aina mbili -- ya pesa/fursa na ya vitisho.

Kaka yangu bado u kipenzi cha UMMA, hebu funga safari uende Mbeya, Arusha, Kigoma au Mwanza kama mtalii tu, uone kama watu hawakufunga barabara kwa mapokezi yako, YOU ARE STILL LOVED TO THE HILT.

WAZEE MWINYI/MKAPA/KIKWETE: Ushauri wangu ni kama ufuatvyo, na kama nisemayo yana ukweli wowote tutaona wananchi wengi sana bila kujali itikadi ya vyama, wataniunga mkono na kuwapa wazee wetu moyo wa kuweza kufanya mema na mazuri, yatakayo nyoosha njia nzuri nchi yetu inayohitaji kupita, na pia mtamu weza kumsaidia Mheshimiwa Rais wetu mpendwa kuusikiliza ushauri wenu mzuri na kufanya mema kwa wananchi.
  • Kama wazee wenye dhamana ya chama na nchi, dhamana hiyo mlipewa na Mola, mulipochaguliwa kuwa Ma Raisi wa Tanzania, wajibu huo mnao hadi pumzi yenu ya mwisho hapa duniani. Jialikeni mkutane pamoja bila ya kuficha, kiwe hata chakula cha mchana kwa Mzee Mwinyi. Hicho kikao kwanza kitawafungua macho wengi sana, na kutakuwa na maneno mengi, yalio ya busara, hekima na upendo, na yaliyokuwa na unafiki na fitna. Sisi ni watu wenye busara tutayafuata ya busara na hekima, ya kinafiki yataendelea kuwa ya kinafiki. This will be a wake up call, and will prove that you still matter in this nation.
  • Katika kikao hicho, muanzishe a forum ya viongozi wastaafu ambao hawana tena nia za URAIS, it should include only Ex-Presidents & Ex- Prime Ministers wasiokuwa na ambitions za URAIS, na kila mmoja a sing an undertaking.
  • Muwe na uwezo wa kuweza kukutana na Raisi kwa pamoja sio zaidi ya mara 3 kwa mwaka, na kumshauri a jirekebishe kama kuna jambo muhimu sana na hatari kwa nchi na chama.
  • Muwe na uwezo kuitisha kikao cha kamati kuu ya CCM, kukielezea hoja yenu na kuitaka kamati ichague committee ya chaguo lenu kufuatilia jambo hilo, na kama litaekewa pingamizi, mtakuwa na uwezo kwa jina la chama kuwafikia wananchi kupitia media na kwa kufanya press conference. CCM sio chama cha mtu bali watu.
  • Ajenda yenu sasa ambayo ni muhimu sana ni namna sasa hivi nchi na chama vnavyoendeshwa, viongozi wanavyodhalilishwa.
Ndugu wana CCM,Wantanzania na JF Huu ni ushauri na maoni yangu, nitafurahi kukosolewa na kuungwa mkono. Nia yangu kubwa sio kuona mtu anatukanwa, kebehiwa, bali nitafurahi kama tuna rekishana. Tanzania nz hata chama changu sio mali ya mtu, ni mali ya Watanzania. Lazima tujirekebishe, tunaanza kuona ukabila na udini ukishamiri.

Hii ni nchi yetu wote, tumebahatika sana kuwa na watu tusiokuwa na ukabila na udini, kwani kwa muda mrefu tulikuwa wakweli na wapenda haki, wanasiasa wasitufundishe mgawanyiko ambao hautatusaidia. 1982, palikuwa hakuna hata mfugaji mmoja wa Kimasai au Kisukuma akiishi Mtwara, Lindi au Morogoro, lakini leo mashala ni nyumbani, na hayo ni maendeleo. Lakini hizi siasa za kidini na kikabila zitatuchafua.
Maneno mengi lakini naona kama pumba na propaganda za kipumbavu. Hukufundishwa kitu kinachoitwa ufupisho(precision) shuleni? Unasema hapokei simu za marais wastaafu hii inaleta sense? Yaani JPM asipokee simu ya Rais Mstaafu Mkapa au Kikwete? Wakati alipoenda south kwenye uapisho wa Ramaphosa walikaa kiti kimoja kwenye ndege na JPM akapiga selfie.Pia JPM alimpiga Jakaya na Ramaphosa picha kwa simu yake. Leo hii asipokee simu zao?
Unasema JPM anatakiwa awekwe kitako ajirekebishe kwa makosa yapi?
 
teke la punda anaekata roho la yule katibu mkuu msitafu wa zamani aliyetimuliwa!!

Nilitegemea ungechangia mawazo ya kuboresha thread badala yake kama kawaida yenu nyie ZERO brain umeleta pumba zako!!
 
Maneno mengi lakini naona kama pumba na propaganda za kipumbavu. Hukufundishwa kitu kinachoitwa ufupisho(precision) shuleni? Unasema hapokei simu za marais wastaafu hii inaleta sense? Yaani JPM asipokee simu ya Rais Mstaafu Mkapa au Kikwete? Wakati alipoenda south kwenye uapisho wa Ramaphosa walikaa kiti kimoja kwenye ndege na JPM akapiga selfie.Pia JPM alimpiga Jakaya na Ramaphosa picha kwa simu yake. Leo hii asipokee simu zao?
Unasema JPM anatakiwa awekwe kitako ajirekebishe kwa makosa yapi?
Ubovu ni kuwa mnajifanya mnampenda Raisi, lakini nyie ndio maadui wake wakubwa. Mkiwaona waharibifu wanaotumia jina la Raisi au Chama, mnawasherehekea badala ya kukemea.

Niliyoyasema yapo na yametokea

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ubovu ni kuwa mnajifanya mnampenda Raisi, lakini nyie ndio maadui wake wakubwa. Mkiwaona waharibifu wanaotumia jina la Raisi au Chama, mnawasherehekea badala ya kukemea.

Niliyoyasema yapo na yametokea

Sent using Jamii Forums mobile app
Ubovu ni kuwa mnajifanya mnampenda Raisi, lakini nyie ndio maadui wake wakubwa. Mkiwaona waharibifu wanaotumia jina la Raisi au Chama, mnawasherehekea badala ya kukemea.

Niliyoyasema yapo na yametokea

Sent using Jamii Forums mobile app
Yaani leo hii JPM hapokei simu ya mzee mkapa? Au mzee Jakaya? Na JPM alikiri kwa kinywa chake bila mzee Mkapa asingekuwa raia namba moja hapa Tz
 
Kilio chako kimepata jawabu, wenye chama asilia wamerudi, watesi wenu wale waliojiita mpya wamesogezwa kando.
 
Wataendelea kuimba wimbo wa Katiba mpya?
Wanajua umuhimu wa katiba wakishakuwa nje ya mfumo na sio ndani ya mfumo.Leo makamba hawezi yarudia Yale maneno ya atawabatizeni kwa moto.Wakiwa madarakani huwa ni vipofu na upanda miba njia awajui kesho watapita njia hio hio.Leo Membe,Lowasa, sumaye,mkapa eti wanaimba wimbo wa katiba mpya hali walikuwa na nafasi ya kuleta mabadiliko walitegemea kila siku ni jumapili.Nyerere ndie wa kulaumiwa kwa kuicopy katiba hii mbovu bila kuwashirikisha wananchi. Yapo makabila ni maalumu kwa kazi za kutumia nguvu na sio za reasoning so ukimix hivi vitu ni lzm mambo yaende mrama hata ukistudy kuhusu mfumo wa colonial administration utaona jamii ipi ilikuwa kwa ajili ya kazi za kutumia nguvu na zipi za kutumia reasoning.
 
Back
Top Bottom