JaxenDL
JF-Expert Member
- May 17, 2022
- 1,118
- 2,581
Baada ya misheni ya kwanza ya Apollo 11 kufanikiwa, Rais Richard Nixon alituma zawadi kwa mataifa 135 duniani, ikiwemo Tanzania.
Zawadi hii ilijumuisha: Chembe nne ndogo za mchanga wa mwezi (zenye ukubwa wa punje za mchele) zilizowekwa ndani ya tufe la plastiki, Bendera ndogo ya Tanzania ambayo ilisafirishwa na wanaanga hadi mwezini na kurudi, Kibao cha mbao (plaque) chenye maandishi yanayosema zawadi hiyo ni ya watu wa Tanzania
Pia Baada ya misheni ya mwisho ya Apollo 17, Tanzania ilipewa tena kipande kingine cha mwamba wa mwezi. Kipande hiki kilikuwa kikubwa kidogo kuliko vile vya mwanzo na kilikatwa kutoka kwenye mwamba mkubwa unaojulikana kama "Goodwill Rock" (Lunar Basalt 70017).
kama ilivyotajwa na NASA kwa sasa zaidi ya vipande 180 vimepotea duniani, zawadi za Tanzania kimsingi ni mali ya serikali na hutunzwa katika makumbusho ya taifa au ofisi kuu za kiserikali.
Gharama yake kwenye blackmarket
Joseph Gutheinz Jr., maarufu kama "The Moon Rock Hunter", ni wakili na aliyekuwa ajenti maalumu wa NASA ambaye amejitolea kutafuta miamba ya mwezi iliyopotea duniani kote na Oparesheni "Lunar Eclipse".
Gutheinz anafahamika zaidi kwa kuongoza operesheni ya siri mwaka 1998 iliyofanikiwa kuipata mwamba wa mwezi wa nchi ya Honduras uliokuwa unauzwa kimafia kwa Dola milioni 5 (13 Billion)Apo ni mwaka 1998 sasaivi bei itakua maradufu.
Joseph Gutheinz, Katika utafiti wake na waandishi kama Joe Kloc (mwandishi wa kitabu The Case of the Missing Moon Rocks), Tanzania bado imeorodheshwa kama moja ya nchi ambazo miamba yake haijulikani ilipo (location unknown)
Licha ya juhudi zake za kupata zaidi ya miamba 79 duniani kote kwa msaada wa wanafunzi wake, hakuna ripoti alifanikiwa kuipata ile ya Tanzania hadi sasa. Miamba yetu bado inabaki kuwa siri au "lost" katika orodha zake za kimataifa.