Iko wazi kwa sasa mama anahujumiwa kwa akili ya juu sana

Matongee

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2023
Posts
1,234
Reaction score
3,192
Huu ni ukweli mchungu. Haihitaji degree kujua kwa sasa kuna watu wazito karibu na mama wanaosukuma karata zao kwa umakini mkubwa huku wakimwingiza mama kingi. Ubaya ni kwamba hawa waovu hawajitokezi hadharani kufanya uovu wao...

Kwa mfano kuwatumia hawa zero brain kama Steve kukisemea chama na serikali ni dharau kubwa kwa wapiga kura. Yaani maprofesa na wanazuoni wengine hawapo CCM hadi chama kiwatumie zero brain? Hii ni hujuma ya wazi kwa uongozi wa mama.
 
Your browser is not able to display this video.
 
Steve Mengele ni mkurugenzi wa taasisi ya mama ongea na mwanao🤣
 
Mkuu,

Hizi habari za Samia kuhujumiwa zingeweza kuwa na mashiko kama Samia mwenyewe tungemuona smart.

Samia mwenyewe mjinga, anajihujumu mwenyewe kabla ya mtu yeyote kumhujumu.

Kashindwa hata kujitengenezea "plausible deniability" kwenye utekaji.

Huyu ni mtu anayeshindwa kwa sababu anahujumiwa au kwa sababu yeye mwenyewe ni mjinga tu?

Kama anahujumiwa yeye mwenyewe hajui kuchuja mambo? Mbona ana taasisi kubwa tu yenye mkono mrefu sana?
 
Top brass yote inayomzunguka ndiyo wanaomhujumu kutomshauri sawasawa ama kumpotosha!

Yanayofanywa kwa sasa, hata hao wanaojifanya kukaa kimya sisi wananchi tunawaona kama wanaunga mkono ama kuyafurahia matendo haya ya kuumiza wananchi, ni viongozi wasiofaa kabisa.

Hata wale waliojitokeza kubweka wakati wa Magufuli na sasa wanajifanya kuufyata, ndiyo hao hao ambao hatutaki hata kusikia habari zao.

Viongozi wastaafu pamoja na viongozi wote wa dini waliojitokeza kutusemea wananchi, tumezitambua dhamira zao pamoja na juhudi zao, tunawapa shime na Mungu atawabariki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…