Ikulu, Chamwino: Rais Magufuli aapisha Baraza la Mawaziri. Awapunguzia adhabu wafungwa waliohukumiwa kunyongwa

Ikulu, Chamwino: Rais Magufuli aapisha Baraza la Mawaziri. Awapunguzia adhabu wafungwa waliohukumiwa kunyongwa

ila tuongee jambo hapa..kama umehukumiwa kunyongwa kwanini usitoroke? Maana huna cha kupoteza
Bora upigwe risasi ukiwa unakimbia kuliko kusikilizia maumivu ya kamba.
 
Saidi Bagaile huyo na hajakubali matokeo yuko chimbo anataka kupindua meza kibabe hadi mtu ameshindwa kuapa, Mzee wa makafara siyo wa spoti spoti
 
Wakuu...
Ebu naomba wajuzi mkuje tuichambue hotuba ya Rais JPM aliposema yafuatayo:-
1. Kuna mmoja alikua akitumia ndege za TANAPA kwenda kwela starehe (nahisi ni Dr Hamisi)...
Kama ametaja ndege za TANAPA huyo atakuwa Hamisi.La kusikitisha ni kuwa JPM alifika Nzega na kumpigia debe Hamisi achaguliwe tena wakati alijua Hamisi ametumia mali ya umma vibaya.Hapo sasa
 
Amesema anasita kuitekeleza hio adhabu kwani atakuwa ndiye muuaji mkubwa pia amesamehe wafungwa Zaidi ya 3000.
Mfalme Daudi aliua maelfu kwa makumi elfu, na bado Yesu Kristo aliitwa mwana wa Daudi, kwa kuwa alitekeleza vyema majukumu yake pale ilipompasa kufanya hivyo. Sheria kama inatoa adhabu na utekelelezaji wa hukumu ya kifo.

Adhabu hii inapaswa kutekelezwa, la sivyo kushindwa kufanya hivyo inahesabika kuwa ni woga, kukosa ujasiri, kushindwa ama kukwepa kwa makusudi kutekeleza majukumu ambayo mtu amepewa kikatiba.

Sent from my Nokia 2.1 using JamiiForums mobile app
 
Amesema anasita kuitekeleza hio adhabu kwani atakuwa ndiye muuaji mkubwa pia amesamehe wafungwa Zaidi ya 3000.
Yeye anasaini, hakuna muuaji bali ni sheria, ndiyo maana tunasema hii nchi inahitaji maombi.
 
Hapa nawaza tu, mfano yule mama aliyewapa sumu watoto wake wawili na kuwauwa kisa ugomvi na mume wake ahukumiwe kunyongwa alafu aachwe kwa msamaha wa rais.
 
hapa nawaza tu, mfano yule mama aliyewapa sumu watoto wake wawili na kuwauwa kisa ugomvi na mume wake ahukumiwe kunyongwa alafu aachwe kwa msamaha wa rais
Ndiyo, na wale majambazi waliomuua Dkt Mvungi kwa kumpiga risasi, wapo 5 na wamesamehewa.
 
Kama ametaja ndege za TANAPA huyo atakuwa Hamisi.La kusikitisha ni kuwa JPM alifika Nzega na kumpigia debe Hamisi achaguliwe tena wakati alijua Hamisi ametumia mali ya umma vibaya.Hapo sasa
 
Kiukweli ninamuunga mkono Rais Magufuli kwenye issue ya matumizi mabaya ya fedha serikalini. Kweli kabisa "mtumishi wa umma" unanunua gari la ofisi la milioni 400 hata roho haikuumi japo kidogo? Halafu unataka kuletewa ufadhili wa kujenga vyoo vya shule visivyozidi milioni 30, ukazindue ukiwa kwenye gari la milioni 400!

Tafadhali sana asiishie kwa huyo tu, kuna wengi tu kwenye sekta ya umma ukiangalia matumizi wanayofanya yasiyo ya lazima unatamani kuwafunua roho uone kama mishipa ya uungwana imekuwa disconnected.

Halafu kuna sera, sheria na kanuni za manunuzi ya ofisi za umma, zinakwama wapi?! Inauma sana!
 
Back
Top Bottom