Ikulu, Chamwino: Rais Magufuli ateua Baraza la Mawaziri lenye Wizara 23. Aunda Wizara mpya ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Ina maana wabunge wote hawakusoma shule!
Wewe unaamini Tanzania nzima kuna waislamu watatu tu ambao waliosoma?
Ndio usomeshe mwanao awe waziri mliwapeleka madrasa saa hizi mnatamani uwaziri, kwanza Waziri akiwa mkiristo unakosa nini?
 
Tuseme basi Wasukuma nao basi hawakutakiwa kuwepo kwa kuwa wanalisha ng'ombe zaidi kuliko kusoma. Hana hoja huyu
 
Kwani.makabila ni hayo tu mawili sukuma na Chaga? Mbona wabende hatuna mtu hapo hata aliyekuwepo hapo nyuma kafurushwa? [emoji23] Lakini tumetulia?
 
Habari njema ni kwamba, Kigwangwala, Shonza, Nape na January wote wametupwa nje. Huenda wakasugua benchi mpaka 2025. Tutakutana nao mitandaoni tu tukironga umbeya, ubuyu, uchechi na kulike twitter za Kigogo.
 
Mmehama kwenye HOJA za kura feki sasa mnarejea katika hisia KONGWE za UDINI ee?!!

Yaani ninyi ni KUHAMISHA MAGOLI TU...

Wangekuwa wako 20 ndipo hapo ROHO YAKO ingekuwa KWATUUU?!!si ndiyo?

Huu ni uzi wa baraza la mawaziri na sio uzi wa uchaguzi. Ziko nyuzi kibao za mambo ya uchaguzi, zinajadili ule ujinga wa mtu mweusi kwenye box la kura.
 
Kwanini
Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya habari wamemweka mtu asiye na background ya aina hiyo yaani Dkt Faustine Ndugulile au nimekosea kuhoji?
 
CCM Mpya inaendelea na "mfumo kristo" siwaoni ndugu zangu wa upande wa pili ktk hawa 23 walio mawaziri kamili, ngoja nirudie kusoma ktk kundi hili la manaibu mawaziri pia labda nitabaini sura ya 'utaifa' kivingine.

Nikiangaza ktk unaibu naona makamanda wastaafu toka chama letu wa'meula', swali kuu ndani ya CCM Mpya bado kunaonekana wale wakongwe wanywa maji ya bendera hakuna 'viongozi' imebidi 'wakodishe majeshi' toka chama kikuu cha upinzani.
 
Vigezooooooo!!!!
Unamaanisha Tanzania nzima kuna waislamu watatu tu Ndio wanakidhi Vigezo vya kua mawaziri???
Anyway I feel sorry kwa waswahili wenzangu waliokuwa wanamshadadia mtu anaeonyesha chuki za dhahiri kwetu
Usisahau kuwa Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu ni sehemu ya Baraza la Mawaziri. Lakini dini siyo mojawapo ya vigezo, na si sahihi kuchunguzana kwa dini, kabila, eneo nk. Pia tusisahau kuwa wanaweza kukidhi 100, 200 je tuwe na baraza kubwa kama hilo?! Hapana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…