Ikulu, Chamwino: Rais Magufuli ateua Baraza la Mawaziri lenye Wizara 23. Aunda Wizara mpya ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Ikulu, Chamwino: Rais Magufuli ateua Baraza la Mawaziri lenye Wizara 23. Aunda Wizara mpya ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Kwenye 23 kuwepo 3 isn't fair,haijawahi kutokea toka uhuru
Acheni inferiority complex Wazee. Hivi jina kuwa la kikristo linamfanya mtu kuwa Mkiristo? By the way, Serikali haina dini. Mtu yeyote anaweza kuwa Waziri bila kujali ana dini au hana.
 
Wizara ya habari na wizara ya teknolojia ya habari mbona ni kitu kilekile au mi ndio sjaelewa
 
Baraza limekamilika? Tuone sasa wale waliokua wanapishana Insta kutuonesha utekelezaji wa miradi ya maendeleo majimboni kwao tangu wameapishwa kama wataendelea
 
Naomba kujua huyu Kwandikwa Waziri wa Ulinzi ana CV gani kwenye jeshi au mambo ya Usalama au katoka uko kama alivyokuwa Hussein Mwinyi, Daktari wa Mifupa kisha Waziri wa Ulinzi.
 
Matangazo ya moja kwa moja kutoka Ikulu, Chamwino mkoani Dodoma kuhusu Uteuzi uliyofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli leo tarehe 05 Desemba 2020



========
Rais Magufuli pia amewateua kuwa Wabunge Dkt. Dorothy Gwajima(Alikuwa Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI - Afya) na Dkt. Leonard Chamuliho (alikuwa Katibu Mkuu Uchukuzi).

Pia Rais Magufuli ameunda Wizara mpya ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.

Orodha ya Mawaziri kama ilivyotangazwa na Katibu Mkuu Kiongozi.

1. Wizara ya Maji - Juma Aweso

2. Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo - Innocent Bashungwa

3. Wizara ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Vijana na wenye ulemavu - Jenister Mhagama

4. Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto - Dkt. Doroth Gwajima

5. Wizara ya Uwekezaji ofisi ya Rais - Profesa Mkumbo Kitila

6. Wizara ya Katiba na Sheria - Dkt. Mwigulu Nchemba

7. Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia - Profesa Joyce Ndalichako

8. Wizara ya Mifugo na Uvuvi -Mashimba Mashauri Ndaki

9. Wizara ya Maliasili na Utalii - Dkt. Ndumbalo Damas

10. Ofisi ya Rais TAMISEMI -Suleiman Jaffo

11. Wizara ya Madini - Dotto Biteko

12. Wizara ya Nishati - Dkt. Medard Kalemani

13. Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi - Mhandisi Dkt Leonard Chamuliho

14. Wizara ya Kilimo - Profesa Adolph Mkenda.

15. Wizara Viwanda na Biashara - Mwambie Geofrey Idelphonce

16.Wizara ya Mambo ya Ndani - George Simbachawene

17. Wizara ya Muungano na Mazingira - Ummy Mwalimu

18. Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya habari - Dkt Faustine Ndugulile

19. Wizara ya Fedha na Mipango - Dkt. Philip Mpango

20.Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki - Profesa Paramagamba Kabudi

21. Wizara ya Ardhi na Makazi -William Lukuvi

22. Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa - Elias John Kwandikwa

23. Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora - Capt Mstaafu George Mkuchika

Katika mawaziri wote na manaibu wao waislamu ni takriban 3% tu. Na ukiacha wizara muhimu kama TAMISEMI na fedha hata hao waislamu kidogo wametupwa kama kwenye wizara kama za sanaa, muungano na mazingira!
 
NAIBU WAZIRI

Biashara - Silaoneka

Ardhi - Anjelina
Mabula

Kazi - Patrobas Katambi

Mambo ya ndani - Hamza

Fedha - Mwanaidi

Sayansi - Kipanga

TAMISEMI- Festo john

Nishati - Biabati

Utumishi- Ndejembi

Mawasiliano- Engineer Kundo

Mifugo na Uvuvi- Philipo

Madini - Ndulanye

Ujenzi - kasekenya

Ulemavu - Ummy
Nderiananga

Maji - Prisca Mahundi

Sanaa - Abdalah Ulega

Mazingira - Mwita witara

EAC - William Openshaw

Utalii- Marry Masanja

Tamisemi - Ernest

Kilimo - H Bashe

Afya - Dr Godwin Mollel

Katiba na sheria -Geofrey Mizengo Pinda
 
Katika baraza hili lenye mawaziri 23 kwa haraka haraka
-Wanawake 4 (wanaume 19)
-?Waislamu 2 (?Wakristo 21)
-Mchaga 1 (Wasukuma 5+)
-Mzanzibar 0 (watanganyika 23)
Vipi wangoni, wakurya, wakwere, waha, wahehe?
 
Back
Top Bottom