Kulingana na katiba Ya Kenya, rais hana mamlaka Ya kukataa maamuzi Ya bunge. Mswaada umeshapitishwa na bunge Rais ana option mbili tu. Ya kwanza anaweza kuurudisha bungeni Kwa ajili Ya marekebisho machache na si kuufuta.. Pili ni kuusaini au aache. Kwa mujibu wa katiba Ya Kenya Rais hata asipousaini baada Ya siku 14 utakuwa sheria. Kabla Ya bunge kuupitisha Rais alipaswa kulishawishi bunge kuufutilia mbali mswaada huo. Ndiyo maana waandamanaji wanataka kumng'oa rais Kwa sababu anacheza na akili za wakenya.