Ikulu chini ya Ulinzi Mkali Nchini Kenya

Bora sisi huwa ikitokea fujo wanawapelekea wale wa ukonga wapashe kwanza kidogo ndiyo waingie mzigoni, sasa kenya wameruhusu kwa raia
Yeah Baba Bora huku wamewapa kipaombele Wazee wa hizi kazi sio kuruhusu kila mtu ale mirungi na Bange ni hatari wote mnakua mazombie
 
Kwamba wewe raia wa mchamba wima utambue uwepo wa big fishes ila rais wa nchi pamoja na kitengo cha usalama wa taifa la kenya wameshindwa kubaini,wewe noma saaaaaaaana
 
Kwamba wewe raia wa mchamba wima utambue uwepo wa big fishes ila rais wa nchi pamoja na kitengo cha usalama wa taifa la kenya wameshindwa kubaini,wewe noma saaaaaaaana
Mchambawima unapachukulia poa sana? Ndiyo comment na wewe wa Maguruwe na Tandika Kaburi moja ndiyo ume comment kichwakichea ukijifanya unajua zaidi
 
Kulingana na katiba Ya Kenya, rais hana mamlaka Ya kukataa maamuzi Ya bunge. Mswaada umeshapitishwa na bunge Rais ana option mbili tu. Ya kwanza anaweza kuurudisha bungeni Kwa ajili Ya marekebisho machache na si kuufuta.. Pili ni kuusaini au aache. Kwa mujibu wa katiba Ya Kenya Rais hata asipousaini baada Ya siku 14 utakuwa sheria. Kabla Ya bunge kuupitisha Rais alipaswa kulishawishi bunge kuufutilia mbali mswaada huo. Ndiyo maana waandamanaji wanataka kumng'oa rais Kwa sababu anacheza na akili za wakenya.
 
Unataka kusema kwamba hao waandamanaji hawajui wanachokitaka? Maana madai ya ni kutosaidiwa kwa ile Bill hadi ifanyiwe marekebisho na ndicho alichofanya Ruto, hajafuta bali hajau sign na anauridisha bungeni ili bungeni akiwa ameweka mapendekezo kama wanavyodai hao Generation Zombies.
Hapo anachezaje na akili zao?
 
Unajua kusoma kweli wewe!? Waandamanaji wanataka mswaada wote uondolewe na si kufanyiwa marekebisho. Mapendekezo Ya kuufanyia marekebisho yalishafanyika mwanzo tu wa maandamano hayo. Waandamanaji hawautaki mswada wote.. Na alichokisema ruto kwenye hotuba yake Ya jtano tarehe 26 June anataka bunge liufute mswada wote kitu ambacho hakiwezekani. Na hata asiposaini Mswada utakuwa sheria baada Ya siku 14. Sijui utakuwa umeelewa!? Soma uelewe badala Ya kukombilia ku-comment.
 
1. Kinachopingwa kwenye muswada ule ni ongezeko la kodi Kenya anti-tax protests unveil youth verve that could change region’s future politics | The East African
Kama ongezeko la kodi ndiyo linapingwa katika muswada huo wa fedha maana yake kuna maeneo ya kurekebisha.

2. Bahati nzuro umejikanusha, maana uliongelea habari za Ruto kufuta muswada, ila hapa umesema ameliagiza bunge kufuta (siyo Ruto tena) so hilo nitakuacha.

3. Kilichopitishwa na bunge ili rais aweke sign ikatokea kimeshindikana kusainiwa na kikarudishwa bungeni basi binge ndiyo litakitengua, kwa kuwa bunge lina hayo mamlaka.
Ndiyo maana, hata sheria zinazotungwa na bunge, watu wana ruhusiwa kwenda kuzioinga mahakamani, ikitokea mahakama ikaona hoja ya walalamikaji na kuwapa ushindi, sheria hiyo hurudishwa bungeni, hao ndiyo wenye mamlaka ya kutunga sheria nyingine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…