Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu (DPC),
Zuhura Yunus akizungumza na Vyombo vya Habari Ikulu jijini Dares Salaam leo Tarehe 12 Novemba, 2022
Ningependa tu kwa niaba ya Rais kutoa pole kwa wafiwa wote wa ajali ambayo ilitokea ya kampuni ya Precision Air iliyokuwa ikitokea jijini Dar es Salaam kuelekea Bukoba. Kwa taarifa tu kutakuwa na mkutano wa dharura tarehe 14, siku ya Jumatatu, jijini Dodoma, utakaojadili zaidi janga hilo.
ZIARA YA KIHISTORIA
Na sasa baada ya taarifa hiyo tuelekee katika ziara yenyewe. Kama mnavyojua Mh. Rais kuanzia tarehe 2 - 4 mwezi huu Novemba, alikwenda nchini China kwa mwaliko maalum wa Rais wa nchi hiyo Xi Jinping. Ziara hiyo ilikuwa ni ya kihistoria. Hakika, ni kwasababu ni ziara iliyofanywa na kiongozi wa juu kutoka barani Afrika tangu kumalizika kwa mkutano wao wa 20 wa Chama cha Kikomunisti cha China (CCCP).
ZIARA YA KWANZA YA KIONGOZI WA AFRIKA TANGU COVID-19
Vilevile, ziara hizo ni miongoni mwa za kwanza kabisa tangu lile janga la COVID-19. Yeye ndiyo kiongozi wa kwanza kabisa wa Afrika kutembelea nchi hiyo; kama nilivosema kwa mwaliko wa Rais mwenyewe - Xi Jingping.
Kwa ujumla wake, ziara ilienda salama; ilikuwa nzuri sana. Na mbali na kukutana na mwenyeji wake Xi Jingping, vilevile alikutana na Waziri Mkuu wa China na pia Spika wa Bunge la China. Kwahiyo, alikutana na viongozi wa nafasi zote - karibia - za juu.
USHIRIKIANO WA CHINA-TANZANIA
Kwa kifupi tu nitaelezea mafanikio. Kwanza, ni suala la kidiplomasia. Kulikuwa na mazungumzo ya kina sana hapa, hasa China na Tanzania kuendeleza ushirikiano, hasa kwakuwa nchi hizo tayari zianashirikiana katika masuala ya kimataifa na kikanda.
USHIRIKIANO WA KIMKAKATI
Na vilevile, walikubaliana kupandisha hadhi mahusiano yao - yaani baina ya China na Tanzania ili kuwa na ushirikiano wa kina na kimkakati katika nyanja zote. Kwa Kiingereza wanaita Comprehensive Strategic Cooperative Parternership. Hilo ni muhimu sana kwasababu maana yake ni nini; ni kwamaba nchi hizo zitakuwa na mawasiliano ya mara kwa mara muda wowotw kwa maslahi mapana ya nchi zote mbili.
Na vilevile, ushirikiano wa nchi hizo mbili katika nyanja mbalimbali yanakuwa yakipewa kipaumbele... na ndiyo maana kupandisha hadhi ushirikiano huo lilikuwa ni jambo kubwa sana na la muhimu.
UAGIZAJI WA BIDHAA KUTOKA TANZANIA
Kiuchumi ni kwamba wameongeza zaidi uagizaji wa bidhaa kutoka Tanzania. Kwahivyo, wafanyabiashara wetu wa Kitanzania watanufaika na hilo hasa katika bidhaa zetu za kilimo, mifugo uvuvi na madini.
KUTOTOZA USHURU KWA 98% BIDHAA ZINAZOTOKA TANZANIA
N vilevile China imeahidi kutotoza ushuru kwa 98% ya bidhaa zinazosafirishwa kutoka Tanzania kwenda China. Kwahiyo, bila shaka hilo ni jambo la msingi sana na lenye faida kwa wafanyabiashara wa Tanzania.
KUONGEZA UWEKEZAJI
China, vilevile, imeahidi kuongeza uwekezaji wa hapa Tanzania kwa kupitia makampuni yao ya China ili kuchangia maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika nchi yetu.
UJENZI WA VIWANDA
Zimekubaliana pia ushirikiano katika ujenzi wa viwanda ili kuiongezea nchi yetu uwezo katika uzalishaji, usindikaji na utengenezaji wa bidhaa mbalimbali.
UCHUMI WA KIDIGITALI
Na wakubaliana kukuza ushirikiano kwenye Uchumi wa Kidigitali - yaani
Digital Economy; Uchumi wa Bluu (
Blue Economy) na Maendeleo ya Kijani (
Green Development) - ambayo kwa kifupi ni dhana ya kuhakikisha kwamba utekelezaji wa miradi mbalimbali unazingatia suala la mazingira.
KUFUFUA RELI YA TAZARA
Na pia miongoni mwa miradi ambayo wamejadili na bado mazungumzo yanaendelea, lakini wako tayari kuiunga mkono Tanzania, ni kutekeleza mradi wa kufufua Reli ya TAZARA.
ULINZI NA USALAMA
Nchi zote zimekubaliana kuimarisha ushirikiano ili kudumisha amani na usalama.
MASUALA YA KIJAMII
Mwaka 2024 nchi zote mbili zitaadhimisha miaka 60 ya mahusiano ya kidiplomasia; kwahiyo wamekubaliana kuwa uwe mwaka wa utalii wa utamaduni wa China na Tanzania. Namna ambavyo itakuwa tutajua baadaye lakini mwaka 2024 nchi zote mbili zitashirikiana katika hilo.
UFADHILI WA MASOMO
China wameahidi kutoa ufadhili wa masomo kwa wanafunzi wa Kitanzania zaidi kwasababu tayari wanatoa, lakini ziada.
TIMU ZA MATIBABU
Na vilevile wameahidi kupeleka timu za matibabu Tanzania Bara na vilevile Zanzibar.
USHIRIKIANO WA KIMATAIFA
Mambo mengine ambayo wamezungumzia ni Ushirikiano wa Kimataifa ambao wamekuwa nao lakini wataongeza.
UTIAJI SAINI HATI ZA MAKUBALIANO 15
Jambo lingine kubwa ni utiaji saini Hati za Makubaliano mbalimbali, mikataba. itifaki pia. Jumla zilitiwa saini Hati za Makubaliano 15:
1. Fursa Zinazopatikana
i. Wakulima wa Tanzania - hasa wanaolima zao la parachichi, sasa wamefunguliwa fura kabisa ya kuuza maparachichi katika soko kubwa la China.
ii. Wavuvi wa Tanzania - hasa wanaofanya biashara ya kuuza mabondo ya samaki. Nao wamefunguliwa fursa ya kuuza bidhaa zao katika soko kubwa la China. Awali, kama mnavyojua, wauzaji wa mabondo walikuwa wanauza bidhaa zao katika la China lakini ilikuwa lazima wapitie nchi ya Vietnam. Lakini sasa, kuna makubaliano haya - itakuwa moja kwa moja.
2. Sekta ya Utalii
Sekta ya Utalii natyo imepata manufaa. Wamepata msaada wa kujenga Makumbusho ya kisasa ya kutunza nyayo za binadamu wa kwanza wenye umri wa miaka milioni 3 zilizopo katika Hifadhi ya Ngorongoro.