Ikulu, Dar: Rais Samia akutana na Freeman Mbowe

figganigga

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
25,724
Reaction score
55,906

Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan leo amekutana na kuzungumza na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Freeman Mbowe Ikulu Mkoani Dar Es Salaam.

Rais Samia amesisitiza kuwa kuna umuhimu wa kushirikiana ili kuijenga Tanzania kwa kuaminiana na kuheshimiana kwa misingi ya haki.

Mhe. Mbowe amemshukuru Rais Samia kwa kuonesha kwake kujali huku akikubali kuwa msingi mkubwa wa kujenga taila la Tanzania ni kusimama katika haki.

Vile vile, amesema wamekubaliana kufanya siasa za kistaarabu na kiungwana na kuwa yuko tayari kushirikiana na Serikali katika kuleta maendeleo ili nao pia waweze kutekeleza majukumu yao ipasavyo.

Your browser is not able to display this video.

Your browser is not able to display this video.
====

Picha Mbalimbali zikimuonesha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na kuzungumza na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe alipowasili Ikulu Jijini Dar Es salaam leo tarehe 04 March 2022

 
Tunategemea chadema itaendelea na mapambano ya kudai Haki na uhuru wa vyama vingi hili likishindikana basi tena tujiunge wote na ccm tu hakuna namna. Kwahiyo mwenyekiti pamoja na yote mliyozungumza na Rais samia leo baada ya kutoka gerezani hilo naomba uliweke akilini.
 
Usiogope!
 
Naiona Tanzania Mpya hii hapa...
Mwendazake alituelekeza mkondo wa kuzimu!
Sasa tushikamane sote tudai uhuru kamili tusonge mbele na ujenzi wa taifa letu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…