Tena alikuwa anataka afanye ufunguzi hata wa kisima cha maji, anapiga push ups nayo inakuwa habari.
Alikuwa anatembea na maburungutu ya fedha kama papaa, anakula kijiweni nayo habari, Mara ananunua mapapai nayo inakuwa habari.
So heri mama anafanya Mambo ya maana sio kupiga push ups na kutafuna mahindi na kununua kuku barabarani.
Kwa kweli marehemu aliwadharau sana Watanzania.
Kwa zaidi ya 90% siasa zake zilikuwa za uwongo na hila. Alifurahia sana uwepo wa wajinga wengi maana hao aliwafanya mayeka wake.
Wakidanganywa, ndani ya makinikia kuna dhahabu 90%, wanashangilia. Akiwadanganya, Tanzania ina uwezo wa kusaidia Ulaya,wanashangilia. Akiwadanganya kuwa yeye ndiye aliyejenga kilometa nyingi za lami kuliko awamu nyingine yoyote, wanashangilia. Akiwadanganya kuwa utawala wake ndio wa kwanza kununua ndege nyingi, wanashangilia.
Utawala wa marehemu ulifanya maovu mengi kuliko mema. Tufanye jitihada na tumwombe Mungu, isitokee kipindi hata kimoja, Taifa letu likaangukia kwenye utawala unaofanana na wa marehemu.
Tunakushukuru Mungu maana aliyaona machozi ya Watanzania. Tuliomba tupate kiongozi mzuri, tuliomba utuondolee kiongozi dhalimu na dhulumati. Hatukuomba kifo. Lakini kama hekima yako iliona ndicho kilicho heri kwa wengi wenye kudhulumiwa na ambao wangeendelea kudhulumiwa, ni nani sisi hata tuihoji hekima yako?
Tunakushukuru Mungu maana mtawala alikuwa tayari kutesa na kuua walio wengi wenye kumkosoa na waliotaka mabadiliko, wewe mkuu mwenye hekima, kwa kuwapenda watu wako, ukayaleta bila hata ya tone moja la damu kupotea. Huenda tumeshukuru kidogo kwa kuwaokoa walioteseka, na kwa hilo tunaomba usituhesabie kosa maana sisi ni dhaifu wa akili na mioyo. Daima tunahitaji msaada wako. Daima tunaomba kilicho chema katika maisha yetu, japo kuna wakati hata hatujui ni kipi kilicho chema.