Ikulu Dar: Rais Yoweri Museveni na Rais Samia Suluhu washuhudia utiaji saini wa mikataba ya utekelezaji wa mradi wa bomba la mafuta

Ikulu Dar: Rais Yoweri Museveni na Rais Samia Suluhu washuhudia utiaji saini wa mikataba ya utekelezaji wa mradi wa bomba la mafuta

Rais wa Jamhuri ya Uganda, Mhe. Yoweri Kaguta Museveni leo tarehe 20 Mei, 2021 atafanya ziara ya kikazi ya siku 1 hapa nchini kwa Mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan...
Duh hizi sign sasa zinachosha, hii itakuwa labda ya 5.Tuomba mfike mwisho kazi ianze.
 
Mambo ya Gas anasaini mtu ambae mkataba wetu wa kuwepo yeye hapa unakataza mambo ya Gas na Mafuta kuwepo ndani.
 
Rais wa Jamhuri ya Uganda, Mhe. Yoweri Kaguta Museveni leo tarehe 20 Mei, 2021 atafanya ziara ya kikazi ya siku 1 hapa nchini kwa Mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Akiwa hapa nchini Mhe. Rais Museveni na Mhe. Rais Samia watashuhudia utiaji saini wa mikataba ya utekelezaji wa mradi wa bomba la mafuta la kutoka Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga nchini Tanzania kati ya Serikali ya Tanzania na kampuni za uwekezaji katika mradi huo (Host Government Agreement) utakaofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam kuanzia saa 4:00 asubuhi.

FB_IMG_1621489669508.jpg
 
Mkuu ebu tueleweshe Hii Saini Saini Ya Huu Mkataba. Maana nikikumbuka Hii Ni Mara ya 3 o 4 Mkataba wa Hili Bomba Unasainiwa.
Hii project sio ndogo na sio ya muda mfupi. Kuna siasa nyingi lazima ziwekwe sawa. Nchi za Afrika hatuaminiki, ndio maana kuna guarantee nyingi za kuwapa.

Kama nchi hazina Bilateral Investment Agreement i.e makubaliano ya kulinda uwekezaji wa makampuni kutoka nchi fulani, ndio wanakuja na hii Host Government Agreement, yaani serikali lazima ifanye commitment kuhusu uwekezaji wa hao wageni.

Ndio humu kuna misamaha ya kodi etc. Na huu mradi una upinzania sana, hata mabenki yanagwaya kutoa fedha, naona ndio maana inabidi hizi high level propaganda ziwepo kuonyesha kuwa nchi ziko serious na hili jambo na kuna usalama wa mradi.
 
Usishangae ukisikia kuwa Uhuru Kenyatta nae atafanya ziara ya kikazi ya siku moja hapa kesho...
 
Mbona mikataba imekuwa mingi hivi. Kila mara ni kusaini mikataba ya bomba la mafuta.
 
Duh hizi sign sasa zinachosha,hii itakuwa labda ya 5.Tuomba mfike mwisho kazi ianze.
Itakuwa kama safari ya kuhamia Dodoma ilikuwa na story nyingiiiiiii
Awamu ya kwanza haikufanikiwa
Awamu ya pili nayo ikakwama
Awamu ya tatu haikusumbuka nalo
Awamu ya nne haikutaka kabisa kusikia habari hiyo 🤣
 
Nilikuwa nategemea kusikia kazi ya ujenzi imeanza na sio kutia kidole...
 
Rais wa Jamhuri ya Uganda, Mhe. Yoweri Kaguta Museveni leo tarehe 20 Mei, 2021 atafanya ziara ya kikazi ya siku 1 hapa nchini kwa Mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan...
Saini MARA YA TATU, ama kipindi kile JIWE alikuwa anaendaga kufanyanniin huko kenya na uganda?
 
Hawa walioapishwa kuwa wakuu wa mikoa jana hapo kwenye viti wanasubiri nini?, walitakiwa wawe wanapokelewa leo ofisini!.
Siasa zetu tunazijua wenyewe.
 
Back
Top Bottom