Ikulu Dar: Rais Yoweri Museveni na Rais Samia Suluhu washuhudia utiaji saini wa mikataba ya utekelezaji wa mradi wa bomba la mafuta

Ikulu Dar: Rais Yoweri Museveni na Rais Samia Suluhu washuhudia utiaji saini wa mikataba ya utekelezaji wa mradi wa bomba la mafuta

Viongozi wa kiafrika bwana kila siku kama si kuzindua basi kusaini jambo moja kila muda.

Kwani mama alivyoenda safari ya kwanza Uganda akusaini au karatasi zilikuwa zimeisha?
 
Viongozi wa kiafrika bwana kila siku kama si kuzindua basi kusaini jambo moja kila muda.

Kwani mama alivyoenda safari ya kwanza Uganda akusaini au karatasi zilikuwa zimeisha?
Hahahaha mkuu ivi ww unaweza kwenda kujadili mambo ya ndani ya ndoa yako kwa jiran yako ? Huo ni uchulooo
 
M7 ni msanii kichizi,aliwahi kupewa bandari kavu huko tanga mpk leo sijui mwaka wa ngapi huu hata kuiwekea kibanda cha nyasi hajawahi
 
Viongozi wa kiafrika bwana kila siku kama si kuzindua basi kusaini jambo moja kila muda.

Kwani mama alivyoenda safari ya kwanza Uganda akusaini au karatasi zilikuwa zimeisha?
Mara moja moja chekelea ikiisha akili hua zinawarudia.
 
Rais wa Jamhuri ya Uganda, Mhe. Yoweri Kaguta Museveni leo tarehe 20 Mei, 2021 atafanya ziara ya kikazi ya siku 1 hapa nchini kwa Mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Akiwa hapa nchini Mhe. Rais Museveni na Mhe. Rais Samia watashuhudia utiaji saini wa mikataba ya utekelezaji wa mradi wa bomba la mafuta la kutoka Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga nchini Tanzania kati ya Serikali ya Tanzania na kampuni za uwekezaji katika mradi huo (Host Government Agreement) utakaofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam kuanzia saa 4:00 asubuhi.

========

Shughuli inaanza kwa nyimbo za Taifa na wimbo wa Afrika Mashariki. Gerson Msigwa anaanza kwa kutoa ufafanuzi wa wingi wa mikataba inayosainiwa kwenye bomba hilo.

Msigwa amefafanua mkataba wa leo ni makubaliano kati ya nchi ya Tanzania na kampuni itakayotekeleza mradi, amesema miradi mikubwa kama huu wa mafuta unaohusisha zaidi ya pande moja huambatana na utiaji saini wa mikataba kadha kadha hivyo hakuna kujirudia kwa utiaji saini wa mikataba.

Mkataba wa bomba la mafuta umetiwa saini na waziri wa nishati, Medard Kalemani shuhuda akiwa mwanasheria mkuu wa Tanzania, Prof. Kilangi na kwa upande wa kampuni ya EACOPP ni mkuregunzi mkuu wa kampuni hiyo, Martin John na atashuhudiwa na rais wa utafiti na uzalishaji wa Total Afrika, Nicholaus Teraz.

========

Pia soma

kila siku kutia sahihi ?
 
Mkuu ebu tueleweshe Hii Saini Saini Ya Huu Mkataba. Maana nikikumbuka Hii Ni Mara ya 3 o 4 Mkataba wa Hili Bomba Unasainiwa.
Unamuuliza kapuku suala la kiserikali hebu jiongeze basi kiakili

Nadhani saizi majibu unayapata mubashara
 
Mkataba wa bomba la mafuta umetiwa saini na waziri wa nishati, Medard Kalemani shuhuda akiwa mwanasheria mkuu wa Tanzania, Prof. Kilangi na kwa upande wa kampuni ya EACOPP ni mkuregunzi mkuu wa kampuni hiyo, Martin John na atashuhudiwa na rais wa utafiti na uzalishaji wa Total Afrika, Nicholaus Teraz.
Mbona hawa hawajatajwa na wapo hapo

Akiwa hapa nchini Mhe. Rais Museveni na Mhe. Rais Samia watashuhudia utiaji saini wa mikataba ya utekelezaji wa mradi wa bomba la mafuta la kutoka Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga nchini Tanzania kati ya Serikali ya Tanzania na kampuni za uwekezaji katika mradi huo
 
Mwisho wa siku mwenye bomba ni Uganda sisi ni wabembelezaji tuu kutaka wapitishe kwetu wanaweza wakaamua vinginevyo
 
Back
Top Bottom