Ikulu Dar: Rais Yoweri Museveni na Rais Samia Suluhu washuhudia utiaji saini wa mikataba ya utekelezaji wa mradi wa bomba la mafuta

Ikulu Dar: Rais Yoweri Museveni na Rais Samia Suluhu washuhudia utiaji saini wa mikataba ya utekelezaji wa mradi wa bomba la mafuta

Rais wa Jamhuri ya Uganda, Mhe. Yoweri Kaguta Museveni leo tarehe 20 Mei, 2021 atafanya ziara ya kikazi ya siku 1 hapa nchini kwa Mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Akiwa hapa nchini Mhe. Rais Museveni na Mhe. Rais Samia watashuhudia utiaji saini wa mikataba ya utekelezaji wa mradi wa bomba la mafuta la kutoka Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga nchini Tanzania kati ya Serikali ya Tanzania na kampuni za uwekezaji katika mradi huo (Host Government Agreement) utakaofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam kuanzia saa 4:00 asubuhi.

View attachment 1791412
Maeveni is a murderer he should be arrested and locked for life
 
Hapa ndipo Nimeshangaa, Hata Mwendazake pia alishasaini na Huyu Pia akaenda Huko Sasa kusaini Kusaini kusaini Kila Wakati.
Toka 2017 hilo bomba mikataba inasadikiwa tu. Yaani utiaji saini umezidi hata muda wa ujenzi!
 
Hii nenda rudi ya Samia Kampala na Museveni Dar es Salaam inaanza kunitia Shaka ila ngoja kwa sasa niusome Mchezo mzima.
Nauliza tu, hivi rais wa Rwanda yuko wapi, sijamsikia kitambo sana
 
Hivi watia mikataba ngapi, mbona kila siku ni kutia vidole kuanzia enzi ya Hayati?
Au wamebadilisha mkataba baada ya mwenye boma kusepa?
 
Rais wa Jamhuri ya Uganda, Mhe. Yoweri Kaguta Museveni leo tarehe 20 Mei, 2021 atafanya ziara ya kikazi ya siku 1 hapa nchini kwa Mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Akiwa hapa nchini Mhe. Rais Museveni na Mhe. Rais Samia watashuhudia utiaji saini wa mikataba ya utekelezaji wa mradi wa bomba la mafuta la kutoka Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga nchini Tanzania kati ya Serikali ya Tanzania na kampuni za uwekezaji katika mradi huo (Host Government Agreement) utakaofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam kuanzia saa 4:00 asubuhi.

========

Shughuli inaanza kwa nyimbo za Taifa na wimbo wa Afrika Mashariki. Gerson Msigwa anaanza kwa kutoa ufafanuzi wa wingi wa mikataba inayosainiwa kwenye bomba hilo.

Msigwa amefafanua mkataba wa leo ni makubaliano kati ya nchi ya Tanzania na kampuni itakayotekeleza mradi, amesema miradi mikubwa kama huu wa mafuta unaohusisha zaidi ya pande moja huambatana na utiaji saini wa mikataba kadha kadha hivyo hakuna kujirudia kwa utiaji saini wa mikataba.

Mkataba wa bomba la mafuta umetiwa saini na waziri wa nishati, Medard Kalemani shuhuda akiwa mwanasheria mkuu wa Tanzania, Prof. Kilangi na kwa upande wa kampuni ya EACOPP ni mkuregunzi mkuu wa kampuni hiyo, Martin John na atashuhudiwa na rais wa utafiti na uzalishaji wa Total Afrika, Nicholaus Teraz.

========

Pia soma

HILO BOMBA LIMETIWA SAINI (DOLE )MARA NGAPI? NAONA KILA SIKU NI KUTIA SAINI! MBONA MNAVUTA VUTA SANA NINYI WATU? KWANI HAMUWEZI KUSAINI DOCUMENTS ONLINE NA KAZI IKAANZA? DUUH, ANAYEJUA ATUFAHAMISHE HIZI SAINI NI ZA NINI? MBONA WALISHASAINI MARA NYINGI? ANY IDEA?
 
Hapana siwezi mkuu.
Kama huwezi basi ndionmaana mkataba wa Tz umekuka sainiwa Tz, kuna kitu kinaitwa triple parties, mradi huu ndugu unapelekea kuanzishwa kwa kampuni ya shea serikaki ya Tz , UG, na Total... (Kama sijakosea) so wana hisa wana ingia mikataba kuanzishwa kwa kampuni iyo EACOP.
 
Back
Top Bottom