Ikulu Dar: Rais Yoweri Museveni na Rais Samia Suluhu washuhudia utiaji saini wa mikataba ya utekelezaji wa mradi wa bomba la mafuta

Ikulu Dar: Rais Yoweri Museveni na Rais Samia Suluhu washuhudia utiaji saini wa mikataba ya utekelezaji wa mradi wa bomba la mafuta

Guys Energy security is one of those matters which is at the intersection of both national interest and national security. We need to up our game.
 
Rais wa Jamhuri ya Uganda, Mhe. Yoweri Kaguta Museveni leo tarehe 20 Mei, 2021 atafanya ziara ya kikazi ya siku 1 hapa nchini kwa Mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Akiwa hapa nchini Mhe. Rais Museveni na Mhe. Rais Samia watashuhudia utiaji saini wa mikataba ya utekelezaji wa mradi wa bomba la mafuta la kutoka Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga nchini Tanzania kati ya Serikali ya Tanzania na kampuni za uwekezaji katika mradi huo (Host Government Agreement) utakaofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam kuanzia saa 4:00 asubuhi.

========

Shughuli inaanza kwa nyimbo za Taifa na wimbo wa Afrika Mashariki. Gerson Msigwa anaanza kwa kutoa ufafanuzi wa wingi wa mikataba inayosainiwa kwenye bomba hilo.

Msigwa amefafanua mkataba wa leo ni makubaliano kati ya nchi ya Tanzania na kampuni itakayotekeleza mradi, amesema miradi mikubwa kama huu wa mafuta unaohusisha zaidi ya pande moja huambatana na utiaji saini wa mikataba kadha kadha hivyo hakuna kujirudia kwa utiaji saini wa mikataba.

Mkataba wa bomba la mafuta umetiwa saini na waziri wa nishati, Medard Kalemani shuhuda akiwa mwanasheria mkuu wa Tanzania, Prof. Kilangi na kwa upande wa kampuni ya EACOPP ni mkuregunzi mkuu wa kampuni hiyo, Martin John na atashuhudiwa na rais wa utafiti na uzalishaji wa Total Afrika, Nicholaus Teraz.

Rais Samia Suluhu Hassan
“Rais Museveni sio Mgeni Tanzania, ameishi hapa, amepata Elimu yake ya Chuo Kikuu hapa na hata baadhi ya Watoto wake amepatia hapa kwahiyo huyu ni nusu Mtanzania na nusu Mganda, tunamkaribisha sana”

“Hayati Magufuli na Museveni walianza mchakato wa mradi huu wa ujenzi wa bomba la mafuta la Hoima - Tanga na Mimi nimekuja kuuendeleza, mradi huu una faida nyingi ikiwemo pia kuwapatia ajira Wananchi wetu”

“Nakushukuru Rais Museveni kwa kuja licha ya changamoto ya Corona, asante nilikuwa na wasiwasi ila umenithibitishia nyumbani ni nyumbani,najua umekuja kutokana na uzito wa mradi huu wa bomba la mafuta, Watanzania wamesikia maneno kwa miaka 5 tuache maneno tukatekeleze”

“Kuna mambo yanashangaza kulikuwa na sheria wote tusajili laini tuweke vidole ili Mtu akifanya utapeli ajulikane lakini utapeli wa mtandao unaendelea na Watu hawafikishwi Mahakamani, sasa ule usajili ulikuwa kiini macho au nini!? Maana wote tumesajili na majina yapo.

Yoweri Museveni
“Mimi naelewa kiswahili lakini nimesafiri na Wazungu weusi nilionao hapa kutoka Uganda wanajifanya hawaelewi Kiswahili na masikio yanawauma kwa vitu walivyoweka masikioni”

“Sekta muhimu nne ni Kilimo ambacho utapata chakula na utajiri, sekta ya pili ni viwanda, sekta ya tatu ni service (huduma), sekta ya nne ni ICT, sekta hizi zinataka miundombinu kama barabara, umeme, nishati na hizi sekta zote haziwezi kuendelea bila soko”

“Wananchi wa Uganda na Tanzania wasilewe na sekta ya mafuta na gesi wakasahau sekta nyingine kama kilimo, ICT, viwanda n.k, kwasababu mafuta yanaisha lakini kilimo, utalii vinaendelea kwahiyo tutumie rasilimali zenye ukomo kuendeleza rasilimali endelevu”

========

Pia soma

Hii nchi ina viongozi WA hovyo Sana basi Tu,
Mnatoa gesi hapa mnaipeleka Kenya alfu muda huo huo unawakamata wananchi wako na magunia ya mkaa.
Kama hamtaki tutumie mkaa mtuachie Hy gesi, mwenda zake alikuwa na akili Sana.
Ni Mambo ya hovyo Sana,nlifiki labda Hy gesi ingefanyiwa utaratibu ichimbwe hapa ili wananchi waepuke matumizi ya mkaa, unawapelekea watu Alf bado unakamata watu Kwa kuntumia mkaa....🤣🤣🤣 Ni wendawazimu
 
Hapa ndipo Nimeshangaa, Hata Mwendazake pia alishasaini na Huyu Pia akaenda Huko Sasa kusaini Kusaini kusaini Kila Wakati.
hapa ndio nimejua watz wengi si waelewa wa mambo na shule ni ndogo sana. hebu tafuta hata articles google ujifunze kidogo kipi kilisainiwa na bado nini na nini
 
ngoja niwajuze watu hapa msiojua hii mikataba iliosainiwa.
2017 mu7 na magufuli walisaini mkataba wa awali unaitwa MOU (memorandum of understanding). huu ni non binding agreement. yaani mtu anaweza jitoa mda wowote akitaka

chato: mu7 na JPM waka initialize miakataba wa HGA (host government agreement). yaani makubaliano ya mwanzo kuwa UG na Tz wamekubaliana kutekeleza huu mradi kwa pamoja na TZ itakuwa na hisa asilimia 5%

Samia, mu7, Total na CNOOC in uganda: mikataba 3 ilisainiwa, yaani tripertite, a) TTA transportation tax agreement- makubaliano ya usafirishaji mafuta b) SHA - share holders agreement- wenye share ya bomba ni Ug 15%, TZ, 15%, TOTAL na CNOOC wanagawanabhizo zilizobaki. c) HGA agreement, uganda, total na cnooc walikubaliana ( kumbuka hga,ya UG samia hauhusika sababu haikumuhusu.

Leo: TZ, total, CNOOC, wamesaini HGA, TZ leo wamekubali rasmi kuchua shares 15% na imekubali kutekelwza yote yaliofikiwa k.m kutoa ardhi, security, pesa ili wapewe hiyo 15%. nakaribisha maswali
 
TTA ni TARRIF TRANSPORTATION AGREEMENT
 
Kazi iendelee na kupigwa juu yaani na kusaini kote huko tunaambulia ka 5% tu.
Mbali ya hiyo 5% mkuu usisahau hapo kuna ajira, kuna fidia tutapata kwa mtu mmoja mmoja na serikali pia.
Kuna biashara pia, Mama lishe, wauza matunda nk.
Wakati wa ujenzi wa hilo bomba kutakuwa na mzunguko mkubwa wa pesa ambao tutanufaika nao.
 
Rais Samia pengine anao umri wa mama yako mzazi. Jaribu uwe na adabu japo za kinafiki.

Watu wa aina yako ndio mnaoanzisha uzi wa kudharau serikali ya sasa kila siku, ujumbe wenu wa msingi kabisa ni akili za kipumbavu kama hizi.
lighten up JF police. It was all written in good spirit. If at all you felt offended ungepita kimya kimya.
 
lighten up JF police. It was all written in good spirit. If at all you felt offended ungepita kimya kimya.
Siwezi kuwa offended ila naamini wapo wengi wasiopenda udhalilishaji wa jinsia ya kike.

Humu kuna wengine ni vijana wadogo sana wanapoingia katika majukwaa kama haya na kukutana na lugha za dhihaka tena zenye kuelekezwa kwa Rais wa nchi wanalidharau jukwaa hili na wote tunaoandika michango ya maoni yetu.
 
HAYA NISAMEHE BWANA BUKILILO. SITORUDIA TENA KUFANYA DHIHAKA.

Happy?????
 
Hapa ndipo Nimeshangaa, Hata Mwendazake pia alishasaini na Huyu Pia akaenda Huko Sasa kusaini Kusaini kusaini Kila Wakati.
Tupo pamoja kimawazo, mkataba huu unasainiwa mara tatu mwenye ujuzi wa mambo haya hatueleze me sielewi kuhusu huu mkataba wa bomba la mafuta.
 
hapa ndio nimejua watz wengi si waelewa wa mambo na shule ni ndogo sana. hebu tafuta hata articles google ujifunze kidogo kipi kilisainiwa na bado nini na nini
Wewe ndiwe wa hovyo zaidi kuliko huyo jamaa uliyemshutumu.

Kwa vile wewe ni mjuaji ungekosa kitu gani kumuelewesha hayo unayojuwa wewe?
 
Tupo pamoja kimawazo, mkataba huu unasainiwa mara tatu mwenye ujuzi wa mambo haya hatueleze me sielewi kuhusu huu mkataba wa bomba la mafuta.
Nani alikuambia usifuatilie live tukio la utiaji saini ungefuatilia ungejua Sasa tafuta bundle ingia YouTube sikiliza walichokuwa wanafafanua wakubwa
 
JPM alienda Uganda kusaini, Museven akaja dar kusaini, Museven akaja tena Chato kusaini, Samia akaenda Uganda kusaini na sasa Museven kaja Dar kusaini.Wanachofanya hawa viongozi ni kuwapiga wananchi changa la macho.Huwa wanaamini kuwa wananchi ni wajinga kama wao.
 
Back
Top Bottom