Linguistic
JF-Expert Member
- Mar 16, 2021
- 3,669
- 8,268
- Thread starter
- #101
Guys Energy security is one of those matters which is at the intersection of both national interest and national security. We need to up our game.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Rais wa Jamhuri ya Uganda, Mhe. Yoweri Kaguta Museveni leo tarehe 20 Mei, 2021 atafanya ziara ya kikazi ya siku 1 hapa nchini kwa Mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Akiwa hapa nchini Mhe. Rais Museveni na Mhe. Rais Samia watashuhudia utiaji saini wa mikataba ya utekelezaji wa mradi wa bomba la mafuta la kutoka Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga nchini Tanzania kati ya Serikali ya Tanzania na kampuni za uwekezaji katika mradi huo (Host Government Agreement) utakaofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam kuanzia saa 4:00 asubuhi.
========
Shughuli inaanza kwa nyimbo za Taifa na wimbo wa Afrika Mashariki. Gerson Msigwa anaanza kwa kutoa ufafanuzi wa wingi wa mikataba inayosainiwa kwenye bomba hilo.
Msigwa amefafanua mkataba wa leo ni makubaliano kati ya nchi ya Tanzania na kampuni itakayotekeleza mradi, amesema miradi mikubwa kama huu wa mafuta unaohusisha zaidi ya pande moja huambatana na utiaji saini wa mikataba kadha kadha hivyo hakuna kujirudia kwa utiaji saini wa mikataba.
Mkataba wa bomba la mafuta umetiwa saini na waziri wa nishati, Medard Kalemani shuhuda akiwa mwanasheria mkuu wa Tanzania, Prof. Kilangi na kwa upande wa kampuni ya EACOPP ni mkuregunzi mkuu wa kampuni hiyo, Martin John na atashuhudiwa na rais wa utafiti na uzalishaji wa Total Afrika, Nicholaus Teraz.
Rais Samia Suluhu Hassan
“Rais Museveni sio Mgeni Tanzania, ameishi hapa, amepata Elimu yake ya Chuo Kikuu hapa na hata baadhi ya Watoto wake amepatia hapa kwahiyo huyu ni nusu Mtanzania na nusu Mganda, tunamkaribisha sana”
“Hayati Magufuli na Museveni walianza mchakato wa mradi huu wa ujenzi wa bomba la mafuta la Hoima - Tanga na Mimi nimekuja kuuendeleza, mradi huu una faida nyingi ikiwemo pia kuwapatia ajira Wananchi wetu”
“Nakushukuru Rais Museveni kwa kuja licha ya changamoto ya Corona, asante nilikuwa na wasiwasi ila umenithibitishia nyumbani ni nyumbani,najua umekuja kutokana na uzito wa mradi huu wa bomba la mafuta, Watanzania wamesikia maneno kwa miaka 5 tuache maneno tukatekeleze”
“Kuna mambo yanashangaza kulikuwa na sheria wote tusajili laini tuweke vidole ili Mtu akifanya utapeli ajulikane lakini utapeli wa mtandao unaendelea na Watu hawafikishwi Mahakamani, sasa ule usajili ulikuwa kiini macho au nini!? Maana wote tumesajili na majina yapo.
Yoweri Museveni
“Mimi naelewa kiswahili lakini nimesafiri na Wazungu weusi nilionao hapa kutoka Uganda wanajifanya hawaelewi Kiswahili na masikio yanawauma kwa vitu walivyoweka masikioni”
“Sekta muhimu nne ni Kilimo ambacho utapata chakula na utajiri, sekta ya pili ni viwanda, sekta ya tatu ni service (huduma), sekta ya nne ni ICT, sekta hizi zinataka miundombinu kama barabara, umeme, nishati na hizi sekta zote haziwezi kuendelea bila soko”
“Wananchi wa Uganda na Tanzania wasilewe na sekta ya mafuta na gesi wakasahau sekta nyingine kama kilimo, ICT, viwanda n.k, kwasababu mafuta yanaisha lakini kilimo, utalii vinaendelea kwahiyo tutumie rasilimali zenye ukomo kuendeleza rasilimali endelevu”
========
Pia soma
- Marais Museveni na Magufuli wakubaliana kujenga bomba la mafuta
- Rais Magufuli na Museven kuzindua mradi wa Bomba la Mafuta kutoka Uganda wiki ijayo
- Chongoleani, Tanga: Rais Magufuli na Museveni waweka la jiwe la Msingi mradi wa bomba la mafuta kutoka Hoima - Tanga
- Ujenzi wa Bomba la Mafuta: Ziara ya Rais Museveni nchini Tanzania - Septemba 13, 2020
- Serikali za Tanzania na Uganda zatiliana saini mkataba wa Ujenzi wa Bomba la Mafuta
- Tanzania yasaini mkataba wa ujenzi wa Bomba la Mafuta Ghafi kutoka Hoima, Uganda
- Kampuni ya Uchimbaji mafuta Uganda yavunja Mkataba na TOTAL. Je, maslahi yetu kwenye Bomba la Mafuta yatakuwaje?
- Kampuni ya Uchimbaji mafuta Uganda yavunja Mkataba na TOTAL. Je, maslahi yetu kwenye Bomba la Mafuta yatakuwaje?
hapa ndio nimejua watz wengi si waelewa wa mambo na shule ni ndogo sana. hebu tafuta hata articles google ujifunze kidogo kipi kilisainiwa na bado nini na niniHapa ndipo Nimeshangaa, Hata Mwendazake pia alishasaini na Huyu Pia akaenda Huko Sasa kusaini Kusaini kusaini Kila Wakati.
TTA ni TARRIF TRANSPORTATION AGREEMENTngoja niwajuze watu hapa msiojua hii mikataba iliosainiwa.
2017 mu7 na magufuli walisaini mkataba wa awali unaitwa MOU (memorandum of understanding). huu ni non binding agreement. yaani mtu anaweza jitoa mda wowote akitaka
chato: mu7 na JPM waka initialize miakataba wa HGA (host government agreement). yaani makubaliano ya mwanzo kuwa UG na Tz wamekubaliana kutekeleza huu mradi kwa pamoja na TZ itakuwa na hisa asilimia 5%
Samia, mu7, Total na CNOOC in uganda: mikataba 3 ilisainiwa, yaani tripertite, a) TTA transportation tax agreement- makubaliano ya usafirishaji mafuta b) SHA - share holders agreement- wenye share ya bomba ni Ug 15%, TZ, 15%, TOTAL na CNOOC wanagawanabhizo zilizobaki. c) HGA agreement, uganda, total na cnooc walikubaliana ( kumbuka hga,ya UG samia hauhusika sababu haikumuhusu.
Leo: TZ, total, CNOOC, wamesaini HGA, TZ leo wamekubali rasmi kuchua shares 15% na imekubali kutekelwza yote yaliofikiwa k.m kutoa ardhi, security, pesa ili wapewe hiyo 15%. nakaribisha maswali
Mbali ya hiyo 5% mkuu usisahau hapo kuna ajira, kuna fidia tutapata kwa mtu mmoja mmoja na serikali pia.Kazi iendelee na kupigwa juu yaani na kusaini kote huko tunaambulia ka 5% tu.
lighten up JF police. It was all written in good spirit. If at all you felt offended ungepita kimya kimya.Rais Samia pengine anao umri wa mama yako mzazi. Jaribu uwe na adabu japo za kinafiki.
Watu wa aina yako ndio mnaoanzisha uzi wa kudharau serikali ya sasa kila siku, ujumbe wenu wa msingi kabisa ni akili za kipumbavu kama hizi.
Siwezi kuwa offended ila naamini wapo wengi wasiopenda udhalilishaji wa jinsia ya kike.lighten up JF police. It was all written in good spirit. If at all you felt offended ungepita kimya kimya.
HAYA NISAMEHE BWANA BUKILILO. SITORUDIA TENA KUFANYA DHIHAKA.Siwezi kuwa offended ila naamini wapo wengi wasiopenda udhalilishaji wa jinsia ya kike.
Humu kuna wengine ni vijana wadogo sana wanapoingia katika majukwaa kama haya na kukutana na lugha za dhihaka tena zenye kuelekezwa kwa Rais wa nchi wanalidharau jukwaa hili na wote tunaoandika michango ya maoni yetu.
Hii nenda rudi ya Samia Kampala na Museveni Dar es Salaam inaanza kunitia Shaka ila ngoja kwa sasa niusome Mchezo mzima.
' Kumwarika ' ndiyo Kiswahili cha wapi?Kwani nani kamwarika mwenzake kuja kutiliana sahihi, labda tuanzie hapo.
Haonani na Majuha huonana na Werevu.Nauliza tu, hivi rais wa Rwanda yuko wapi, sijamsikia kitambo sana
Tupo pamoja kimawazo, mkataba huu unasainiwa mara tatu mwenye ujuzi wa mambo haya hatueleze me sielewi kuhusu huu mkataba wa bomba la mafuta.Hapa ndipo Nimeshangaa, Hata Mwendazake pia alishasaini na Huyu Pia akaenda Huko Sasa kusaini Kusaini kusaini Kila Wakati.
Wewe ndiwe wa hovyo zaidi kuliko huyo jamaa uliyemshutumu.hapa ndio nimejua watz wengi si waelewa wa mambo na shule ni ndogo sana. hebu tafuta hata articles google ujifunze kidogo kipi kilisainiwa na bado nini na nini
Yeye si mama atakuwa ajakosea!!Yawezekqna ile ya JPM imetoka, kama ataingia rais mwingine nae atasaini.
Ila mama awe mwangalifu asiingizwe cha kike
Nani alikuambia usifuatilie live tukio la utiaji saini ungefuatilia ungejua Sasa tafuta bundle ingia YouTube sikiliza walichokuwa wanafafanua wakubwaTupo pamoja kimawazo, mkataba huu unasainiwa mara tatu mwenye ujuzi wa mambo haya hatueleze me sielewi kuhusu huu mkataba wa bomba la mafuta.