Ikulu, Dodoma: Makabidhiano ya Ripoti ya CAG - Machi 28, 2021

Ikulu, Dodoma: Makabidhiano ya Ripoti ya CAG - Machi 28, 2021

Ubadhirifu ulioko Bandari/TPA sio wa kuvumiliwa hata kidogo,

isiishie tu kumsimamisha Mkurugenzi wake lkn pia walioko chini yake wote wasimamishwe na uchunguzi wa kina ufanyike,
na hatua kali zichukuliwe ikiwemo kufikishwa mahakamani na kutaifishwa mali zao.

TAKUKURU, FIU na vyombo vingine vinao wajibu wa kushughulikia hili la TPA na sisi wananchi tunataka kuona matokeo haraka.
 
Kuna ishu ukiwa kiongozi hutakiwi kukurupuka ktk maamuzi, ATCL ni ishu kubwa hivyo lazima atulie kuifanyia maamuzi tena anaweza kuwasikia wabunge mchango wao ndio amalize. Uraisi ni taasisi bado kuna vyombo vingine bado kuna think tank, hao ni washauri wa raisi waliobobea sio lazima wawe wazawa.
Sio kweli huyo alivyogundua mzee kafariki kuna viashiria watu wamkanyaga mguu kimtindo huwezi kuja na lawama badala ya mapendekezo na unaposema wabunge wakaongee wabunge wa bunge lipi labda LA 2014 kurudi nyuma huko sio hilo LA akina babu tale...
 
Katika Maelezo yake kwa Mh Rais wakati wa kusomwa kwa ripoti ya CAG , Kicheere amesema kuna Majina nane ya Wakurugenzi ambao halmashauri zao zimepata hati chafu

Anayefahamu halmashauri hizo pamoja na Majina ya hao Wakurugenzi walioboronga atusaidie kututajia ile mjadala uwe mpana zaidi .
 
Anayewafàhamu ni jaff ila nina wasiwasi isiwe ikawa mbinu tu ya kumzuga mama Samia ili asimtoe, yeye ndio mhusika mkuu
 
Salam ndugu zangu | JF na watanzania kwa ujumla 🇹🇿


Nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu muweza wa yote kwa kutujalia nafasi ya kuwa hapa siku ya leo. 28 March 2021. Pia nipende kutoa pole kwa ndugu zangu watanzania wote kwa msiba wa Hayati Dr. John Pombe Magufuli, roho yake ilazwe mahala pema...​
1.Kampuni binafsi inayochaguliwa na PAC

Mengine wanaojua watasema
 
CAG aliyepita prof Assad alitoa ripoti mbaya ya ununuzi wa hizo ndege matokeo yake Ndungai akamvalia njuga hadi akatolewa na Mara zote mkuu aliyepita alitangaza faida ya hizi ndege. Mkaguzi Kichere atuambie ni kweli hii ndiyo taarifa aliandaa kumpelekea JPM au ameiedit baada ya kugundua kuwa anaepelekewa siyo JPM tena.
 
Back
Top Bottom