Ikulu, Dodoma: Rais Magufuli amewaapisha Viongozi Wateule mbalimbali, amewasisitiza kuridhika na nafasi walizoteuliwa

Ikulu, Dodoma: Rais Magufuli amewaapisha Viongozi Wateule mbalimbali, amewasisitiza kuridhika na nafasi walizoteuliwa

Ipo siku watia nia watafika milioni moja.
forms za kugombea ulaji ni chanzo kipya cha mapato sisiem inatakiwa kuamka na kuruhusu kila ngazi watia nia wachukue forms kwa misafara huku meza kuu ikipanga safu! hebu fikiri watia nia millioni moja sh ngapi zingekusanywa?

hata urais mila ya kuzuia wengine kuchukua form ya urais imepitwa na wakati, mwaka huu watia nia wakiongozwa na Membe na Nyalandu wangeachwa wafurike kuchukua form za urais bara na sisiem ingepiga hela ndefu na sote tunajua hakuna ambae angemshinda Magu na hata kama yupo ambae angemshinda asingetangazwa!

Bashiru akili zako za kule Mlimani umeweka kabatini?kwanini sisiem haikuchukua hela za mafisadi walizoiba serikalini ambazo zingerudi kupitia forms za urais bara!!

Rais ajae asiwe muoga wa kupingwa kama huyu!

akili yangu yaniambia Mkulu hakutaka wengine wachukue forms za urais bara ili mkutano mkuu wa sisiem uwe mubashara na nchi nzima na dunia yote tuone Mkulu anapendwa anaimbiwa nyimbo na mapambio na kashinda kura za maoni kwa kishindo na kuteuliwa mgombea pekee ikiwa ni strategy yake kujijengea heshma na imani ya raia wataompigia kura uchaguzi mkuu!!

fame versus money! Mkulu kapata sifa sisiem imekosa pesa!!

vita ipo kati ya sisiem asili (wazee, watu wa porini, washamba, analogi, walipigwa viboko na wakoloni, mawazo mgando, mawazo ya kikoloni, mila , desturi na miiko ya chama, udikteta, kiswahili, elimu ya ngumbaru, ujamaa na wizi wa mali za umma, kulindana , hakikisha raia ni wajinga na maskini) versus sisiem academia ( vijana , watoto wa mjini dot com, digital, ubepari, english, demokrasia, pesa mbele, elimu ya juu, twende na wakati, tumbua wezi na wazembe, economic development, democracy and human rights activists)
 
Kuna watu watatumbuliwa live leo. Ila Magufuli ana roho mbaya na ni mbinafsi. Leo yeye angekuwa ni Rais ?Kama angeridhika na ualimu wa secondary ?Mwaka jana angekuwa ameretire na kiinua mgongo cha million 70.
Angewaacha tu. Kwani kura za maoni zinachukua mwezi ?Walioshindwa wangerudi kwenye nafasi zao. Walioshinda hapo ndo angewareplace.
Any way............Yeye ndo Rais ana mamlaka yote kasoro kuzuia kifo chake tu.
Hizo zilikuwa enzi za chama kimoja hazirudi tena!!! ukiamua kujitosa siasa jitose kimoja usiende kubania watu .Enzi hizo wasomi walikuwa wachache .Mtu alikuwa akichukua unpaid leave anakaa hata miaka kumi nafasi yake inamsubiri sasa hivi ni bandika bandua.Ukinyanyua mguu tu haraka unakuwa replaced chap chap.Ni kata mti panda mti
 
Bashite aondoke Jumba la serikali la Oysterbay aende kwao Misungwi maana kwasasa ni raia tu wa kawaida.
Kwahiyo zile mbwembwe za kutembea na msafara wa magari 10 na polisi si ndio basi tena au ?!, [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Jamani mtu akampige picha akiwa anahama pale Masaki atuwekee humu
 
Kwahiyo zile mbwembwe za kutembea na msafara wa magari 10 na polisi si ndio basi tena au ?!, [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Jamani mtu akampige picha akiwa anahama pale Masaki atuwekee humu
Msafara itabidi apokonywe ila kwakuwa ana fedha za wizi ataajiri walinzi binafsi au baba yake atampa kutoka teeth.
 
Naona Chalamila kaamua kuwachomea wenzake kina Bashite kwa kutangaza nia ....... Mama Samia akachochea.

Lakini naona Mukulu kaamua uichunia kiaina.

Usidanganyike mkuu.
Naona siasa wewe huijui.

Kunawatu walipewa uteuzi ili wasiende kugombea kwa msukuma. Unaikumbuka hiyo?

Chalamila ni mwanasiasa!! Makonda 100% katumwa!!!

Vinginevyi angeenda nyamagana kugombea! Maana baba yke ypo igoma.

Ccm hawakurupuki!! Hata kawe!! Atapita Gwajima.

Misungwi atapita Myeti.
 
Alifanyalo analijua sana na habahatishi waziri mtarajiwa
Ngoja tusubiri inawezekana kweli na hivi uchaguzi wa mwaka huu sio wa rushwa bali ni waganganga chochote kinaweza tokea.
 



Viongozi Wateule walioapishwa Leo ni:
1.
Bw. Aboubakar Kunenge- Kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam

2. Bw. Joseph Joseph Mkirikiti - Kuwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara

3. Bw.Paulo Mshimo Makanza - Kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam

4. Bw. Gabriel Pascal Malata- Kuwa Wakili Mkuu wa Serikali

5. Dkt. Boniface Luhende-Kuwa Naibu Wakili Mkuu wa Serikali

6. Dkt. Maduhu Isaac Kazi - Kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC)

Pia Mhe. Rais atashuhudia Uapisho wa Wakuu wa Wilaya za Kongwa, Chunya, Kiteto, Moshi na Hanang

Eneo: Viwanja vya Ikulu Chamwino.
===

UPDATES
-
Rais Magufuli ameshafika katika viwanja hivi kwa ajili ya kuapisha

- Zoezi la kuwaapisha Viongozi mbalimbali walioteuliwa linaendelea.

- Zoezi la kuapa kwa Kiongozi mmoja mmoja limekamilika. kwa sasa Viongozi Wateuliwa watatoa ahadi ya Uadilifu ya Viongozi wa Umma ambapo viongozi hao wanaapa kwa makundi.

Baada ya kukamilika kwa zoezi la uapishaji kwa sasa Viongozi wachache wamepewa nafasi ya kutoa salaam. Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh. Chalamila amepewa nafasi ya kutoa salam kwa niaba ya Wakuu wa Mikoa ambapo amemshukuru Rais Magufuli kutokana na fedha mbalimbali zilizotolewa ili kutekeleza miradi ya maendeleo katika mkoa wa Mbeya na kuahidi kuendelelea kutimiza majukumu yake ya ukuu wa Mkoa katika jiji hilo.

Katika kueleza hili Mh. Albert Chalamira anasema "Katika jiji la Mbeya wachache wamesema hakuna maendeleo yanachotekelezwa lakini hivi karibuni tumepokea zaidi ya bilioni 3.6 kwa ajili ya miundombinu ya Elimu. Hili ni moja ya mambo yaliyonifanya nibaki jiji la Mbeya bila kwenda kugombea"

Baada ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya kutoa salamu kwa sasa amekaribishwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi General Salvatory Mabeyo ambaye anatoa salamu kwa niaba ya Vyombo vya Ulinzi na usalama. General Mabeyo ambapo ameshukuru kwa kupewa nafasi hiyo pamoja na kuwapongeza viongozi wote walioteuliwa na kuwasisitiza kwenda kutimiza majukumu yao.

General Mabeyo amesema "Kwa niaba ya wenzangu nawapongeza walioapishwa kwenda kushika madaraka yao. Lengo kubwa ni kwenda kuwatumikia wananchi lakini kubwa ni kujitafakari na kujitambua kuwa tunapotumikia nafasi zetu tujue dhamana hiyo ni kwa ajili ya maendelo ya Taifa na Wananchi"

Waziri wa Tamisemi Mh. Seleman Jafo amekaribishwa kwa ajili ya kutoa salamu. Aidha, Mh. Jafo amewapongeza Viongozi wote walioteuliwa pamoja na kuwasisitiza wote kwenda kutimiza majukumu yao.

Katika hili Mh. Seleman Jafo amesema "Viongozi mlioapishwa tukamsaidie Rais, tusiende kutafuta umaarufu bali umaarufu uwafuate ninyi. Wanaotafuta umaarufu mara nyingi mwisho wao sio mzuri sana. Nendeni mkahakikishe zile fedha ambazo Rais amezielekeza huko mnazisimamia"

Sambamba na hilo, Jafo amesema Tangu Rais ameingia, ‘trend’ ya udhibiti wa fedha za mamlaka za Serikali za Mitaa umeongezeka kwa umakini mkubwa. Nendeni mkatimize majukumu yenu. Huwa haipendezi unatoka hapa unafika ‘site’ jukumu alilotakiwa kufanya Mkuu wa Wilaya hajafanya. Tembeleeni miradi"

Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan amewapongeza viongozi wote walioteuliwa na kuapishwa katika nafasi mbalimbali. Pia, Mh. Samia amewasisitiza viongozi hao kwenda kutekeleza majukumu yao.

Zaidi ya hayo, Mama Samia Suluhu amewaonya viongozi na kuwasisitiza viongozi kuridhika na madaraka wanayopewa. katika hili Makamu wa Rais amesema Imempendeza Rais kuwapa madaraka akiamini mtakwenda kuwatumikia watu. Mwanadamu unapoishi unatakiwa kutosheka. Utawala wetu sasa hivi sio utawala wa kuhaha na madaraka. Kuwatumikia watu sio kuwaongoza, nendeni someni na angalia wapi pa kurekebisha

HOTUBA YA RAIS MAGUFULI
Rais Magufuli amewapongeza viongozi wote walioapishwa siku ya leo pamoja na kuwasisitiza kwenda kuwatumikia Wananchi wote kwa bidii. Zaidi ya hayo Rais Magufuli amewasisitiza Viongozi walioteuliwa kuridhika wanapopewa madaraka mbalimbali.

Rais Magufuli amesema "Mtambue kwamba hizi nafasi mmezipata kwasababu Mwenyezi Mungu alitaka. Mkawatumikie Wananchi hasa Wananchi masikini. Dkt. Luhende umekuwa Mhadhiri Chuo Kikuu cha Dar. Kanali Songea tumekupeleka Kiteto migogoro ipo mingi, tumekupeleka ukaishughulikie.

Katika hili Rais Magufuli amesema kuwa "Kwenye hizi kazi kuridhika ni kitu kikubwa. Yule kijana pale anaitwa Selemani ana PHD lakini mshahara ni laki 5. Aliridhika na mshahara wake. Ilipojitokeza fursa ndiyo tukamteua kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kongwa. Mmefanikiwa kuipata fursa, hivyo makafanye kazi". Aidha, katika hili Rais Magufuli ametoa mifano ya viongozi mbalimbali walioteuliwa na namna walivyovumilia katika majukumu mbalimbali.

Rais Magufuli amesema "Viongozi vijana imekuwa ngumu kuridhika hasa waliozaliwa miaka ya 1982. Nilikuwa napewa taarifa na Makamu wa Rais kuwa waliojitokeza kugombea kupitia CCM mpaka sasa ni zaidi ya 8,000 na Dar es Salaam ndiyo inaongoza ambapo hadi leo alfajiri wapo 829" .

Aidha, Rais Magufuli amesisitiza kuwa hajamtuma kiongozi yoyote kwenda kugombea nafasi yoyote. Hivyo, viongozi waliochukua fomu ndani ya chama hicho wapimwe inavyostahili.

Katika jambo hili Rais Magufuli amesema "Nataka kuwathibitishia wananchi na wanaCCM hakuna mtu yeyote aliyetumwa na mimi, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Mzee Mangula wala Katibu Mkuu Dkt. Bashiru. Kama wapo watu kule wanaozungumza huko wametumwa na Rais ni waongo. Wapimeni wagombea itakavyowafaa" Siwezi kutuma mtu nyuma ya mgongo".

"Kama ningekuwa na uwezo wa kukutuma wala nisingehakaika, ningesubiri kwenye viti vyangu 10 nikakuteua. Mtu asijekusema ametumwa na IGP au na CDF, wangetaka wangekuteua kuwa hata Kanali. Nendeni mkatumwe na wananchi huko, kila mahali kuna tatizo lake"

zaidi ya hayo rais Magufuli amesisitiza viongozi hao kwenda kuwatumikia wananchi. Mathalani, akimuongelea Mkurugenzi wa TIC Rais Magufuli amesema amemtaka kiongozi huyo kuhakikisha anatafuta Wawekezaji wengi.

Katika jambo hili Rais Magufuli amesema "Kumekuwa na tabia ya kuwazungusha wawekezaji. Mwekezaji amekuja na pesa lakini wewe mara njoo huku mara njoo kesho. Msiwazungushe wawekezaji maana wakiwekeza tutatengeneza ajira. Kuna mwekezaji anataka kujenga kiwanda cha vifaa vya umeme ila nasikia amezungushwa"

Zaidi ya haya Rais Magufuli amewasisitiza kuwa "Kila mmoja katika eneo lake akafanye ambavyo anaona inafaa sio kwamba tumekuwa tukifanya hivi. Tuongeze ‘speed’ na tunataka twende ‘speed’ kubwa zaidi ‘We used’ inakuwa ‘past tense’ kwenye kiingereza, ‘We do this’ hicho ndicho ninachotaka kila mtu akashughulikie"

Mwisho, Rais amewashukuru na kuwatakia mafanikio mema Viongozi wote walioteuliwa pamoja na kupiga nao picha za kumbukumbu.

Yeye mbona hakuridhika na ualimu pale Sengerema?
 
Usidanganyike mkuu.
Naona siasa wewe huijui.

Kunawatu walipewa uteuzi ili wasiende kugombea kwa msukuma. Unaikumbuka hiyo?

Chalamila ni mwanasiasa!! Makonda 100% katumwa!!!

Vinginevyi angeenda nyamagana kugombea! Maana baba yke ypo igoma.

Ccm hawakurupuki!! Hata kawe!! Atapita Gwajima.

Misungwi atapita Myeti.
sasa bongo ni Jamhuri ya Sukumaland!! ujanja wao wasukuma wa kupeana madaraka bila elimu kama Bashite vyeti feki ushashtukiwa nchi nzima japo hatuna la kufanya wasukuma wako wengi mno hata demu wangu ni msukuma na ana heshima mnoooo!nitamuoa na kumbadili dini soon awe muislam.

wajameni tumekwisha!!

kote wajazane wasukumu sitajali sana ila Porn Star Gwajima akipita ubunge nahama CCM naenda ACT!!

hivi miaka mitano ya Magu inakwisha lini?
 
Yeye mbona hakuridhika na ualimu pale Sengerema?
kutoridhika kwa Magu kwenye ualimu Sengerema je kunaondoa ukweli kuwa kutoridhika ni kitu kibaya? tena katika wakati huu 92% ya raia hawana ajira rasmi wala regular income?? je tunaweza kuhukumu mambo ya leo kupitia old practices?
 
Hizo zilikuwa enzi za chama kimoja hazirudi tena!!! ukiamua kujitosa siasa jitose kimoja usiende kubania watu .Enzi hizo wasomi walikuwa wachache .Mtu alikuwa akichukua unpaid leave anakaa hata miaka kumi nafasi yake inamsubiri sasa hivi ni bandika bandua.Ukinyanyua mguu tu haraka unakuwa replaced chap chap.Ni kata mti panda mti
Ila Kitila Mkumbo yeye hajawa replaced,au muda wake bado ?
 
Usidanganyike mkuu.
Naona siasa wewe huijui.

Kunawatu walipewa uteuzi ili wasiende kugombea kwa msukuma. Unaikumbuka hiyo?

Chalamila ni mwanasiasa!! Makonda 100% katumwa!!!

Vinginevyi angeenda nyamagana kugombea! Maana baba yke ypo igoma.

Ccm hawakurupuki!! Hata kawe!! Atapita Gwajima.

Misungwi atapita Myeti.
Mwanza sio wapuuzi.Makonda anajua Nyamagana kuna ushindani mkubwa. Anajua asingepata. Kigamboni ni rahisi kupata maana ukuu wake wa mkoa kautumia vizuri kujijengea mazingira mazuri pale Kigamboni na kuna wasukuma kibao pale Kigamboni.
 
Sheikh ponda njoo huku uangalie uwiano mwingine[emoji1787][emoji1787]
 
kutoridhika kwa Magu kwenye ualimu Sengerema je kunaondoa ukweli kuwa kutoridhika ni kitu kibaya? tena katika wakati huu 92% ya raia hawana ajira rasmi wala regular income?? je tunaweza kuhukumu mambo ya leo kupitia old practices?
Yap tunaweza kuhukumu, yeye anavyotaka maisha mazuri na wengine wanataka
 
Back
Top Bottom