Gloves ni kwa ajili ya kumkinga mtoa chanjo asiambukizwe virusi vya ukimwi kutoka kwa anayemchanja ikitokea huyo anayechanjwa anavyo na mtoa chanjo akagusa damu yake.
Kwa kifupi kama unayemchanja una wasi wasi anaweza kuwa na virusi vya ukimwi, vaa glovu au hakikisha kabisa hugusi damu yake. Kama una uhakika hana virusi hivyo acha kuvaa glovu kwani glovu pia ina madhara yake (though rare) kwa mchanjaji na anayechanjwa. Ni kama yalivyo matumizi ya kondomu. Kama una uhakika mwenza wako hana hivyo virusi usivyae kodomu.
Hao waliochanjwa leo hakuna wasi wasi huo. Pia waliotoa chanjo hizo leo ni wabobezi wa kazi hiyo na hivyo hawawezi kabisa kugusa damu ya mtu waliyemchanja. They know the technique very well. Nadhani uliona kila aliyekuwa akidungwa hiyo sindano alivyokuwa anashikilia damu yake mwenyewe kwenye swab (kipamba) aliyopewa. Ila wachanjaji watakaokuja kukuchanja wewe lazima watavyaa gloves kama walivyovaa walipokuwa wanamchanja huyo rais wa amerika, kwani watakuwa na wasi wasi na wewe wa kutokuwa na virusi vya hiv and hepatitis.