#COVID19 Ikulu, imekaaje viongozi kuchomwa chanjo ya Corona bila wauguzi kuvaa gloves?

#COVID19 Ikulu, imekaaje viongozi kuchomwa chanjo ya Corona bila wauguzi kuvaa gloves?

Unaiga kuandika yanayozunguka mitandaoni!
Ni jambo rahisi kama la Gwajima, una hakika anachochanjwa bilionea ni sawa na unachochanjwa wewe? Chanjo yenyewe ya msaada!
Hata anachochanjwa waziri mkuu ni kile utakachochanjwa wewe kesho

Na wewe iga Mkuu , maana hata hiyo statement "Unaiga kuandika yanayozunguka mitandaoni!" na yenyewe umeiga hakuna kitu kipya ambacho kizazi cha leo kitazungumza ambacho hakijawai kuandikwa.

Gwajima aka Mkono wa Baunsa ni TAPELI ,Chanjo zilizokuwa approved na WHO ndio zinatumika kwahiyo kuna option JJ ,Pfizer ,Astazenica etc kwahiyo kama Majaliwa kachanjwa JJ na mimi pfizer ni kweli tofauti.
 
Chanjo ni hiari wakuu ,tuache conspiracy ,kama hautaki acha usichome waacheni wanaotaka ,mabilionea wanachanja ,wewe mwenzangu na mimi account ina zero nukta mbili unasema mabeberu wanataka kukuua.
Tena watulie maana chanjo yenyewe haitutoshi ambao tuko tayari kuchanjwa kwa hiari.... sijui kwanini wanateseka...
 
Mimi ni muhudumu wa Afya, nafanya kazi RCH. Ni kawaida tu na ninatoa sana chanjo bila globes wala si ajabu, kwaiyo ni swala la kawaida usijari
Ukawaida wake uko wapi ndivyo ulivyofunzwa?
 
Eti wazungu wañataka kutuua,ujinga mtupu,wakuue una lipi la kuwatisha,mnagombania nini wakuue,oooh wanataka tusizaane,sasa mzee wa miaka 60 anaechanjwa kwa kipaumbele kwanza anazaa nini sasa

Kabisa Mkuu yaani inasikitisha utakuta mtu amepita darasani lakini anaongea UTUMBO mtupu!! Mzungu kama anataka kutuua hawezi kusubiri kwenye chanjo ya corona , tuna machanjo kibao tunaletewa na wazungu na tunayatumia.
 
Back
Top Bottom