Dr Akili
JF-Expert Member
- Aug 21, 2011
- 5,119
- 4,569
Gloves ni kwa ajili ya kumkinga mtoa chanjo asimbukizwe virusi vya ukimwi kutoka kwa anyemchanga ikitokea huyo anachanjwa anavyo na mtoa chanjo akagusa damu yake.
Kwa kifupi kama unayemchanja una wasi wasi anaweza kuwa na virusi vya ukimwi, vaa glovu. Kama una uhakika hana virusi hivyo acha kuvaa glovu kwani glovu ina madhara yake pia (though rare) kwa mchanjaji na anayechanjwa. Ni kama yalivyo matumizi ya kondomu. Kama una uhakika mwenza wako hana hivyo virusi usivyae kodomu.
Hao waliochanjwa leo wako salama. Ila watakapokuja kukuchanja wewe lazima watavyaa gloves kama walivyovaa walipokuwa wanamchanja huyo rais wa amerika, kwani watakuwa na wasi wasi na wewe wa kutokuwa na virusi vya hiv and hepatitis.
Sababu kubwa ya watoa huduma ya afya kuvaa gloves ni kujikinga kuambukizwa virusi vya hiv na vya hepatitis ikitokea wakashika au kugusa damu ya mtu ambaye ana virusi hivyo. Kabla ya ujio wa virusi vya ukimwi mwaka 1984 walikuwa hawavyai gloves isipokuwa wakati operesheni ambako walivaa surgical sterile gloves kwa ajili ya kutompandikiza bacteria mgonjwa wanayemfanyia upasuaji (surgical site infection), kitu ambacho ni hatari sana kwa mgonjwa. Surgical gloves hizo ziliwakinga wanaofanya operesheni wasiambukizwe na virusi vya hepatitis virus kutoka kwenye damu ya mgonjwa wanayempasua. Hata kwenye kuzalisha huko labour ward walikuwa hawavyai gloves. Manesi na madaktari walikuwa wanazalisha bila kuvaa gloves. Walivyaa surgical gloves tu pale ilipobidi kuongeza njia ya uzazi kwa kuichana kwa mkasi (episitomy) na baadaye kuishona.Umejuaje wewe anayechanjwa na anayechanjwa wako salama?
Kumbe glove huwavaliwa kwa ajili ya kujikinga na UKIMWI tu? Vipi magonjwa mengine ya kuambukizwa kwa njia ya majimaji au damu huvai glove?
Kwanini wanaohudumia wagonjwa wa Corona wanavaa glove?
Kama hakuna kuambukizwa kwa kumshika mtu maji tiririka ya Nini?
Gloves zilizokuwapo ni surgical sterile gloves kwa ajili ya operesheni. Non surgical gloves zilikuwapo kwa ajili ya examination maalum kwa mgonjwa kama (i)per rectal examination ambapo daktari anaingiza kidole ndani ya mkundu wa mgonjwa na (ii) per vaginal examination ambapo daktari au muuguzi anaingiza vidole viwili au vitatu kwa pamoja ndani ya uke wa mgonjwa.
Examination zingine za mgonjwa au utoaji wa huduma kama kuchoma sindano na kufunga kidonda hakukuhitaji kuvaa gloves ila mtoa huduma alinawa mikono kwa sabuni au antiseptics (hizi antiseptic ndiyo leo mnaziita sanitaizer) kabla na baada ya kumuhudumia/ kumgusa mgonjwa ili kuzuia kusambaza (transmission) vya vidudu hatarishi kama vya bacteria, virus na fungus (pathogenic microorganism) -- nasocomial aka hospital infections. Mbinu nyingine anayotumia mtoa huduma bila kuvaa glovu inaitwa non touch technique - mtoa huduma anahakikisha hagusi damu ya mteja wake. Kwa mfano akishakugunga hiyo sindano ya chanjo, anweka kipamba (swab) kwenye hiyo sehemu na mgonjwa mwenyewe ndiye anaigandamiza hiyo pamba kwa kidole chake mwenyewe hadi damu itakapoacha kutoka. Hivyo mtoa chanjo hagusi damu ya huyo mteja wake bali mteja ndiye anashika damu yake na baada ya hapo anapewa sehemu ya kuitupa.
Huu uvaaji holela wa gloves zisizo sterile kwa kila mtu ni kwa sababu la kujikinga na janga la ukimwi ingawa pia vi
unasaidia kukinga kupata virusi hepatitis.