#COVID19 Ikulu, imekaaje viongozi kuchomwa chanjo ya Corona bila wauguzi kuvaa gloves?

Great foul..... kosa kubwa wamejisahau! mikono yake hatuwezi kuiamini.... hata mavazi, ilibidi avae nguo za hospital/gown kuonesha professionalism

......
HAPO HAKUNA CHANJO HUYO MAMA NI MSANIHII NGULI WA CHAMA NA SERIKALI
 
huyo nesi ameonyesha unprofessionalism ya hali ya juu.tena kwenye picha ya waziri mkuu itakayosambaa dunia nzima na watu wote wataona namna manesi wa tz wanavyofanya kazi.
HUYO NESI HANA TATIZO HAPO KUNA MADAKTARI BINGWA NA MAPROFESA NESI KASAIDIA KUTHIBITISHIA UMA WA WATANZANIA NA DUNIA KUWA VIONGOZI TULIO NAO BAADA YA MAGUFULI NI UTOPOLO.
 
Mimi ni muhudumu wa Afya, nafanya kazi RCH. Ni kawaida tu na ninatoa sana chanjo bila globes wala si ajabu, kwaiyo ni swala la kawaida usijari
Muuguzi wa afya hajui hata kuandika gloves
 
Ukielewa utajua watu wanapigia nin keke
Chanjo ni hiari wakuu ,tuache conspiracy ,kama hautaki acha usichome waacheni wanaotaka ,mabilionea wanachanja ,wewe mwenzangu na mimi account ina zero nukta mbili unasema mabeberu wanataka kuk
 
Wanaotaka kuchoma hio chanjo wachome sisi akina gwajiboy acha tujifukize na kula matangawizi na malimao
 
WAMECLARIFY KUWA GLOVES SIYO LAZIMA.
Ningependa kusikia kauli ya chama cha kitaaluma .... Chama cha wauguzi Tanzania,wenye fani yao wana maoni gani kwenye hili. hao wengine ni wanasiasa wasanii tu.
 
Pich
Picha ya kwanza
Kashika sindano kama anachora tattooπŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
 
Kweli wewe ni mhudumu? Kuandika kwenye ni

Nina wasi wasi na elimu yako Kama nimfanyakazi was afya au health personary how about hepatitis virus back to school dear
 
Tatizo la siku hizi kila mtu aki google something anajiona amekuwa mtalaamu wa hicho alicho google na kuwaona wale watalaam halisi ya hicho kitu amewazidi na anaanza kuwasahihisha. Yaani mtu aliyegoogle kitu kwa dakika tano anajiona anakijua hiko kitu kuliko hao waliokisomea chuoni kitu hicho kwa miaka isiopungua mitano ya chuo kikuu. Hata wakieleweshwa hawataki kukubali kwani wanaamini walichokiona kwa mr google.

Hilo la uvaaji glovu nimesha kutoa elimu yake ya kisayansi. Ninairudia tena hapa kama ulikuwa hujaisoma huko juu:

Sababu kubwa ya watoa huduma ya afya kuvaa gloves ni kujikinga kuambukizwa virusi vya hiv na vya hepatitis ikitokea wakashika au kugusa damu ya mtu ambaye ana virusi hivyo. Kabla ya ujio wa virusi vya ukimwi mwaka 1984 walikuwa hawavyai gloves isipokuwa wakati wa operesheni huko theatre ambako walivaa surgical sterile gloves kwa ajili ya kutompandikizia bacteria au fungus mgonjwa wanayemfanyia upasuaji (surgical site infection prevention), kitu ambacho ni hatari sana kwa maisha ya mgonjwa anayefanyiwa surgery. Surgical gloves hizo ziliwakinga wanaofanya operesheni pia wasiambukizwe na virusi vya hepatitis virus kutoka kwenye damu ya mgonjwa wanayempasua. Hata kwenye kuzalisha huko labour ward (delivery rooms) walikuwa hawavyai gloves. Manesi na madaktari walikuwa wanawazalisha mama wajawazito bila kuvaa gloves. Walivyaa surgical gloves tu pale ilipobidi kuongeza njia ya uzazi (vagina) kwa kuichana kwa mkasi (episiotomy) na baadaye kuishona.

Gloves zilizokuwapo ni surgical sterile gloves kwa ajili ya operesheni na non sterilr examination gloves kwa ajili ya examination kwenye maeneo maalum ya mgonjwa mgonjwa kama (i)per rectal examination ambapo daktari anaingiza kidole chake kimoja (index finger) ndani ya mkundu wa mgonjwa na (ii) per vaginal examination ambapo daktari au muuguzi anaingiza vidole viwili kwa pamoja ndani ya uke wa mgonjwa. Gloves hizo zinamkinga daktari au muuguzi vidole vyake kushika mavi au uchafu ulioko ukeni. Lakini kwenye hali ya emergency na gloves kutokuwepo bado daktari au muuguzi atashika huo uchafu mikononi mwake kuokoa maisha ya mgonjwa, atanawa mikono yake kwa maji na sabuni kufanya disinfection.aka sanitization ya mikono yake.

Examination zingine za mgonjwa au utoaji wa huduma kama kuchoma sindano na kufunga kidonda hakukuhitaji kuvaa gloves ila mtoa huduma hunawa mikono kwa sabuni au antiseptics (hizi antiseptic ndiyo leo mnaziita sanitaizer) kabla na baada ya kumuhudumia/ kumgusa mgonjwa ili kuzuia kusambaza (transmission) ya vidudu hatarishi kama vya bacteria, virus na fungus (pathogenic microorganism) -- nasocomial infections aka hospital infections. Mbinu nyingine anayotumia mtoa huduma bila kuvaa glovu inaitwa non-touch technique - ambayo mtoa huduma anahakikisha hagusi damu au uchafu mwingine kutoka kwa mteja/ mgonjwa wake. Kwa mfano akishakudunga hiyo sindano ya chanjo, anaweka kipamba (swab) kwenye hiyo sehemu na mgonjwa mwenyewe ndiye anaigandamiza hiyo pamba kwa kidole chake mwenyewe hadi damu itakapoacha kutoka. Hivyo mtoa chanjo hagusi damu ya huyo mteja wake bali mteja ndiye anashika damu yake na baada ya hapo anapewa sehemu ya kuitupa.

Huu uvaaji holela wa gloves zisizo sterile na wala si examination gloves kwa kila mtu ni kwa sababu la kujikinga na janga la ukimwi ingawa pia vinasaidia kukinga kupata virusi vya viral hepatitis.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…