Ikulu: Kikao cha kusaini hati za kuondoa hoja tano za Muungano zilizotatuliwa. Sasa rasmi mafuta na gesi kila mtu kivyake

Ni hatua nzuri kwa Muungano wetu. Tunaamini mambo mazuri yanakuja zaidi.

October 28th tuipe CCM kura za kishindo kwa MAENDELEO ya Tanzania

JPM ANATOSHA
CCM KWA MAENDELEO YA TANZANIA
 
Hamuwaondoi wazanzibar kwenye mstari hata siku 1 kwa uchaguzi unaokuja, subirini kwanza upigwe uchaguzi halafu yatafuata maigizo
 
Makosa ya siku za nyuma bado yanaendelezwa kwasababu za kisiasa

1. Kutangazwa live na TBC ni propaganda tu. Hivi barabara ya Chake chake na Mnazi mmoja ni mambo ya Muungano? Yanahusikaje na Muungano?

2. Uwepo wa Hussein Mwinyi mteuliwa wa NEC bara ni propaganda tu za kampeni za kisiasa

3. NEC walitakiwa wazuie hili kwasababu ni '' rushwa ya kisiasa''

4. Haya ni makubaliano tu ''agreement'' ambayo hayana mashiko kisheria. Kamati za muungano zimeundwa kwa mujibu wa sheria gani? Zinapatakana kwa mujibu wa sheria gani? Makubaliano hayo ni kwa mujibu wa sheria gani?
Kwahiyo kilichotokea ni propaganda za uchaguzi, haya makubaliano hayana mashiko kisheria.

5. Kwavile Bunge la JMT na BLW hayakushirikishwa hoja za Muungano zitaendelea kuleta matatizo.
Nani amesaini makubaliano kwa niaba ya Tanganyika?

Haya mambo yanayofanywa kisiasa ndiyo yanatufikisha hapa, na bado watu hawajajifunza. Hili ni suala la kushughukiwa na BLW na Bunge la Tanganyika.

Watanganyika wamebeba mzigo na siku watakapotaka makubaliano, siku hiyo muungano utakufa ghafla.
Yes watadai makubaliano tu ili kuhakikisha Zanzibar wanawajibika na kwavile si masuala ya kisheria, watapitisha makubaliano yao kama ilivyo leo.

Hivi Shamsa Vuai aliyeshughulikia sana haya mambo yupo wapi?

tindo JokaKuu
 
Shamsi Vuai yuko Mwanakwerekwe, kwao huko.
 

..kwenye nchi za wenzetu makubaliano kama haya yasingesainiwa wakati huu siku 11 kabla ya uchaguzi mkuu.
 
Kwa taarifa yako wapiga kura ni 29m+, nusu ya watanzania wote, kama mlipika data mkitegemea kunajisi box la kura, basi safari hii mmeliwa.
Kamanda mwenzangu, probability ipo wazi tumeshashinda uchaguzi, hakuna dhuluma wala kunajisi box la kura.
 
Wazanzibar wanataka nchi yao ikiwa huru kabisa! Dawa iko inachemshwa ma Maalim Seif sijui mtawaambiaje!
 
Punguzeni jazba zisizo na kichwa Wala miguu, endelea kupiga debe huko kwenye Sacco's, wenzenu wanatarget ruzuku tu kwa kuwatumia huku wakijua hawawezi hata nusu ya kura za waTZl
Kamanda mwenzangu,probability ipo wazi tumeshashinda uchaguzi,hakuna dhuluma wala kunajisi box la kura
[/QUO
 
Tanganyika imewakilishwa na nani?
 
Hiyo ni kwa ajili yenu wengi hatuhitaji hata kuifuatilia
 
Mzizi wa tatizo ni muundo wa Muungano. Baaaasi!!!!!
 
..kwenye nchi za wenzetu makubaliano kama haya yasingesainiwa wakati huu siku 11 kabla ya uchaguzi mkuu.
Yote hii ni ghilba tu. Sikiliza barabara za Chake chake na Hospitali ya Mnazi mmoja. Yanatuhusu nini?
Halafu anatajwa Hussein Mwinyi, mgombea wa NEC bara kule Zanzibar.

Tume ya uchaguzi ilipaswa kuona jambo hili kama 'rushwa'' ya kisiasa kutokana na muda.
Hili si dharura ya nchi. Hivi akina Kabudi na Zungu wanakuwa na nguvu gani nje ya dharura?

Makubaliano hayana nguvu za kisheria. JK alifanya haya diamond kwa kuondoa mafuta na gesi na kuwaambia Wazanzibar wanaweza kwenda kukopa nje bila kupitia JMT.
Matokeo yake leo wanasaini yale yale aliyosaini JK Diamond kwasababu ni makubaliano tu si sheria.
 
Shamsi vuai yuko mwanakwerekwe,kwao huko
Dah! huyu Shamsa ni 'muumini wa muungano'' lakini pia anakubalika sana kwa utetezi wake upande wa Zanzibar
CCM- NEC Zanzibar wanamkubali sana na walijua ndiye chaguo lao.
Ilipofika machinjioni Dodoma, akaonekana ni 'kaidi' si mnyenyekevu kama mwana wa Mkuranga, ataleta tabu lete kapu tupa karatasi lenye jina kamwage taka ! Vuai katendewa ukatili sana na sijui kama ana hamu na Dodoma tena!
 
Serikali ngapi zilihudhuria huo mkutano?
 
Kwanza uelewe umoja wa mataifa hujiungi bure ni pesa
Pili unaongelea kuwa fursa zitaongezeka hao wafanyakazi wa ubalozini 200 ni gharama kwa zanzibar mfano kila mmoja analipwa milioni 5 wastani hapo unaongelea shilingi bilioni moja kwa mwezi kwa mwaka ni bilioni 12 gharama kwa serikali ya Zanzibar hapo unaongelea mishahara tu hujaongelea gharama za ofisi zao

Unachosahau unaongelea ajira mpya zitakazopatikana unasahau ajira zitakazopotea!! MFANO kuna maelfu ya wazanzibari wanafanya kazi kwenye wizara za muungano mfano JESHI NA POLISI.muungano ukivunjika hao watafunga virago

Wafanyakazi kibao wataachishwa kazi muungano ukivunjika walio taasisi za umma na binafsi wa zanzibari sababu ajira halitakuwa tena swala la kimuungano kila mtu aende kwake na watakaobaki bara lazima wawe wale tu ambao ajira zao zitakuwa zile tu ambazo wazawa hawaziwezi.Hivyo jiandae kupokea ma jobless kibao zanzibar ambao wamejazana bara wengine wakiwa madereva wa daladala ,bajaj na bodaboda wengine utingo wengine mafundi pikipiki nk

WAko wengine kwenye taasisi za kimuungano hao nao wataondoka

Lakini pia unasahau wapemba waliojazana na wanamiliki ardhi ,biashara ,uvuvi na kilimo nk bara.Muungano ukivunjika nao itabidi wafunge virago sababu maswala hayo sio ya muungano.Wakihitaji itabidi sheria zinazotumika kwa raia wa kigeni zitumike ikiwemo kutoruhusiwa kumiliki ardhi au kufanya biashara ambazo wazawa waweza fanya.Watawekwa kundi moja na wakenya,waganda nk

Pili Zanzibar inategemea bara kwa chakula itabidi muanze kununua kwa pesa za kigeni kama wenzenu

Pia kuna swala la gharama za uendeshaji wa majeshi hizo zote zitaongezeka sana na kuwa kubwa kwenu mnunue midege ya kivita ,mivifaru nk ardhi yenyewe ndogo sijui hata hiyo midege mtapaki wapi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…