IKULU mawasiliano inahitaji data analyst and propagandist, sio mwanahabari otherwise Rais atabadili sana. Mchukueni David Kafulila

IKULU mawasiliano inahitaji data analyst and propagandist, sio mwanahabari otherwise Rais atabadili sana. Mchukueni David Kafulila

Kafulilaa kafulilaaa...
What's wrong!?
 
Ukuu wa mkoa ulimshinda, sembuse Ikulu?
Alishindwaje? Hufahamu kuwa ni yeye akiwa RC Simiyu alipaisha Bei ya pamba kufikia 2200 kwa kilo,Bei ambayo haijawahi kutokea tangia tupate uhuru? Hujuwi ni chuma Kafulila ndio aliweka rekodi hiyo ambayo haijavunjwa?
 
Sio tu Kafulila anafaa kwa nafasi hiyo bali jamaa ni kiraka. Binafsi David Kafulila ni one of my role models…


Jamaa hata nafasi ya PM anaimudu, sababu kuwa leader ni zaidi ya weledi bali lqzima pia uwe political strategist.
Huyu huyu two2? Au kuna Kafulila mwingine..
 
Wivu tu unawasumbua wengine. Lakini moyoni wanajuwa kuwa David Kafulila ni jembe na ataiweza vyema sana nafasi hiyo .
Nikuambia ukweli kuwa Kafulila katumia njia mbaya ya kuwatumia nyie machawa, kama kweli anaitaka hiyo nafasi angekaa kimya tu. Angalia comments za wadau na jiulize hata kama ungekuwa wewe ungemteua hiyo nafasi? Huoni kama mmemvua nguo bila kujua mkidhani mnamchawia.
 
Sio kijana ana miaka mingapi?
Kafulila anao uwezo hata kama ni Mzee ila bado uwezo wake ni mkubwa

..Je, Kafulila anajua kuongea, na kuandika, Kiswahili, na Kiingereza, kwa ufasaha?

..Je, anaweza kuwasiliana kwa niaba ya Raisi, au kumsemea, kwa viwango vinavyokubalika?

..Hizo ndizo sifa kuu anazopaswa kuwa nazo muandishi wa habari wa Raisi / Ikulu.

..Waandishi wa habari wa Raisi ninaowakumbuka ni pamoja na Paul Sozigwa, Ben Mkapa, Sammy Mdee, Habib Halahala, Patrick Chokala, Godfrey Nkurlu, kuwataja baadhi yao.

..Tunapotafuta muandishi wa habari wa Raisi, tunapaswa kuchagua mtu ambaye kitaaluma, na kiuweledi, anaweza kutosha ktk " viatu " vya manguli waliotangulia ktk nafasi hiyo.

..Kwa maoni yangu ofisi ya muandishi wa habari wa Raisi / Ikulu imepwaya tangu kipindi cha Uraisi wa Kikwete.

Cc Nguruvi3, Kiranga
 
Back
Top Bottom