IKULU: Picha rasmi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan

IKULU: Picha rasmi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan

Picha Rasmi ya Rais Wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania inayotakiwa kubandikwa Kwenye Ofisi mbalimbali. MwenyeziMungu amtunze Rais Wetu

Kuna mapungufu kwa mpiga picha sijui ni nani, kakosea kwenye background kuna mwanga na hijab pia inaakishi mwanga,mpiga picha alitakiwa apunguze mwanga na pia angepunguza kidogo exposure ili nguo ionekana nyeusi kiasi pia angemwambia Mh raisi asogee mbele kidogo asiwe karibu na kitambaa cha nyuma(background) na mwisho uchaguzi wa background rangi ya blue si nzuri ama angeweka nyeupe ingefaa zaidi na pia angemwelekeza mh raisi asikae upande(nyuzi 45) bali awe amekaa sawa na kamera asingekaa upande.
 
Uko sahihi.
Amekaa upande.
Naungana nawe pia kwa maoni mengine uliyo ya orodhesha, umenisemea...
 
Sijui nina tatizo gani naona kama jiwe bado yupo ila tu ameacha Urais na nchi bado haina rais
 
Hiyo picha rasmi Ina kasoro kwani mhedhima amekaa upande , picha rasmi huwa zinaonyesha kwa ufasaha mabega yote na masikio yote , waliofika nchi za watu , abroad wanajua picha rasmi lazima ionyeshe masikio yote mawili kwa ufasaha ni sio upande , anyway picha ni nzuri .
Kweli na memo kidogo yanakuwa yanaonekana. Picha zote angalia kuanzia awamu ya kwanza mpaka ya huyo Marehemu zina mfanano. Hii labda ni maalum kwa Rais mwanamke!!!
 
Ukijua ni kwa haraka kiasi gani nafasi yako ya umma itakavyotafutiwa mbadala pale unapoaga dunia basi unapata jibu hakuna haja ya kuringia vyeo hivi. Ndo basi tena.
 
Mnakumbuia ya Marehemu ya mwanzo kabisa ilibadilishwa? Na hii natamani waifanyie marekebisho. Ninaamini watafanya hivyo.
 
Safiii Mama yetu, Rais wetu, Samia Suluhu Hassan.. You have our support and God bless you Mama 🙏🗽💚💛☀🔰
 
Mimi nilikuwa naombea ingependeza picha rasmi ingekuwa ya muonekano huu hapa chini, lakini naona wamependa hiyo nyingine.

Photo: H.E Samia Suluhu Hassan, President of the United Republic of Tanzania.
Picha za viongozi huwa na tai nyekundu kwa wanaume, na wanawake tai nyekundu au kilemba chekundu
 
Back
Top Bottom