Labda mafuriko nchi nzima na miundo mbinu kuharibiwa ilikuwa ni agenda. Hii haiwezi kuwa ni siri chini ya viapo, hivi vitu ni vya kawaida na wananchi wangetaka kujua baraza la mawaziri wana agenda gani kila kunapotokea changamoto.
Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM kila mara inapokutana kujadili mambo, Humphrey Polepole baadaya hutoa taarifa kwa umma juu ya agenda, maazimio na maelekezo kwa serikali .
Nini kinaifanya Sekretariati ya Kabineti ya Serikali ya CCM kufanya kila kitu siri na kutuletea mapicha picha bila taarifa kwa umma juu ya mambo ya kawaida yasiyo chini ya siri za viapo.