Ikulu ya Magogoni ibadilishwe matumizi isiwe maskani ya popo

Ni humu humu JF tulisoma uzi wa mwekezaji aliyeleta fedha zake 150milioni dola za Marekani akitaka kuwekeza kujenga kiwanda Cha madawa huko Arusha. Fedha zake zimezuiwa BoT akitakiwa atoe rushwa kuijenga Dodoma. Amekataa sasa anataka hela yake akawekeze Kenya wanaomhitaji. Mods wanaweza kurejesha uzi huo.

Nasema uongo ndugu zangu..
Uzi ule ulipigwa pini?!

Mizengwe: Bilioni 425 za Mwekezaji zazuiliwa Tanzania, Kenya yamshawishi ahamie kwao​

December 4, 2020
WAWEKEZAJI na matajiri wa viwanda katika nchi kadhaa duniani, familia ya Jamal Hassan Abdullah Alawadhi ya Kuwait, wamekumbana na mkwamo wa kuanzisha kiwanda cha dawa nchini Tanzania baada ya kuleta nchini kiasi cha Euro 150,000,000 ambazo ni takribani Shilingi za kitanzania bilioni 425, ambazo bado zinadaiwa kushikiliwa na serikali kwa zaidi ya miaka miwili sasa.

Chanzo
Familia ya matajiri hao iliingia ubia na kampuni ya wazawa (Watanzania) ya Pharmaceutical Investment Limited (PIL) ambayo ilinunua asilimia 60 ya hisa za kiwanda cha Serikali cha kutengeneza dawa cha Tanzania Pharmaceutical Industries Limited (TPI) kilichopo Arusha. Serikali ya Tanzania ilibaki na asilimia 40 ya hisa.

Aidha, inaelezwa kuwa baada ya kukamilika kwa mchakato wa awali wa kununua hisa, hatimaye mwekezaji aliridhika na kuamua kuwekeza fedha katika kiwanda hicho, makubaliano yakiwa matengenezo yakamilike haraka na uzalishaji wa dawa uanze mapema kadri inavyowezekana.
Kiasi hicho cha fedha kilitumwa nchini na kupokelewa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) mnamo Septemba 12, 2018, ikiwa ni mtaji wa kuanzisha kiwanda hicho cha dawa muhimu kwa matumizi ya binadamu.

Baada ya BoT kupokea kiasi hicho cha fedha, ilitakiwa kuingizwa kwenye akaunti ya PIL iliyoko Benki ya CRDB, tawi la Holland House, Dar es Salaam ili matumizi yake yaanze mara moja kwa kiwanda kuanza uzalishaji.

Mkwamo
Hadi leo, ikiwa ni miaka miwili na miezi miwili, bado kiasi hicho hakijaingizwa kwenye akaunti za wahusika. Sababu; haziko wazi, ingawa inawezekana kuna baadhi ya maofisa Serikalini bado wanaendelea na mchakato wa kujiridhisha kuhusu vyanzo vya fedha hizo.

Mmoja wa wanafamilia ya Jamal Alawadhi ameongea na mwandishi wa habari hii kuhusu uhalali wa fedha hizo za uwekezaji na amekiri kwamba amewahi kuhojiwa na kuombwa nyaraka kadhaa zinazoonyesha vyanzo vya fedha zake.
Anasema katika vikao walivyofanya na uongozi wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) na BoT, Serikali iliridhika kuwa fedha hizo ni halali na kwamba wakati wowote zingeweza kuingia kwenye akaunti ya kampuni ya PIL.

“Jamal amekuja Dar es Salaam mara nyingi na kuwa na vikao na viongozi wa TIC, na hakuna wasiwasi wowote juu ya uhalali wa kipato chake binafsi wala cha familia yetu, tunafanya biashara halali na mara nyingi tuko kusaidia jamii,” anaongeza mwanafamilia huyo.

Rais Magufuli ahusishwa kuokoa jahazi
Hata hivyo, pamoja na ahadi hiyo ya BoT ya fedha kuingizwa kwenye akaunti yao, bado dalili za kuanza kazi ya kukifufua kiwanda zilikuwa finyu, hivyo uongozi wa PIL uliamua kuandika barua kwa Rais John Magufuli – Januari 15, 2019 kumjulisha juu ya jambo hili na pia kuomba msaada wake ili kuhimiza utekelezaji wake.

Taarifa tulizo nazo zinaonyesha kwamba Ikulu ilijibu barua hiyo siku – Januari 16, kwa simu ikieleza kwamba uongozi wa PIL unatakiwa kuonana na Mkurugenzi Mkuu wa TIC ili kufikia muafaka.

Kilichotokea TIC
Januari 17, 2019, uongozi wa PIL, ulifika ofisi za TIC na kukutana na Mkurugenzi Mkuu, Geoffrey Mwambe (hivi sasa hayupo tena) ambaye kwa mujibu wa maelezo ya wawekezaji hao, aliwapa ushirikiano na kuwaeleza kwamba suala lao litamalizika karibuni.

Katika mkutano na Mwambe, PIL ilitakiwa kuonyesha muhtasari na mchanganuo wa fedha hizo zitakavyotumika, uhalali wake (kwa mara nyingine) na kuomba wawekezaji wote, ikiwemo familia ya Alawadhi kufika nchini kukutana na “mamlaka zinazohusika.”

Siku 10 baada ya kumalizika kwa kikao hicho, mmoja wa wanafamilia ya Alawadhi, Eng. Jamal aliwasili nchini na siku iliyofuata, Januari 28, 2019, akiwa amefuatana na wanahisa (Watanzania) walifanya kikao na Mwambe, jijini Dar es Salaam na kukubaliana kukutana baada ya siku mbili ili kukamilisha mazungumzo hayo.

Inaelezwa kuwa Januari 30, 2019, Eng. Jamal na wanahisa wengine walifika TIC na kufanya kikao ambacho kilichukua muda mrefu huku Mwambe akiwaambia wawekezaji hao “wasiwe na wasiwasi,” kwani suala lao limekamilika.
Baada ya kumalizika kwa kikao hicho, Eng. Jamal alilalamikia uwepo wa vikao vingi huku akionyesha kutokujua lini kiwanda kingeanza uzalishaji.

Mwekezaji akata tamaa, ashawishiwa kuhamia Kenya
Taarifa zinaeleza kwamba Eng. Jamal ametishia kuondoa fedha zake ikiwa ataendelea kupewa ‘ahadi’ ambazo zinachelewesha kuanza kwa uzalishaji wa dawa.

Uchunguzi wa awali unaonesha kuwepo kwa madalali kutoka Kenya wanaomshawishi Eng. Jamal kupeleka fedha hizo nchini kwao ili kiwanda hicho kijengwe haraka.
“Jamal amefuatwa na Wakenya, wanaomba akawekeze kwao, lakini amesema bado hana nia hiyo, lakini ikiwa atashindwa kabisa itabidi aondoe fedha zake na kwenda huko,” anasema mwanafamilia.

Imebainika kwamba Wakenya hao aliokutana nao Dar es Salaam, wameahidi kumpa eneo kubwa la uwekezaji huko Mombasa au mahali anapopenda ili kuanza ujenzi wa kiwanda na kuwa atapewa fursa ya kipekee katika utekelezaji wa uwekezaji wake.

Mkuu Mpya wa TIC anena
Mkurugenzi Mtendaji wa TIC, Maduhu Kazi akizungumzia suala hilo, amesema wahusika wa uwekezaji huo wafike ofisini kwake ili kuona ni wapi wamekwama na kuchukua uamuzi wenye manufaa kwao na Tanzania na watu wake.
Kazi amesema ofisi yake iko wazi na kwamba haina kikwazo kwa mwekezaji yeyote ikiwa atafuata na kutimiza masharti na matakwa ya kisheria ya uwekezaji na kwamba uamuzi ikiwa kila kitu kimekamilishwa, utatolewa kwa muda mfupi.
Rais Magufuli na ahadi ya kuboresha mazingira ya uwekezaji

Katika hotuba yake bungeni, Dodoma, wakati wa kulifungua Bunge baada ya kutangazwa mshindi wa urais kwenye Uchaguzi wa Oktoba 28, 2020, Rais Magufuli alitangaza uamuzi wake kuweka TIC chini ya Ofisi ya Rais.

Alisema hatua hiyo ina nia ya kuharakisha uamuzi kwa wawekezaji makini, kwani Tanzania inahitaji zaidi uwepo wa wawekezaji ili kuimarisha uchumi wake unaoendelea kukua.
Faida za kiwanda kujengwa Tanzania
Ikumbukwe kuwa kuanza kazi ya uzalishaji wa dawa hizo muhimu, kungepunguza zaidi gharama za kuagiza Dawa kwa Serikali na kuokoa zaidi ya Shilingi bilioni 900 zinazotumika kila mwaka kuagiza dawa nje ya nchi.

Mbali na kuokoa fedha, kiwanda hicho kingeongeza ajira kwa Watanzania na kupunguza kadhia ya ukosefu wa ajira.
Mbali na faida hizo, kiwanda hicho kingekuwa chanzo kikubwa cha kodi ambayo ingekuwa chachu ya maendeleo kwa kuwezesha kuwepo kwa barabara, ujenzi wa shule na hata hospitali.
 
Dar state house ndio Ikulu, Dodoma ni kitongojo.
Mabalozi walipo ndio maelezo,huwezi kumlazimisha balozi ahame.
2025 sio mbali,wajanja wameishastuka,wanaagalia move.
 
Ni suala la muda tu, magogoni itarudia enzi yake ngoja mtu aondoke uone.

Hakuna mtu atakaye kaa kwenye vumbi Dodoma.
Hii comment itakuja kuwa kweli. Hata mimi naamini rais ajaye atarudisha wizara zote Dar es salaam.
 
Long winded story when its all about Awadhi mu Oman...

Hivi wewe Nyarugusi unadhani ukiwa Oman watakujadili kwenye mitandao au magazeti yao eti kuna mwekezaji Ngonyani Chakubimbi from Tanzania anataka kudhulumiwa ?

Mbona Waafrika tuko hypnotized na wageni ambao wao wanatuona mbolea za nguruwe ?

Mwekezaji mu- Oman can suck my peanuts!
Nasoma between the lines, hili jibu ni zaidi ya mchangiaji wa kawaida wa jf!
 
Ni suala la muda tu, magogoni itarudia enzi yake ngoja mtu aondoke uone.

Hakuna mtu atakaye kaa kwenye vumbi Dodoma.

Kwangu mimi naona ikulu ya Dodoma ni kwa ajili ya Magufuli, japo wazo ni la Nyerere. Sioni ikulu kubaki Dodoma baada ya awamu hii, labda hiyo ikulu ya Dar iuzwe au ibadilishiwe matumizi. Hata hivyo tuna katiba mbovu kabisa, ambayo vipao mbele vya rais ndio hugeuzwa vya nchi. Usishangae hiyo ikulu hata ikiuzwa, akaja rais mwingine akajenga ikulu nyingine na watu wakamsifia!
 
Long winded story when its all about Awadhi mu Oman...

Hivi wewe Nyarugusi unadhani ukiwa Oman watakujadili kwenye mitandao au magazeti yao eti kuna mwekezaji Ngonyani Chakubimbi from Tanzania anataka kudhulumiwa ?

Mbona Waafrika tuko hypnotized na wageni ambao wao wanatuona mbolea za nguruwe ?

Mwekezaji mu- Oman can suck my peanuts!
Kwa hiyo unataka kuwaibia mali zao kisa kwao huthaminiwi? Ushetani wa kupitiliza!
 
Uzi ule ulipigwa pini?!

Mizengwe: Bilioni 425 za Mwekezaji zazuiliwa Tanzania, Kenya yamshawishi ahamie kwao​

December 4, 2020
WAWEKEZAJI na matajiri wa viwanda katika nchi kadhaa duniani, familia ya Jamal Hassan Abdullah Alawadhi ya Kuwait, wamekumbana na mkwamo wa kuanzisha kiwanda cha dawa nchini Tanzania baada ya kuleta nchini kiasi cha Euro 150,000,000 ambazo ni takribani Shilingi za kitanzania bilioni 425, ambazo bado zinadaiwa kushikiliwa na serikali kwa zaidi ya miaka miwili sasa.
Chanzo
Familia ya matajiri hao iliingia ubia na kampuni ya wazawa (Watanzania) ya Pharmaceutical Investment Limited (PIL) ambayo ilinunua asilimia 60 ya hisa za kiwanda cha Serikali cha kutengeneza dawa cha Tanzania Pharmaceutical Industries Limited (TPI) kilichopo Arusha. Serikali ya Tanzania ilibaki na asilimia 40 ya hisa.
Aidha, inaelezwa kuwa baada ya kukamilika kwa mchakato wa awali wa kununua hisa, hatimaye mwekezaji aliridhika na kuamua kuwekeza fedha katika kiwanda hicho, makubaliano yakiwa matengenezo yakamilike haraka na uzalishaji wa dawa uanze mapema kadri inavyowezekana.
Kiasi hicho cha fedha kilitumwa nchini na kupokelewa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) mnamo Septemba 12, 2018, ikiwa ni mtaji wa kuanzisha kiwanda hicho cha dawa muhimu kwa matumizi ya binadamu.
Baada ya BoT kupokea kiasi hicho cha fedha, ilitakiwa kuingizwa kwenye akaunti ya PIL iliyoko Benki ya CRDB, tawi la Holland House, Dar es Salaam ili matumizi yake yaanze mara moja kwa kiwanda kuanza uzalishaji.
Mkwamo
Hadi leo, ikiwa ni miaka miwili na miezi miwili, bado kiasi hicho hakijaingizwa kwenye akaunti za wahusika. Sababu; haziko wazi, ingawa inawezekana kuna baadhi ya maofisa Serikalini bado wanaendelea na mchakato wa kujiridhisha kuhusu vyanzo vya fedha hizo.
Mmoja wa wanafamilia ya Jamal Alawadhi ameongea na mwandishi wa habari hii kuhusu uhalali wa fedha hizo za uwekezaji na amekiri kwamba amewahi kuhojiwa na kuombwa nyaraka kadhaa zinazoonyesha vyanzo vya fedha zake.
Anasema katika vikao walivyofanya na uongozi wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) na BoT, Serikali iliridhika kuwa fedha hizo ni halali na kwamba wakati wowote zingeweza kuingia kwenye akaunti ya kampuni ya PIL.
“Jamal amekuja Dar es Salaam mara nyingi na kuwa na vikao na viongozi wa TIC, na hakuna wasiwasi wowote juu ya uhalali wa kipato chake binafsi wala cha familia yetu, tunafanya biashara halali na mara nyingi tuko kusaidia jamii,” anaongeza mwanafamilia huyo.
Rais Magufuli ahusishwa kuokoa jahazi
Hata hivyo, pamoja na ahadi hiyo ya BoT ya fedha kuingizwa kwenye akaunti yao, bado dalili za kuanza kazi ya kukifufua kiwanda zilikuwa finyu, hivyo uongozi wa PIL uliamua kuandika barua kwa Rais John Magufuli – Januari 15, 2019 kumjulisha juu ya jambo hili na pia kuomba msaada wake ili kuhimiza utekelezaji wake.
Taarifa tulizo nazo zinaonyesha kwamba Ikulu ilijibu barua hiyo siku – Januari 16, kwa simu ikieleza kwamba uongozi wa PIL unatakiwa kuonana na Mkurugenzi Mkuu wa TIC ili kufikia muafaka.
Kilichotokea TIC
Januari 17, 2019, uongozi wa PIL, ulifika ofisi za TIC na kukutana na Mkurugenzi Mkuu, Geoffrey Mwambe (hivi sasa hayupo tena) ambaye kwa mujibu wa maelezo ya wawekezaji hao, aliwapa ushirikiano na kuwaeleza kwamba suala lao litamalizika karibuni.
Katika mkutano na Mwambe, PIL ilitakiwa kuonyesha muhtasari na mchanganuo wa fedha hizo zitakavyotumika, uhalali wake (kwa mara nyingine) na kuomba wawekezaji wote, ikiwemo familia ya Alawadhi kufika nchini kukutana na “mamlaka zinazohusika.”
Siku 10 baada ya kumalizika kwa kikao hicho, mmoja wa wanafamilia ya Alawadhi, Eng. Jamal aliwasili nchini na siku iliyofuata, Januari 28, 2019, akiwa amefuatana na wanahisa (Watanzania) walifanya kikao na Mwambe, jijini Dar es Salaam na kukubaliana kukutana baada ya siku mbili ili kukamilisha mazungumzo hayo.
Inaelezwa kuwa Januari 30, 2019, Eng. Jamal na wanahisa wengine walifika TIC na kufanya kikao ambacho kilichukua muda mrefu huku Mwambe akiwaambia wawekezaji hao “wasiwe na wasiwasi,” kwani suala lao limekamilika.
Baada ya kumalizika kwa kikao hicho, Eng. Jamal alilalamikia uwepo wa vikao vingi huku akionyesha kutokujua lini kiwanda kingeanza uzalishaji.
Mwekezaji akata tamaa, ashawishiwa kuhamia Kenya
Taarifa zinaeleza kwamba Eng. Jamal ametishia kuondoa fedha zake ikiwa ataendelea kupewa ‘ahadi’ ambazo zinachelewesha kuanza kwa uzalishaji wa dawa.
Uchunguzi wa awali unaonesha kuwepo kwa madalali kutoka Kenya wanaomshawishi Eng. Jamal kupeleka fedha hizo nchini kwao ili kiwanda hicho kijengwe haraka.
“Jamal amefuatwa na Wakenya, wanaomba akawekeze kwao, lakini amesema bado hana nia hiyo, lakini ikiwa atashindwa kabisa itabidi aondoe fedha zake na kwenda huko,” anasema mwanafamilia.
Imebainika kwamba Wakenya hao aliokutana nao Dar es Salaam, wameahidi kumpa eneo kubwa la uwekezaji huko Mombasa au mahali anapopenda ili kuanza ujenzi wa kiwanda na kuwa atapewa fursa ya kipekee katika utekelezaji wa uwekezaji wake.
Mkuu Mpya wa TIC anena
Mkurugenzi Mtendaji wa TIC, Maduhu Kazi akizungumzia suala hilo, amesema wahusika wa uwekezaji huo wafike ofisini kwake ili kuona ni wapi wamekwama na kuchukua uamuzi wenye manufaa kwao na Tanzania na watu wake.
Kazi amesema ofisi yake iko wazi na kwamba haina kikwazo kwa mwekezaji yeyote ikiwa atafuata na kutimiza masharti na matakwa ya kisheria ya uwekezaji na kwamba uamuzi ikiwa kila kitu kimekamilishwa, utatolewa kwa muda mfupi.
Rais Magufuli na ahadi ya kuboresha mazingira ya uwekezaji
Katika hotuba yake bungeni, Dodoma, wakati wa kulifungua Bunge baada ya kutangazwa mshindi wa urais kwenye Uchaguzi wa Oktoba 28, 2020, Rais Magufuli alitangaza uamuzi wake kuweka TIC chini ya Ofisi ya Rais.
Alisema hatua hiyo ina nia ya kuharakisha uamuzi kwa wawekezaji makini, kwani Tanzania inahitaji zaidi uwepo wa wawekezaji ili kuimarisha uchumi wake unaoendelea kukua.
Faida za kiwanda kujengwa Tanzania
Ikumbukwe kuwa kuanza kazi ya uzalishaji wa dawa hizo muhimu, kungepunguza zaidi gharama za kuagiza Dawa kwa Serikali na kuokoa zaidi ya Shilingi bilioni 900 zinazotumika kila mwaka kuagiza dawa nje ya nchi.
Mbali na kuokoa fedha, kiwanda hicho kingeongeza ajira kwa Watanzania na kupunguza kadhia ya ukosefu wa ajira.
Mbali na faida hizo, kiwanda hicho kingekuwa chanzo kikubwa cha kodi ambayo ingekuwa chachu ya maendeleo kwa kuwezesha kuwepo kwa barabara, ujenzi wa shule na hata hospitali.
Kadhulumu bilioni 425 naye kadhulumiwa tilioni Saba na Kagame na urafiki umekufa .
 
Ikulu ni ofisi ya Rais .so hata awe wapi akikaa na atakapo kuwepo ndipo panaitwa ikulu.
As long as maisha yetu yapo stable ikulu hata. Iwe Ruangwa sawa tu.
 
Back
Top Bottom