Kwa kuwa serikali imesema kuwa hati ya Muungano ambayo imekuwa kizungumkuti miaka mingi na mara nyingine ikapelekwa hati Tasa yenye saini feki, sasa italetwa bungeni. Tusubiri tuipokee na tuitendee kazi kama ifuatavyo.
Sasa wote tunajua Maudhui ya Hati ilikuwa ni kwamba masuala ya Muungano ni kumi na Moja. Sasa ikiletwa wote tudai masuala ya Muungano yawe kama ilivyo kwenye Hati Husika. Na sasa tuje tuone wale Wazanzibari wanaotokana na CCM ambao wanasema wanataka serikali mbili kama watakubali Zanzibar irudi kule na kuwa kama ilivyokuwa wakati tumeungana. Aidha tuone kama kweli hawa wazanzibariCCM watakubali kurejea katiba ya Zanzibari iliyokuwepo ambayo inatokana na Hati ya Muungano huo. Niwashukuru sana wale waheshimiwa wachache wenye kuwakilisha kundi kubwa kama kina JUSA, LISU, DUNI, MNYIKA, na wote wanaounga mkono Rasmu ya Mheshimiwa sana Warioba.