Ikulu Yaita Waandishi Wa Habari kuwaonesha Hati Ya Muungano

Ikulu Yaita Waandishi Wa Habari kuwaonesha Hati Ya Muungano

watakayoiona iyo hati watueleze kama imetaja nchi inayoitwa Tanzania, kama imetaja nchi ya tanganika na tunaomba mtueleze mambo ya Muungano ni yepi katika iyo hati. Kama ina neno Tanganyika, mungu ashukuriwe nchi yetu tanganyika imerudi! kama haijataja neno Tanganyika, naomba rais atumie madaraka yake, apige marufuku kutaja neno Tanganyika! Kama kuna neno Tanganyika, kuanzia leo watupe Tanganyika yetu!
 
Naona watawala wamechanganyikiwa! Hati imeombwa bungeni, Katibu wa bunge 1964 amekiri wazi kuwa hakuwahi kuiona, Karume ambaye ni rais mstaafu wa Zanzibar naye alishawahi kukiri hadharani kuwa kwa miaka kumi aliyokaa ikulu Zanzibar hakuwahi kuiona; Hiyo iliyotolewa leo tena kwa kuita waandishi wa habari wameitoa wapi! Kama ilikuwepo, kwa nini muda wote wasiipeleke kwa wanaoihitaji...

Huu ni usanii kama walivyozoea kujiaminisha KELELE ZA MLANGO HAZIMNYIMI MWENYE NYUMBA KULALA lakini katika hili naona mwenye nyumba anakosa usingizi na anaanza kujidunga mvinyo na whisky ili kupoteza mawazo.
 
Hawa wazanzibari CCM wanafiki sana wakati ikifika kuirudisha Zanzibar kutekeleza matakwa ya HAKI wale ZanziCCM utaona watakavyodunda. Wakati kwa sasa wanafursa ya kuifanya Zanzibar kuwa Huru na pia kujitegemea lakini kwa sasa Wanaufyata. Wameufyata kweli hawa ZanziCCM. Shame on you ZanziCCM kwa kuamua wenyewe kuufyata na kuiacha kweli
 
Hata wakiifoji kuna wakuwahoji?
Hii mechakachuliwa makamanda siku zote hizo wanatuonyesha leo?
Nchi inaongozwa ni mifsyukyule.
 
Taarifa nilizozipata muda huu ni kuwa Waandishi wa habari wameitwa Ikulu na Katibu Mkuu Kiongozi lengo ni kuwaonyesha Hati Ya Muungano na kukata mzizi wa Fitina Kwa wajumbe wa bunge la Katiba. Tutawajulisha hapa hapa...
Inahitajika Bungeni sio kwa waandishi wa habari!
Kama ni halari ipelekwe Bungeni.
 
Kupitia StarTV naona katibu mkuu Ikulu akiwaonesha waandishi wa habari hati halisi ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar.



Monday, April 14, 2014

Hati Halali ya Muungano hii hapa ikiwa Imesainiwa ORIGINAL na Rais Nyerere na Rais Karume,Hakuna Uchakachuaji hapa




‪#‎HABARI‬ Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue ameonesha hati ya muungano wa Tanzania, kati ya nchi ya Zanzibar na Tanganyika.

Balozi Sefue amewahakikishia Watanzania kuwa nyaraka hizi muhimu ziko salama ila hakuna haja ya kujua ziko wapi.

Balozi Sefue amesema wanaosema kuwa hati hazipo na sahihi zake ni za kughushiwa, ni waongo.
Mambo 11 waliyokubaliana viongozi, wakati Zanzibar na Tanganyika zinaungana pia yameonekana katika hati ya Muungano.



BlL3iXXIcAAc_v6.jpg:large



Hii ndio

hati halali ya Muungano iliyosainiwa na Rais nyerere na Abeid Karume,.Hati yote nitaiweka hapa Soon.


Source: Habari Kwanza
 
Kama Rais Watanzania tumempata na ni vema tukaangalia kwa mapana aina ya makabila yanayofaa kuongoza nchi kwani kabila hili linalotuongoza sasa halistahili kuongoza kabisa labda kwenye vitongoji vya huko vijijini kwao.

mmh kibgo mm nitakuwa wa mwisho kukuunga mkono katika ili, ukumbuke ili kabila la sasa ndo linatupa mamlaka ya kuirudisha Tanganyika, enzi zetu za mizee iliyopita, ilikuwa ni dhambi kuongelea muungano, ukimuuliza mzee A.Jumbe atakuambia neno muungano lilimkositi, ila leo hii ------ ametupa muda wa kuamua!ukumbuke ccm haikuwai kuwa na lengo ili! Nimelipenda ilo kabila!
 
Katika kujadili ibara ya 1 na ya 6 hati ya muungano ni nyenzo muhimu sana ila nazani hati yenyewe imechezewa ndo maana waliificha. Walitaka waifiche wajumbe kama wakina lissu, mnyika na wengi wanaoweza kuibana serkali ndo wailete mwishoooo. Haya ma ccm bhaaaaanaaaaa
 
Waandishi muingalie vema ili mubaini uhalisia wake kabla hamjatuonesha

Waandishi wenyewe walioitwa ni wa gazeti la Uhuru, Mzalendo na kituo cha TBC na wamelipwa kwa kuwepo hapo sidhani kama watachunguza kama unavyoshauri sie tusubiri tutapata uhalisia kutoka vyanzo vingine sio hao waandishi njaa
 
Hoja ya hati ya Muungano ni hoja muflisi kwa kweli.. sijui kwanini watu wasomi wameing'ang'ania hii! Hivi uhalali wa Muungano unategemea uwepo wa haki ya Muungano? Je kama cheti cha ndoa au pete ya ndoa imepotea ina maana ndoa haina uhalali? Hivi uhalali wa mkataba wowote unategemea uwepo wa nyaraka za mkataba huo hasa kama pande zote zinakubaliana kuwa mkataba ulisainiwa na ushahidi wa watu kusaini na yaliyomo mwenye hiyo hati yanajulikana?
 
mmh kibgo mm nitakuwa wa mwisho kukuunga mkono katika ili, ukumbuke ili kabila la sasa ndo linatupa mamlaka ya kuirudisha Tanganyika, enzi zetu za mizee iliyopita, ilikuwa ni dhambi kuongelea muungano, ukimuuliza mzee A.Jumbe atakuambia neno muungano lilimkositi, ila leo hii ------ ametupa muda wa kuamua!ukumbuke ccm haikuwai kuwa na lengo ili! Nimelipenda ilo kabila!

Naona umelipenda hili kabila kwa sababu ya Udhaifu uliojitokeza kwani limejitahidi kutuingiza katika mchakato ambao linaupinga.
 
hata mama fatma fereji amezungumza vyema, nimependa presentation yake
 
SIamini na wala sikubali kuwa tuna hati 2 ZA muungano. Ile yenye saini feki iliyopelekwa mwanzo na hii ya Sefue aliyowaonyesha wachaguliwa wa waaandishi habari mchana huu. Naomba majibu haya kwa nini walipeleka hati tofauti bungeni? Je Zanzibar wameapprove kuwa hiyo Ndio kweli halisi? Naona sasa suala la muungano lirudi kwa wananchi.
 
Haya hoja ya kuto kuwepo kwa hati imepata jibu sasa ngoja tusubili kama ni yenyewe isije ikawa imechakachuliwa maana hawa jamaa wa serikali kwa uchakachuaji wako vizuri.
 
Back
Top Bottom