Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mzee Mwanakijiji hili ni swali moja tu kati ya maswali mengi ya msingi. Hapa tunaisoma tanganyika na Zanzibar, ambapo sasa tunaisikia Zanzibar tu. Na kwenye hati hii hatujaona muundo wa serikali. Navilevile bado pande zote mbili za muungano tunaweza kupanga aina ya muungano tunaoutaka kufuatia fursa hii ya kutenngeneza katiba mpya.JUst silly! sasa Muungano ni halali kwa vile watu wameona hati?
Tunashukuru kwa kutuonyesha hiyo hati ya muungano, la msingi ni kuyangalia waliokubaliana kwenye huo muungano yanakidhi maitaji ya sasa ndiyo muhimu.
Kwani inatakiwa na waandishi au wajumbe wa katiba? Harufu ya uchakachuaji na kujihami imeanza kuonekana.
Sent from my iPad using JamiiForums
wewe kijana hebu kaa utulie hii ngoma unpoicheza sharti mabega yawe kimzambazi.
Hati ni kielelezo thibitishwa kisheria pale kunapotokea mkanganyiko wa sinto fahamu baina ya pande zinazo pingana.
Unapoongelea mfano wa ndoa lazima utambue na sheria zake,
katika taratibu za mikataba ya miungano ya mataifa mbalimbali lazima nyaraka zitunzwe ili pale zinapohitajika zitumike.
Mfano .u.s.a ile nyaraka ya muungano wao ipo na inatunzwa.
Tunashukuru kwa kutuonyesha hiyo hati ya muungano, la msingi ni kuyangalia waliokubaliana kwenye huo muungano yanakidhi maitaji ya sasa ndiyo muhimu.
Mkuu, kwa fikra zangu hati ya makubaliano ya muungano ndio ya kwanza halafu sheria ya muungano ndio inafuata kwa kutungwa na bunge.Hati?nisaidieni hapa wadau,hati ya muungano na sheria ya muungano kipi kinatangulia kingine na kipi kina nguvu kuliko kingine?
Je kupatikana kw hati hiyo ndio kuhalalisha muungano kwamba ni halali?
Kwenye mambo ya msingi kama haya Ikulu hukaa kimya ila ukigisa jambo binafsi la wana ccm watakuja haraka na waraka
Mkuu naunga mkono hoja yako kwa 100%... Kama kuishi na mwanamke kwa miaka 2 inatambulika kisheria kuwa ni ndoa halali iweje watu walioishi zaidi ya miaka 50 wamezaliana, wameendesha mambo yao pamoja, wamekabiliana na changamoto mbalimbali kwa umoja wao IWEJE leo tuseme eti Muungano ni batili kwakuwa eti cheti hakipo! Makubaliano au muungano ni zaidi karatasi yenye maandishi ya watu wawili! Muungano huu Unawakilisha Muungano wa Jamii ya watu wa Znz na Watu wa bara na umedumu kwa nusu karne mpaka sasa! Ukiangalia kwa undani utagundua kuwa pande zote mbili yaani CCM na UKAWA wote wako bias ile mbaya! Mifumo wanayopendekeza yanajikita kwenye political gain zaidi! CCM wajua kuwa ndani ya mfumo wa dola mbili wataendelea kutawala milele daima, UKAWA wanajua kuwa ndani ya dola tatu CCM itakosa nguvu na kuachia ngazi! Kama kweli wote wangekuwa na dhamira ya kweli ninauhakika leo hii Tanzania Ingekuwa Moja chini ya Serikali Moja yenye kuendeshwa kwa mfumo wa Majimbo kama zilivyo nchi za wenzetu..Hoja ya hati ya Muungano ni hoja muflisi kwa kweli.. sijui kwanini watu wasomi wameing'ang'ania hii! Hivi uhalali wa Muungano unategemea uwepo wa haki ya Muungano? Je kama cheti cha ndoa au pete ya ndoa imepotea ina maana ndoa haina uhalali? Hivi uhalali wa mkataba wowote unategemea uwepo wa nyaraka za mkataba huo hasa kama pande zote zinakubaliana kuwa mkataba ulisainiwa na ushahidi wa watu kusaini na yaliyomo mwenye hiyo hati yanajulikana?