Ikulu Yaita Waandishi Wa Habari kuwaonesha Hati Ya Muungano

Ikulu Yaita Waandishi Wa Habari kuwaonesha Hati Ya Muungano

Tunachohitaji ni scanned copy inayoonyesha rangi halisi kwani kuweza kuforge kwa kuunganisha maandishi na na saini za muhusika na kutoa copy ni rahisi tu na inawezekana ndio kilichofanyika. Nahitaji yenye saini za rangi ya kalamu halisi waliyotumia
 
kama nilivyosema anaongelea Hati ya Muungano, anasema hati ipo, na Rais amesema katibu mkuu ailete hati hiyo mbele ya wanahabari, anasema maneno yamekuwa mengi na yanayosemwa ni mengi na hati imetunzwa vizuri sana hadi sasa, na mwenyekiti wa bunge akiiomba basi wataipeleka huko bungeni na nakala ya hati hii itapelekwa makumbusho ili kila mwananchi aweze kuiona,

Nitakuwa wa kwanza kwenda kuiona
 
1538799_858617424152035_7153846776908188865_n.jpg
 
Mara ipo UN,Heee kumbe sefue anayoooo...sasa mbona alikauka nayoooo!!!!kazi ipoo
 
Juu kabisa kama si macho yangu nasoma yafuatayo;

FAX NO. 2117272

Date April 14 2013

Time 09:55am



Je hii ndiyo maandiko ya 1964?

Kwa mujibu wa Sefue ni kwamba iko mbali sana kwenye usalama. Kwa hiyo hata hapo ikulu imeingia kwa fax......kule iliko itaendelea kukaaa. Hati hiyo ipo UN
 
Juu kabisa kama si macho yangu nasoma yafuatayo;

FAX NO. 2117272

Date April 14 2013

Time 09:55am



Je hii ndiyo maandiko ya 1964?

Mkuu hata mimi nilikiona hicho kitu,ila nikajipa moyo kuwa huenda hizo ni kutoka katika headed paper iliotumika wakati wa kupiga kopi au kuprint hiyo document.Au huenda kifaa au/na software kilichotumika kutoa hiyo copy ndicho kimeweka hizo details automatically.nawaza tu kwa sauti
 
Mkuu naunga mkono hoja yako kwa 100%... Kama kuishi na mwanamke kwa miaka 2 inatambulika kisheria kuwa ni ndoa halali iweje watu walioishi zaidi ya miaka 50 wamezaliana, wameendesha mambo yao pamoja, wamekabiliana na changamoto mbalimbali kwa umoja wao IWEJE leo tuseme eti Muungano ni batili kwakuwa eti cheti hakipo! Makubaliano au muungano ni zaidi karatasi yenye maandishi ya watu wawili! Muungano huu Unawakilisha Muungano wa Jamii ya watu wa Znz na Watu wa bara na umedumu kwa nusu karne mpaka sasa! Ukiangalia kwa undani utagundua kuwa pande zote mbili yaani CCM na UKAWA wote wako bias ile mbaya! Mifumo wanayopendekeza yanajikita kwenye political gain zaidi! CCM wajua kuwa ndani ya mfumo wa dola mbili wataendelea kutawala milele daima, UKAWA wanajua kuwa ndani ya dola tatu CCM itakosa nguvu na kuachia ngazi! Kama kweli wote wangekuwa na dhamira ya kweli ninauhakika leo hii Tanzania Ingekuwa Moja chini ya Serikali Moja yenye kuendeshwa kwa mfumo wa Majimbo kama zilivyo nchi za wenzetu..
Kuna mtu aliuliza kama hii analogy ya ndoa ni sahihi kati ya Zanzibar na Tanganyika nani mke nani mme?
 
Wameshachakachua tayari sanaa na usanii kazi ya ccm. Yana mwisho. Vipi saini ya karume ipo wadau mtujuze
 
mbona kuna fax number na tarehe 14 april hii ina maana gani wanajamii hebu tusaidiane kufuatilia hii fax from where

Isije kuwa ni kutoka mbinguni kama hatutaambiwa ilikotoka.


Sent from my iPad using JamiiForums
 
Hati hii halali ya muungano imefanyiwa editing tarehe 14 apr 2013 huko mtaa wa lumumba, na waliowezesha shughuli hiyo ni --------na kiongozi akiwa mr january jr, asanteni sana.
 
Eti CCM wamegushi saini za Hayati Mwl J. K. Nyerere na Abeid Aman Karume, wameongeza me kwa Karume (kitu ambacho si kawaida ktk saini ya mtu alfabeti kuachana) kwa kutumia komputa (Scan > edit>print). Hata hapo naona kuna hiyo dalili. Je ni kweli au?
 
Back
Top Bottom