Ikulu Yaita Waandishi Wa Habari kuwaonesha Hati Ya Muungano

Ikulu Yaita Waandishi Wa Habari kuwaonesha Hati Ya Muungano

Monday, April 14, 2014

Hati Halali ya Muungano hii hapa ikiwa Imesainiwa ORIGINAL na Rais Nyerere na Rais Karume,Hakuna Uchakachuaji hapa

‪#‎HABARI‬ Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue ameonesha hati ya muungano wa Tanzania, kati ya nchi ya Zanzibar na Tanganyika.

Balozi Sefue amewahakikishia Watanzania kuwa nyaraka hizi muhimu ziko salama ila hakuna haja ya kujua ziko wapi.

Balozi Sefue amesema wanaosema kuwa hati hazipo na sahihi zake ni za kughushiwa, ni waongo.
Mambo 11 waliyokubaliana viongozi, wakati Zanzibar na Tanganyika zinaungana pia yameonekana katika hati ya Muungano.

BlL3iXXIcAAc_v6.jpg:large

Hii ndio

hati halali ya Muungano iliyosainiwa na Rais nyerere na Abeid Karume,.Hati yote nitaiweka hapa Soon.

Source: Habari Kwanza

Forgery!!!
 
mkuu unafanya kazi gani maana 24/7 upo nyuma ya laptop unawatumikia wapiga deal wa kaskazini.

naulizwa na wengi swali kama lako ila nitalijibu baada ya ukombozi wa pili kupatikana mwaka 2015,
tujadili hoja kwanza.
'nakupenda tanganyika'
 
Kama imeombwa 50 Years hamna saa hii wameitoa wapi? Si ile ya kugushi? Magamba mmezoea vya kunynga vya kuchinja sifuri.
 
Mkuu naunga mkono hoja yako kwa 100%... Kama kuishi na mwanamke kwa miaka 2 inatambulika kisheria kuwa ni ndoa halali iweje watu walioishi zaidi ya miaka 50 wamezaliana, wameendesha mambo yao pamoja, wamekabiliana na changamoto mbalimbali kwa umoja wao IWEJE leo tuseme eti Muungano ni batili kwakuwa eti cheti hakipo! Makubaliano au muungano ni zaidi karatasi yenye maandishi ya watu wawili! Muungano huu Unawakilisha Muungano wa Jamii ya watu wa Znz na Watu wa bara na umedumu kwa nusu karne mpaka sasa! Ukiangalia kwa undani utagundua kuwa pande zote mbili yaani CCM na UKAWA wote wako bias ile mbaya! Mifumo wanayopendekeza yanajikita kwenye political gain zaidi! CCM wajua kuwa ndani ya mfumo wa dola mbili wataendelea kutawala milele daima, UKAWA wanajua kuwa ndani ya dola tatu CCM itakosa nguvu na kuachia ngazi! Kama kweli wote wangekuwa na dhamira ya kweli ninauhakika leo hii Tanzania Ingekuwa Moja chini ya Serikali Moja yenye kuendeshwa kwa mfumo wa Majimbo kama zilivyo nchi za wenzetu..

Ni halali kabisa Tz kubaki kama ilivyo kama wasomi na wapiga kura wake ndo wanaweza kutoa mawazo kama wewe.ni mawazo ya kipumba..fu kabisa.
 
Kwa kuwa serikali imesema kuwa hati ya Muungano ambayo imekuwa kizungumkuti miaka mingi na mara nyingine ikapelekwa hati Tasa yenye saini feki, sasa italetwa bungeni. Tusubiri tuipokee na tuitendee kazi kama ifuatavyo.

Sasa wote tunajua Maudhui ya Hati ilikuwa ni kwamba masuala ya Muungano ni kumi na Moja. Sasa ikiletwa wote tudai masuala ya Muungano yawe kama ilivyo kwenye Hati Husika. Na sasa tuje tuone wale Wazanzibari wanaotokana na CCM ambao wanasema wanataka serikali mbili kama watakubali Zanzibar irudi kule na kuwa kama ilivyokuwa wakati tumeungana. Aidha tuone kama kweli hawa wazanzibariCCM watakubali kurejea katiba ya Zanzibari iliyokuwepo ambayo inatokana na Hati ya Muungano huo. Niwashukuru sana wale waheshimiwa wachache wenye kuwakilisha kundi kubwa kama kina JUSA, LISU, DUNI, MNYIKA, na wote wanaounga mkono Rasmu ya Mheshimiwa sana Warioba.

mkuu iyo hati haitaijeresha Tanganyika?iyo hati haitasema Tanganyika ni nchi? Naiona Tanganyika ndani ya miwani ya Tanzania...ni imani yangu iyo hati itaitaja Tanganyika, asante wasiira kwa kuileta hati ili iifufue tanganyika!
 
Na ndiyo maana Lisu kawabana kama mwanasheria na wao bila kujijua wamekimbilia kuitoa. Wakishaitoa sasa mambo yanawekwa sawa sasa wale Wazanzibar majuha wa CCM ndio watwambie bado wanakubaliana na yaliyomo kwenye hati au wanayakana. Wakikubali Zanzibar wataiona moto, wakikataa yaliyomo Tanganyika yetu imezaliwa. Ukishajua sheria bwana unaweza kuchezea vichwa vya watu na wao bila kujijua wakaingia mkenge na hapo ndicho anachofanya LISU

Kwa kuwa serikali imesema kuwa hati ya Muungano ambayo imekuwa kizungumkuti miaka mingi na mara nyingine ikapelekwa hati Tasa yenye saini feki, sasa italetwa bungeni. Tusubiri tuipokee na tuitendee kazi kama ifuatavyo.

Sasa wote tunajua Maudhui ya Hati ilikuwa ni kwamba masuala ya Muungano ni kumi na Moja. Sasa ikiletwa wote tudai masuala ya Muungano yawe kama ilivyo kwenye Hati Husika. Na sasa tuje tuone wale Wazanzibari wanaotokana na CCM ambao wanasema wanataka serikali mbili kama watakubali Zanzibar irudi kule na kuwa kama ilivyokuwa wakati tumeungana. Aidha tuone kama kweli hawa wazanzibariCCM watakubali kurejea katiba ya Zanzibari iliyokuwepo ambayo inatokana na Hati ya Muungano huo. Niwashukuru sana wale waheshimiwa wachache wenye kuwakilisha kundi kubwa kama kina JUSA, LISU, DUNI, MNYIKA, na wote wanaounga mkono Rasmu ya Mheshimiwa sana Warioba.
 
Msamiati mpya...muungano = ndoa....kuna nchi mme na nchi mke tuweke katika kamusi na ifundishwe shuleni
 
hii serikali ina la kutuabia kwanini majibu yao yana mkanganyiko mkubwa sana?
Hii naamini ni usanii wa hali ya juu ili kutuaminisha.
Where is my tanga-nyika?

juu ya huo mdole mbona sijaona neno Tanzania??? kumbe kweli Tanganyika ipo ni msukumo mdogo tu inarudi!!
 
Taarifa nilizozipata muda huu ni kuwa Waandishi wa habari wameitwa Ikulu na Katibu Mkuu Kiongozi lengo ni kuwaonyesha Hati Ya Muungano na kukata mzizi wa Fitina Kwa wajumbe wa bunge la Katiba. Tutawajulisha hapa hapa...

Waipeleke Bungeni. Wandishi wataiona huko.
 
Taarifa nilizozipata muda huu ni kuwa Waandishi wa habari wameitwa Ikulu na Katibu Mkuu Kiongozi lengo ni kuwaonyesha Hati Ya Muungano na kukata mzizi wa Fitina Kwa wajumbe wa bunge la Katiba. Tutawajulisha hapa hapa...

Hati ya Muungano inatakiwa na wabunge wa bunge la katiba, sasa badala ya kuwapa wale unaita waandishi wa habari.
 
Hiyo no fax no. Imetumwa tarehe 14 April 2013imetokea wapi hiyo?kwa nini ikulu inachanganya watu? Si wanasema walikuw wameitunza ilikuwa mahali sasa hiyo kutumwa kwa fax ilikuwa wapi
 
Back
Top Bottom