Ikulu Yaita Waandishi Wa Habari kuwaonesha Hati Ya Muungano

Ikulu Yaita Waandishi Wa Habari kuwaonesha Hati Ya Muungano

Bungeni Bongo Movie = Ndiyooooo
Ikulu Bongo Moviee = Ndiyoooooo
 
SIamini na wala sikubali kuwa tuna hati 2 ZA muungano. Ile yenye saini feki iliyopelekwa mwanzo na hii ya Sefue aliyowaonyesha wachaguliwa wa waaandishi habari mchana huu. Naomba majibu haya kwa nini walipeleka hati tofauti bungeni? Je Zanzibar wameapprove kuwa hiyo Ndio kweli halisi? Naona sasa suala la muungano lirudi kwa wananchi.

Hapa ndipo pa kuanzia
 
Mods, Please shughulikia mzushi huyu. Hawezi kuleta uozo humu halafu mkamwacha hivi hivi.

Unawazimu ni wewe...Umepandwa na pepo mchafu..?????

Watu tumetiza live kupitia Star Tv...Sasa sijui unataka kusema nini hapa..
 
Hii ni "COPY" ...

attachment.php

Hii yaelekea imetoka kusiko na jina.
 
Tunachohitaji ni scanned copy inayoonyesha rangi halisi kwani kuweza kuforge kwa kuunganisha maandishi na na saini za muhusika na kutoa copy ni rahisi tu na inawezekana ndio kilichofanyika. Nahitaji yenye saini za rangi ya kalamu halisi waliyotumia

Angalia neno APRIL. Font na hata wino kwenye hilo neno ni tofauti kabisa na text yote. Lakini pia neno hilo hilo APRIL linaonekana kama limendikwa sasa na sio miaka 50 iliyopita!
 
Yote haya kasababisha Pasco wa JF kauliza maswali magumu wanataka kumjibu kwa majibu mepesi

. . . Na mkataba wenyewe tunataka wapewe forensic experts wachunguze fingertips ili tujue kama ni fake au genuine.
 
Hati ya Muungano ni feki. Sahihi ya Karume imechakachuliwa kwani hata jina lake halijaandikwa hadi mwisho limekatwa na kuandikwa kwa chini. Nimeiona kwenye Facebook Wall ya January Makamba. Yaani kwanini jina la Karume herufi " me " imeandikwa kwa chini ya jina husika ? Why ? Alafu sahihi ya Nyerere imepigwa kwa mhuri sio mwandika original

Mkuu this is serious allegation ... Forgery ni criminal offence! Kama utaweza kututhibitishia hili basi lazima kuna mtu ama watu wanawajibishwa kwa uzembe kwani Ikulu tunaamini kuna Best Brains pale ambao wanaweza kutengeneza kitu kikawa zaidi ya Original...Nini kimewakumba hawa waungwana?...
 
Juu kabisa kama si macho yangu nasoma yafuatayo;

FAX NO. 2117272

Date April 14 2013

Time 09:55am



Je hii ndiyo maandiko ya 1964?
Hizo number za fax ni za city centre hapo Dar, kama ni hivyo ni sawa na mie niambiwe nilete cheti cha form wakati mie ni std 7 nachofanya ni kuchukua cheti cha mtu na kukitoa copy then nabandika jina langu alafu ninakituma kwa fax. (Nawaza kwa sauti tu)
 
Muungano wetu ni sawa na x + y = xy + y whereby x = tanganyika, y= zanzibar and xy = tanzania hii nayo tuiweke kama new mathematica ekwesheni kwenye mtaala wetu watoto wetu wasihojihoji iwe fact

...Kweli mkuu!
 
Tunachohitaji ni scanned copy inayoonyesha rangi halisi kwani kuweza kuforge kwa kuunganisha maandishi na na saini za muhusika na kutoa copy ni rahisi tu na inawezekana ndio kilichofanyika. Nahitaji yenye saini za rangi ya kalamu halisi waliyotumia

Nenda Ikulu mkuu!
 
kama wanayo ni vizuri itapunguza kelele maana tulio wengi tumechoka kelele!
 
Kwanini kitu kukitoa mpaka wapige kelele, ushujaa ni wangeendelea kupiga nayo kimya tu kulikoni hivi mpaka watu wapige kelele wee ndio wanatoa. Kumbe hata tukipiga kelele kuhusu wauza unga ambao viongozi wengi wa serikali wanasema wanawajua ipo siku watawataja
 
Back
Top Bottom