Ikulu Yaita Waandishi Wa Habari kuwaonesha Hati Ya Muungano

Ikulu Yaita Waandishi Wa Habari kuwaonesha Hati Ya Muungano

Habari

Nina mashaka na hati hii iliyotolewa leo ikulu eti ni hati halali ya muungano.

KATIBU KIONGOZI OMBENI SEFUE amewaambia waandishi kuwa sasa itawekwa ktk makumbusho sehemu mbalimbali nchini.

Mbona mwanzo haikuwekwa?

MBONA awali hati iliyopelekwa bungeni ilikuwa na utata hasa ktk saini ya JKN?

JE IMEKWENDA KUCHAKACHULIWA BAADA YA AKINA TUNDU NA JUSSA KUCHACHAMAA?

TUJADILI.
Mbona kuna moja waliitoa hao hao wanaojiita 'sisi serikali' ambayo ina saini tofauti? Pili, hivi Karume alikuwa mjinga kiasi gani kusaini hadi jina jingine Libaki na KUMALIZIWA chini? MASHUHUDA WALIOKUWEPO NI NANI? Imechukua siku ngapi kuipata? Acheni kudanganya watu, hiyo hati si lolote si chochote?
 
Nyongeza tazama kwa ufasaha rangi za maandishi ya hizo saini.

https://www.youtube.com/watch?v=15tUVYimdsY

Kweli Mkuu. Vile vile nimeona kama 'Type writer' za 1964 ziliweza kuandika "mwandiko mlazo" yaani 'Italics'. TAZAMA Peoples Republic of Zanzibar chini ya saini ndefu ya Karume. Je kila mtu alitumia wino tafauti kusaini? Tazama wino wa nyerere ulokolea na uko 'intact' tangu 1964 ili hali maandishi menginne yameshakuwa manjano!!! Tazama pia wino alotumia Karume
 
Kumbe tulifanyamakosa kuwatimua wengereza Tanganyika na kuwafukuza masultani zanzibar?

Kwa hoja ya kuishi miaka mingi na utawala,ndoa,au muungano ndio imekua halali tukawaomberadhi wakoloni coz walitawala miaka mingi kuliko muungano wetu wa Tz.
Mkuu ukiwa unajibu hoja kwa kutumia hoja dhaifu inakuwa hujatutendea haki maana JF ni zaidi ya burudani! kwetu sisi JF ni center of Knowledge creation! Reference yako ya wakoloni si SAWA kwani wakolini walituvamia na kututawala kimabavu LENGU kuu kwao ilikuwa kuchukua Rasilimali zetu na kutanua masoko yao! Leo hii situation haijabadilika sana kwani kuna utawala mamboleo unaoendeshwa kwa Mnururisho, Mpitisho na Mnururisho via WB, IMF na Dola Nyang'anyi hususan za Magharibi.... Muungano wetu ulifanyika mwaka 1961 na ulitiwa saini ikifuatiwa na ishara ya muungano kwa kuchanganya udongo... Picha na wale mashuhuda ni ishara tosha kuwa nchi hizi ziliungana na muungano wetu ni halali! Mapungufu yaliyoko kwenye Hati ikiwa ni pamoja na Kero za Muungano ndiyo mambo ya Msingi ya kujadili! Narudia kusema wanaong'ang'ania Serikali 2 na 3 wako kisiasa zaidi kwa maslahi ya vyama vyao! Muungano usiokuwa na mashaka ni muungano wa nchi moja serikali moja ikiongozwa na sera ya majimbo!!
 
mkataba wa inchi inayoitwa Tanganyika na asili yake wewe unaujua uliko? kina nani walioshiriki kutengeneza Tangayika?

Umesoma haya maneno kwenye taarifa ya ikulu?

Ukweli ni kuwa hati hiyo ipo, ilikuwepo siku zote. Hata hivyo, lazima tukubaliane kuwa zipo Hati fulani ambazo ni kiini cha uwepo wetu kama Taifa huru, Jamhuri huru na Muungano huru, ambazo tunazihifadhi kama mboni ya jicho. Hati hizo ni pamoja na Hati ya Uhuru wa Tanganyika ya mwaka 1961, Hati ya Tanganyika kuwa Jamhuri mwaka 1962, na Hati ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ya mwaka 1964. Hati za aina hii zinahifadhiwa maeneo maalum ambayo ni salama ili zisipotee wala kuharibika. Kwa kawaida hatuzitoi, tunazifungua ili kuzihifadhi kwa namna yoyote ile.
 
Mzee Mwanakijiji

Sikutarajia ati ungefananisha muungano wa Tanganyika na Zanzibar na ndoa baina ya mwanamume na mwanamke. Kwa mfano, kati ya Tanganyika na Zanzibar, ni nani mwanamume na nani ni mwanamke? Sikutarajia Mzee Mwanakijiji ungethubutu kutumia mfano huu mfu.

Bado siamini ati Mzee Mwanakijiji unahoji kwa nini Watetezi wa Tanganyika wahoji uhalali wa muungano? Tangu lini Mzee Mwanakijiji hujui kuwa problematizing the normal ndio hujuza uimara ama ubovu wa normality? Tangu lini hulijui hili?

Ama Mzee Mwanakijiji unaamini malengo ya wachache sio kukuza demokrasia bali kubadilisha dola unayoitumikia hivyo kukosa mkate wako?

Pengine ndiyo Shivji huyu Mwanakijiji?
 
Technically Serikali 3 ni kuvunja Muungano uliodumu kwa miaka 50! Watetezi wa Muundo wa serikali mbili hawana hoja za nguvu kuutetea kutokana na mapungufu mengi yaliyoko ...suluhisho hapa ni serikali moja yenye sera ya majimbo...
 
Siamini kama saini ile ni ya Karume, ile saini ni ya kisomi na ya msomi wa hali ya juu kuliko Abeid Amani Karume.
 
kwani iliyoonywesha inasemekana saini zimegushiwa ni ilikuwa inaitwaje?
 
Ya mwanzo na wewe ipi,lini iliwahi kuoneshwa mnakurupuka tu.
wewe hupo nchi gani? halafu na wasi wasi na iq yako juu ya uelewa wa ubongo wako ,ile iliyoonyeshwa imefojiwa saini ilikuwa inaitwaje?
 
tumewashtukia janja yenu, mlitaka mpewe hati za muungano ili mzipige mkauze nchi?? mtaendelea kuziona kwa mbali tu..
 
Antipas Lissu hamna lolote ni kama mazezeta wa sheria wengne tu,kiboko yake Albert Gasper Msando..
Unazungumzia yule msando aliyeshinda kwa kusaidiwa na TISS!? Kubali kataa wamejikanyaga kupita kiasi. Hivi yule Nahodha aliyesema mkataba uko UN alidanganya eti ehh!! Kifo cha nyani!!!!------
 
Naona umelipenda hili kabila kwa sababu ya Udhaifu uliojitokeza kwani limejitahidi kutuingiza katika mchakato ambao linaupinga.

inaonekana akili yako inaishia mwisho wa pua yako, inakuwaje suala la kabila la mtu kuingia hapa? ni jinsi gani gani kabila la mtu lina uhusiano na anachokifanya? unaweza kuniambia ni jambo gani zuri ulilowahi kulifanya linaloshabihiana na kabila lako bora? JADILI MADA MAHUSUSI!!!
 
Tuwekeeni full content ya hati hiyo ili tujue waliyokubaliana. Au waandishi mlipiga picha sehemu ya sahihi tu? Je vipi zile copy alizosema atawapa, au hakuwapa?
 
Siamini kama saini ile ni ya Karume, ile saini ni ya kisomi na ya msomi wa hali ya juu kuliko Abeid Amani Karume.

hasa jinsi herufi A ya Amani ilivyoandikwa...aliyegushi sahihi ya Karume angeniomba ushauri.
 
baada ya yote je iyo hati inaitaja tanzania au tanganyika???????????????
 
BAADA YA HAPO LISSU ALIWAPA TEANA ASSIGNMENT MPYA YA KUTHIBITISHA UHALALI WA WASHIRIKI waliosaini na waliopitisha.
 
Back
Top Bottom