Ikulu yakanusha Rais kusaini Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba!

Ikulu yakanusha Rais kusaini Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba!

Informer

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2006
Posts
1,606
Reaction score
6,672
Ni kwa mujibu wa Taarifa toka Ikulu:
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Leo, Jumatatu, Oktoba 7, 2013, zimetungwa habari, zikaingizwa kwenye Mitandao ya Kijamii na kusambazwa sana zikidai kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ametia saini Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ambao ulipitishwa na Bunge katika Kikao chake cha mwezi uliopita.

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu inapenda kufafanua kama ifuatavyo:

a) Kwanza, Ofisi ya Rais, Ikulu haijapokea Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba. Inawezekana Muswada huo umekwishakutumwa kutoka Bungeni lakini haujamfikia Mheshimiwa Rais. Hivyo, kama haujamfikia, Mhe. Rais hawezi akawa ameutia saini

b) Pili, Muswada huo ukimfikia Mheshimiwa Rais, inatarajiwa kuwa atautia saini kwa sababu Muswada huo umepitia katika mchakato sahihi na halali wa Kikatiba kwa maana ya kufikishwa Bungeni na Serikali, Kujadiliwa na hatimaye kupitishwa na Bunge.

c) Tatu, kama yapo marekebisho ambayo yanaonekana yanafaa kufanywa katika Sheria hiyo, basi yatafanywa na Bunge baada ya Mhe. Rais kuwa ametimiza matakwa ya Kikatiba ya kutia saini Muswada ambao umepitishwa na Bunge kwa kufuatia mchakato sahihi na halali wa Kikatiba.

d) Nne, na wala hii haitakuwa mara ya kwanza kwa Sheria kupitishwa na Bunge, ikatiwa saini na Mhe. Rais na baadaye kufanyiwa marekebisho na Bunge baada ya kuonekana umuhimu wa kufanya marekebisho hayo. Mwishoni mwa mwaka 2012, Sheria ya Marekebisho ya Katiba ilipitia njia hiyo.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.

7 Oktoba, 2013

Na nyingine:
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Ofisi ya Rais, Ikulu, imeanza mawasiliano na viongozi wa vyama vya siasa nchini vyenye hoja kuhusu Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba uliopitishwa karibuni na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa nia ya kuandaa mkutano kati ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi wa vyama hivyo.

Mawasiliano hayo yameanza leo, Jumatatu, Oktoba 7, 2013, kufuatia maelekezo ya Rais Kikwete kwa Ofisi ya Katibu wa Rais.

Kufuatia matukio yaliyotokea Bungeni wakati wa kujadiliwa na kupitishwa kwa Muswada huo mwezi uliopita, na maneno na kauli mbali mbali ambazo zimetolewa na wabunge wa vyama vya upinzani na wadau wengine kufuatia kupitishwa kwa Muswada huo na Bunge, Rais Kikwete katika hotuba yake kwa wananchi Ijumaa iliyopita, Oktoba 4, 2013, alisema kuwa hoja na kauli za wanaopinga Muswada huo zinazungumzika kwa nia njema ya kutafuta mwafaka katika mchakato wa kutafuta Katiba Mpya.

Kwa mujibu wa maandalizi hayo, Ofisi ya Rais, Ikulu inaangalia uwezekano wa kuitisha mkutano huo Jumapili ya Oktoba 13 ama Jumanne ya Oktoba 15, mwaka huu.
 
asante jk,sikiliza upande wa pili ujijengee heshima na kumbukumbu ambyo kamwe haitaftika ndani ya Taifa hili.
 
kikwete bana....ivi kuna watu wanategemea kitu cha maana kutoka kwake kweli...? itakuwa ndoto za mchana
 
Hahahahaha mbavu mabavu mbavu.

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
Tanzania eeee nchi yangu oo tanzania eeee nchi yanguuuuu. Tanzania eeee n chi yangu ooOooooo

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
Hakuna mahali popote duniani ambapo mswada wa sheria uliopitishwa kihalali bungeni watu hupita mitaani na kutembea jangwani wakinshinikza asiusaini. Nikirudi kwa kauli yake kwamba wabunge warudi bungeni wafanye marekebisho hakuamaanisha kuwa mswada hatausaini. Sana sana alichosema ambacho nataka watu fulani ambao vichwa vyao ni vigumu kuelewa waelewe kuwa Mh Rais alizungumzia kanuni za Bunge kuhusu kamati ya Bunge ya sheria na katiba kutoenda Zanzibar. Baada ya maelezo yake akasema hakuna mahali popote, narudia hakuna mahali popote ambapo kanuni za kudumu za bunge zinasema kamati (yoyote) inabidi iende Zanzibar na kama wabunge wanaona iwe hivyo basi warudi Bungeni wafanye marekebisho ya kanuni. Sasa bahati mbaya kuna watu uelewa wao ni hafifu na wako humu kijiweni; walidhani Mh KASEMA MSWADA URUDI BUNGENI, UFINYU WA FIKRA NA UDHAIFU WA KUELEWA uliwafanya hawa DUNDUNDU wadhani kihivyo na kuanza kusherehekea ufinyu wao wa kuelewa. Ndani mwao kuna wengine wanaelewa alichosema Mh Rais lakini kwa kuwa wanaona wakiwaelimisha alichosema Mh watawachukia kwa kuwa vichwa vimejaa maji tu yaani ni watu wanaoelewa kutokuelewa. Mmoja wao ni Tundu, huyu anajua alichosema Mh Rais lakini amaeacha DUNDUNDU wachemke wenyewe wakidhani yupo pamoja nao. Fikiri kabla ya kutenda, na Waingereza wana msemo mzuri tu kwa kiswahili kisicho rasmi unasema, husiseme kabla hujafanya utafiti maana utaonekana boya na kituko.:frusty:
 
Watu acheni USHAMBA. Mswada kutiwa saini haimaanishi kuwa hauwezi kurekebishwa.

Kila sheria iliyopo kwenye vitabu vyetu inaweza kurekebishwa. Sheria pekee zisizoweza kurekebishwa ni zile zilizotoka kwa Mungu zilizopo kwenye vitabu vitakatifu.
 
Chezeya nguvu ya umma weye!!!
 
foleni tuuuu ili li saa la 2 natamba kwwenye foleniiiiiiii..... Ngoja tusubiri ngojera tena
 
Hahahaha,leo nyuzi kweli zimekua nyuzi yaani kote ni hot sijui nijigawe vipi.
Mswaada utasainiwa,then kama kuna mabadiliko yanazungumzika,then utarudi tena bungeni,huh?.
 
Hakuna mahali popote duniani
ambapo mswada wa sheria uliopitishwa kihalali bungeni watu hupita
mitaani na kutembea jangwani wakinshinikza asiusaini. Nikirudi kwa kauli
yake kwamba wabunge warudi bungeni wafanye marekebisho hakuamaanisha
kuwa mswada hatausaini. Sana sana alichosema ambacho nataka watu fulani
ambao vichwa vyao ni vigumu kuelewa waelewe kuwa Mh Rais alizungumzia
kanuni za Bunge kuhusu kamati ya Bunge ya sheria na katiba kutoenda
Zanzibar. Baada ya maelezo yake akasema hakuna mahali popote, narudia
hakuna mahali popote ambapo kanuni za kudumu za bunge zinasema kamati
(yoyote) inabidi iende Zanzibar na kama wabunge wanaona iwe hivyo basi
warudi Bungeni wafanye marekebisho ya kanuni. Sasa bahati mbaya kuna
watu uelewa wao ni hafifu na wako humu kijiweni; walidhani Mh KASEMA
MSWADA URUDI BUNGENI, UFINYU WA FIKRA NA UDHAIFU WA KUELEWA uliwafanya
hawa DUNDUNDU wadhani kihivyo na kuanza kusherehekea ufinyu wao wa
kuelewa. Ndani mwao kuna wengine wanaelewa alichosema Mh Rais lakini kwa
kuwa wanaona wakiwaelimisha alichosema Mh watawachukia kwa kuwa vichwa
vimejaa maji tu yaani ni watu wanaoelewa kutokuelewa. Mmoja wao ni
Tundu, huyu anajua alichosema Mh Rais lakini amaeacha DUNDUNDU wachemke
wenyewe wakidhani yupo pamoja nao. Fikiri kabla ya kutenda, na
Waingereza wana msemo mzuri tu kwa kiswahili kisicho rasmi unasema,
husiseme kabla hujafanya utafiti maana utaonekana boya na
kituko.:frusty:

mkuu, umeeleweka sana. unajua akili za bavicha ni kama supu iliyowekwa tui la nazi vile. yaani akili zao zinakimbilia kuganda tu
 
Hiyo ndiyo habari ya mjini. Mswada ni lazima usainiwe
 
huyu mzee bana sijui yokoje! yaani kama urais ndo hivi basi nchi hii ina bahati mbya sana ....
 
Ni majanga kuongozwa na rais Wa KUAMBIWA. Nina mashaka hatausoma ATAAMBIWA AUSAINI.sasa kama hajausoma ile hotuba ya juzi aliitoa ya nini? Nina mashaka hata ile hotuba ALIAMBIWA aisome ilivo...terrible
 
Back
Top Bottom