Ikulu yakanusha Rais kusaini Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba!

Ikulu yakanusha Rais kusaini Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba!

Kwahiyo BAVICHA mabango yetu hayana kazi tena? Au maandamano bado yapo palepale?
 
Hawa viongozi wetu wa CHADEMA ni walaghai. Wanapenda kututumia ili wapate nafasi ya kwenda Ikulu kunywa maji ya matunda.

Wanatutangazia maandamano halafu wakishaitwa Ikulu maandamano yanafutwa.
 
Mbona kichwa cha Habari Na Habari Yenyewe Ni Tofauti?Hiyo DIVIDE AND RULE Iko Wapi?
 
hizo hoja zote hapo 3, kuhusu znz kutoshirikishwa, wabunge wa bunge la katiba, na kuvunjwa tume ya katiba yashatolewa ufafanuzi na rais. Sasa kinachofanyika hapo ni kwa viongozi hao kwenda Ikulu kuchukua ushaur ni vipi watawaeleza wafuasi wao.

chezea siasa wewe,
Wenzenu wanakwenda ikulu nyinyi jasho la meno linawatoka.
 
Wewe kwa akili yako unafikiri hawa ccm pamoja na mwenyekiti wao bila shuruti kama hizi wanasikia kitu?hujui kama huo muswada unaenda kufanyiwa amendment unafaida kwako na kw familia yako?jitambue wewe!
 
Hawa viongozi wetu wa CHADEMA ni walaghai. Wanapenda kututumia ili wapate nafasi ya kwenda Ikulu kunywa maji ya matunda.

Wanatutangazia maandamano halafu wakishaitwa Ikulu maandamano yanafutwa.

Hivi wewe gamba ikulu kuna duka la juice? Huna kazi ndiyo maana hata hujui bei ya juisi. Hata hivyo, ikulu ni ya Watanzania wote, wapinzani inclusive. Kwa hiyo hela ya juice na chai ni budgetted for. Hao ni wageni wa rais na siyo wa mwenyekiti wa CCM.
 
Chonde chonde viongozi wetu jamani,mkianza kwenda kwa mafungu wakati mnachopigania ni kitu kimoja mjue hilo ni bao la kisigino?

LIPUMBA,MBOWE,MBATI<LMM> Nendeni nyote kwa pamoja ni bora mkapunguza wapambe wenu kama viti vya ikulu havitoshi kuliko kwenda kwa mafungu maana badaye mtaanza kulaumiana,ni bora lawama zije kwa wote kama mlivyo maana hata Rais kwenye hotuba yake kawaiteni nyote tena kwa majina ya vyama vyenu,so pls pls hizo barua mlizoletewa zijibiwa kuwa hatuko tayari kuja kwa mafungu bali tunakuja kama tulivyo:

Ni wito tu:
 
Jf hongereni sana kwa hili: Nukuu na kanushi hii inahusu jf humuhumu. Wengine walicopy. Inaonyesha jinsi gani mitandao ya kijamii inavyoongezeka kuwa na gnuvu ya nukuu (authencity) na huu ni ushahidi tosha ukiachilia mbali nukuu za raisi katika hotuba zake. Nguvu ya uma kimtandao hasa kupitia mitandao ya kijamii ni kiini kikubwa cha mabadiliko. Wana jf ongezeni nguvu.
 
Kumbe maneno yote yale hata muswaada wenyewe hajausoma? Sasa yale aliyosema yanajadilika kayatoa wapi? Au ndiyo yale ya NIMEAMBIWA?

Hivi inachukua siku ngapi kwa Documet kutoka Bungeni mpaka Ikulu?
Au Umetumwa kwa kutumia Bajaji?

Alafu kumbe ajausoma wala kuuona, ndio maana ilikuwa nimeambiwa, nimesikia, nimesimuliwa. Sasa aliusemea vipi na ilihali ajuhi hata ukoje?

Duhhh hii nchi kweli, sasa mheshimiwa alipokuwa analihutubia taifa na kusema hoja zinajadilika kumbe hata hajausoma?Kweli tusitegemee katiba mpya hapa,kila kitu ni viinimacho tu na mazingaombwe!
 
"Heri mimi sijasema." Ninachowakumbusha Viongozi wa Upinzani walioitwa huko juu kwamba kwamba kwa kila dakika, sekunde,hata nukta ya mazungumzo yao,wasiusahau umma wa Watanzania walioko nyuma yao. Yaani ikiwezekana waongee wakiwa wamekaa chini sakafuni,kuliko namna yoyote ile itakayowafanya kunyamaza mara wakishatoka huko.
 
hata vijuisi wasinywe kabisa. wamaanishe serious business
 
Back
Top Bottom