Ikulu yakanusha Rais kusaini Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba!

Ikulu yakanusha Rais kusaini Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba!

mi sijawahi ona wala kusikia mtu anasaini kitu ambacho hajakipata na kukiangalia kwa kina.

lkn kwa hawa washikaji wamegeuza magogoni ni sehemu ya kupiga soga basi si ajabu rasimu ya marekebisho ya katiba ikasainiwa bila ya mkuru kuupitia na kuosoma kwa makini kwani yeye huridhika na soga za kuambiwa,kusikia na kuelezwa.

Haya kazi kwako chifu Mangungo wa msovero, wananchi tunasubiria another bogus treaty.

Kifupi hapo hakuna jipya toka kwa mshua kwani jamaa anaona hatua moja mbele toka pale aliposimama.

nchi ya majuha hii,watu wanajiburuzia watakavyo.

eeeeeeee tanganyika na watanganyika ,uu wapi utanganyika wenu mlioupigania toka kwa mkoloni mweupe? ona sasa vibaka" wakoloni weusi" wanavyoichezea nchi hii ,yenye kila aina ya neema toka kwa mungu, mithili ya mpira wa kona waushupaliavyo wachezaji uwanjani.

enyi watanganyika tusimame kidete kupigania mkataba wetu sisi wananchi dhidi ya viongozi tunaowapa mamlaka ili kuweza kuliletea taifa maendeleo.

tusikubali vibaka hawa wachache wahodhi kila kitu kinachohusu taifa na uhai wa wananchi wake kwa ujumla.

We have to stand up firm and fight for our own rebirth after a long spell of life under corruption,bribery,mismanagement as well as squandering.

So much exhausted with this sort of bondage that we were used to.
Need to be exonerated from all those agonies that selfish leaders whom we vested our interests have gone astray.

But enough jibber...jabbering here, is on whether the issue get materialized as many would wish it to happen under these arrogant leaders.

#so_obsessed .
 
Hakuna mahali popote duniani ambapo mswada wa sheria uliopitishwa kihalali bungeni watu hupita mitaani na kutembea jangwani wakinshinikza asiusaini. Nikirudi kwa kauli yake kwamba wabunge warudi bungeni wafanye marekebisho hakuamaanisha kuwa mswada hatausaini. Sana sana alichosema ambacho nataka watu fulani ambao vichwa vyao ni vigumu kuelewa waelewe kuwa Mh Rais alizungumzia kanuni za Bunge kuhusu kamati ya Bunge ya sheria na katiba kutoenda Zanzibar. Baada ya maelezo yake akasema hakuna mahali popote, narudia hakuna mahali popote ambapo kanuni za kudumu za bunge zinasema kamati (yoyote) inabidi iende Zanzibar na kama wabunge wanaona iwe hivyo basi warudi Bungeni wafanye marekebisho ya kanuni. Sasa bahati mbaya kuna watu uelewa wao ni hafifu na wako humu kijiweni; walidhani Mh KASEMA MSWADA URUDI BUNGENI, UFINYU WA FIKRA NA UDHAIFU WA KUELEWA uliwafanya hawa DUNDUNDU wadhani kihivyo na kuanza kusherehekea ufinyu wao wa kuelewa. Ndani mwao kuna wengine wanaelewa alichosema Mh Rais lakini kwa kuwa wanaona wakiwaelimisha alichosema Mh watawachukia kwa kuwa vichwa vimejaa maji tu yaani ni watu wanaoelewa kutokuelewa. Mmoja wao ni Tundu, huyu anajua alichosema Mh Rais lakini amaeacha DUNDUNDU wachemke wenyewe wakidhani yupo pamoja nao. Fikiri kabla ya kutenda, na Waingereza wana msemo mzuri tu kwa kiswahili kisicho rasmi unasema, husiseme kabla hujafanya utafiti maana utaonekana boya na kituko.:frusty:

Ila hao sio dundundu kama yule dundundu wa ikulu sliyejigamba ITV kuwa hawatawaita tena wapinzani ikulu...
 
Mwenyezi Mungu anisamehe bure na aniepushe na mkono na mkono wa chuma.

1. Ikulu ina kiri kuwa raisi hajaupokea muswaada na haujapelekwa kwake that means hajausoma maana haujamfikia! yale aliyoyatoa kwenye hotuba yake huku muswaada ukiwa haujafika ikulu kayatoa wapi?! au nayo kaambiwa na akaja kutuambia? si alisha sema akili za kuambiwa changanya na zako? yeye zake alizichanganya naza nani?!

2. Tamko la ikulu linaonyesha ombwe, yaani lina muamulia raisi kusaini mswaada wakati yeye ndiye mwenye mamlaka?! huku sio kumdharau na kuzadharau uwezo wa raisi kweli?! kwani kama muswaada ukipelekwa ikulu mwenye dhamana ya kusaini au kutokusaini ni nani? mpaka aambie saini kwa kuwa yeye hana maamuzi au anasaini kwa utashi na maslahi ya taifa?!

3. wale wazee (hasa wasira) waliosema rais ameshafunga milango ya ikulu na hahitaji kuonana na wapinzani alitumwa na nani mbona kurugenzi tukufu ya ikulu haija wahi kumkanusha wala kukanusha kuwa ile haikuwa kauli ya rais?! hii kurugenzu inayoleta taarifa za ikulu kuandaa mkutano na viongozi wa upinzani ni ile ile aliyowahi kuisemea wasira au hii ni nyingine?!

chaguo la Mungu mbona halifanyi kama machaguo ya Mungu?!
 
Hakuna mahali popote duniani ambapo mswada wa sheria uliopitishwa kihalali bungeni watu hupita mitaani na kutembea jangwani wakinshinikza asiusaini. Nikirudi kwa kauli yake kwamba wabunge warudi bungeni wafanye marekebisho hakuamaanisha kuwa mswada hatausaini. Sana sana alichosema ambacho nataka watu fulani ambao vichwa vyao ni vigumu kuelewa waelewe kuwa Mh Rais alizungumzia kanuni za Bunge kuhusu kamati ya Bunge ya sheria na katiba kutoenda Zanzibar. Baada ya maelezo yake akasema hakuna mahali popote, narudia hakuna mahali popote ambapo kanuni za kudumu za bunge zinasema kamati (yoyote) inabidi iende Zanzibar na kama wabunge wanaona iwe hivyo basi warudi Bungeni wafanye marekebisho ya kanuni. Sasa bahati mbaya kuna watu uelewa wao ni hafifu na wako humu kijiweni; walidhani Mh KASEMA MSWADA URUDI BUNGENI, UFINYU WA FIKRA NA UDHAIFU WA KUELEWA uliwafanya hawa DUNDUNDU wadhani kihivyo na kuanza kusherehekea ufinyu wao wa kuelewa. Ndani mwao kuna wengine wanaelewa alichosema Mh Rais lakini kwa kuwa wanaona wakiwaelimisha alichosema Mh watawachukia kwa kuwa vichwa vimejaa maji tu yaani ni watu wanaoelewa kutokuelewa. Mmoja wao ni Tundu, huyu anajua alichosema Mh Rais lakini amaeacha DUNDUNDU wachemke wenyewe wakidhani yupo pamoja nao. Fikiri kabla ya kutenda, na Waingereza wana msemo mzuri tu kwa kiswahili kisicho rasmi unasema, husiseme kabla hujafanya utafiti maana utaonekana boya na kituko.:frusty:

mbona jazba zimekupanda namna hii??
au wewe ni wassira umechukia mwenyekiti wako kakuangusha??
 
Rais Kikwete ana mambo ambayo Watanzania watamkumbuka pindi atakapomaliza kipindi chake, mojawapo ni katiba mpya.

Tatizo hapa ni kwamba watu wanasahau haraka, ikumbukwe watu kutoka chama chake walisema katiba tulionayo ni nzuri na hatuhitaji mpya, lakini Rais kwa kuzisoma vema alama za nyakati akaanzisha mchakato wa katiba mpya.

Nchi hii ni yetu sote, na kama alivyosema mwenyewe katiba inayoandikwa si ya vyama vya siasa bali ni ya Watanzania wote afterall Watanzania tuko zaidi ya milioni 45, wanachama hai wa vyama vya siasa vyote kwa pamoja hawafiki milioni 10 leo hii watu milioni 10 kwa sababu ya maslahi yao binafsi wanataka eti wao ndio waamue hatma ya nchi kwa niaba ya wale milioni 35, No Rais asikubali. Watu wenye busara bado wanakumbuka ushauri wake 'akili ya kuambiwa changanya na yako'.

Rais yuko katika njia sahihi akifanikisha kuwapatia Watanzania katiba mpya inayokubalika atakuwa ameweka rekodi ambayo haitavunjwa kwa zaidi ya miaka 100 ijayo.

AKILI YA KUAMBIWA CHANGANYA NA YAKO.
 
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu inapenda kufafanua kama ifuatavyo:

a) Kwanza, Ofisi ya Rais, Ikulu haijapokea Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba. Inawezekana Muswada huo umekwishakutumwa kutoka Bungeni lakini haujamfikia Mheshimiwa Rais. Hivyo, kama haujamfikia, Mhe. Rais hawezi akawa ameutia saini.

Hapa napata shida kidogo;Kwanza tumehakikishiwa kwamba Muswada haujapokelewa ofisi ya rais ikulu.Tunaambiwa eti huenda umeshatumwa lakini bado haujamfikia rais.

Najiuliza kama umeshatumwa unawezekana upo kwa nani mpaka mkurugenzi wa habari asijue?

Kama hana uhakika kama umetumwa au la kwanini asiwaulize bunge ili awe na uhakika anapoongelea jambo zito kama hili?Inawezekana hana mawasiliano na bunge?

Muswada unatumwa ikulu kwa njia gani?Inawezekana umekwama au umepotea njiani?

Inawezekana kweli jambo zito kama hili lisijulikane liko wapi alafu watu walichukulie POA TU?
 
Good....Theory imefanya kazi effectively kuliko muda wowote mwingine.
 
Kweli hii nchi ni Mungu tu anajua tunaelekea wapi. Hivi Kilaza ni Rais wetu au watu waliomzunguka? Yaani inamaana bunge lilituma hizo document kwa njia ya posta na zikapotelea posta au DHL wamezipoteza. Kweli kuwa kiongozi Africa ni Rais sana. Hivi ingekuwa ni Ofisi ya Obama au Cameron ndo wanasema hivi sijuhi vyombo vya habari kama vingewaponyesha.
 
"nimeambiwa kuwa muswada huu unajadilika"
 
Kumbe maneno yote yale hata muswaada wenyewe hajausoma? Sasa yale aliyosema yanajadilika kayatoa wapi? Au ndiyo yale ya NIMEAMBIWA?

Ngoma ilishafika ikulu sema ni lazima watafute sababu za kwanini rais hakuusaini mswaada uliopita kihalali kama wanavyodai wenyewe. Wenyewe wanaona watu wanaweza wakahoji kwanini muda wote huo rais anao muswaada na bado hajausaini!! In other words walikuwa wanapima upepo kwanza!!
 
Hakuna mahali popote duniani ambapo mswada wa sheria uliopitishwa kihalali bungeni watu hupita mitaani na kutembea jangwani wakinshinikza asiusaini.Nikirudi kwa kauli yake kwamba wabunge warudi bungeni wafanye marekebisho hakuamaanisha kuwa mswada hatausaini.
Nitolee maelezo hapo kwenye nyekundu kwa faida ya wadau. Ilikuwa kule Ufaranza mfalme Louis XVI alitumia sheria kandamizi kuendesha nchi kama mali yake. Hakuitisha bunge kwa miaka 175, ancien regime ilikuwa inatawala kwa kutumia mabavu na vitisho. Wafaranza walipochoka mwaka 1789 Mei walilazimisha kuitisha bunge (Estates General - first estste ya mamwinyi, second estate ya kanisa na third estate ya wavuja jasho na wakulima). Mfalme kwa kutumia wabunge wa 1st na 2nd estates kw kutumia kanuni za hovyo wakutunga sheria za kuwakandamiza wanyonge. Kilichufuta wanyonge (3rd estate) wakatangaza kujiunda kama bunge la taifa-nationl assembly ili kutetea wanyonge (milioni 23).

Kuona tishio hilo Louis aliwafukuza ukumbini kwa kutumia polisi. Jamaa wale walienda "jangwani" ya kule ilikuw ni tennis court wakachukua kiapo na ndipo the most celebrated French Revolution was planned and finally put into action by first, storming the Bastille (maximum security prison) July 14th 1789, beheading King Louis XVI and his wife Queen Marie Antoinette by guillotine, declaring the rights of man and the citizen, and a constitution republic was put in place. Miswada inaweza kupitishwa mahali popote kutegemea na mazingira yaliyopo na aina ya watu wanaohusika.

Hakuna mtu aliyekuw arrogant kama Antoinette aliwahi kuwaambia wanawake wakati wakiandamana kwa kukosa mkate "if they don't have bread, tell them to eat cake" Mwisho wa yote aliishia kwenye guillotine na hilo haliwezi kutokea mahalipengine hata kama ni Tanzania. Chezea walalahoi na wavuja jasho.
 
asisaini hawa wahuni wa ccm wabunge wajinga sanaa
 
Haukumfikia mheshimiwa Rais sasa alipata wapi nguvu ya kuuzungumzia!Under what basis au ndo ile ya akili ya kuambiwa changanya na ya kwako!!

Ni kwa mujibu wa Taarifa toka Ikulu:

Na nyingine:
 
Kuna mtu alisema "Hakuna chai ya wapinzani Ikulu". Tunaangalia tu bila kufikiria.
 
Wassira alikuwa yuko sahihi na aliwaeleza jambo hilihili hawa jamaa sasa taratibu watarudi kwenye mstari.
 
Back
Top Bottom