Safari hii Press release ya Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu ina nafuu sana. Haina mipasho kama statements za nyuma.
Kuhusu rais ku-sign muswada. Ni kifungu gani cha sheria kinamtaka rais a-sign muswada hata kama anaamini muswada huo ni mbovu? Ukisoma statement ya Ikulu inaonekana kama - kisheria- Rais hawezi kukataa ku-sign muswada ukishapitishwa bungeni. Hii ni sahihi?
Asante kwa kuliona hilo mkuu!
Na mimi niulize, ikiwa ni kweli kuwa endapo mswada umeshatoka kihalali bungeni (kama wanavyodai) hivyo LAZIMA usainiwe kwanza alafu marekebisho yafuate baadae, je ni kwanini huwa hukumu halali zinazotolewa kihalali na Mahakama za watu kunyongwa huwa marais wetu hawalazimiki kuzisaini mara moja zifikapo Ikulu ili sheria ifate mkondo wake? Ni kijiswali tu cha kizushi!