Ikulu yakanusha Rais kusaini Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba!

Ikulu yakanusha Rais kusaini Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba!

Watu acheni USHAMBA. Mswada kutiwa saini haimaanishi kuwa hauwezi kurekebishwa.

Kila sheria iliyopo kwenye vitabu vyetu inaweza kurekebishwa. Sheria pekee zisizoweza kurekebishwa ni zile zilizotoka kwa Mungu zilizopo kwenye vitabu vitakatifu.

Utabadilisha sana kauli mwaka huu!
 
Kwanza niweke hapa taarifa hii rasmi ya Ikulu:

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Leo, Jumatatu, Oktoba 7, 2013, zimetungwa habari, zikaingizwa kwenye Mitandao ya Kijamii na kusambazwa sana zikidai kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ametia saini Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ambao ulipitishwa na Bunge katika Kikao chake cha mwezi uliopita.

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu inapenda kufafanua kama ifuatavyo:

a) Kwanza, Ofisi ya Rais, Ikulu haijapokea Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba. Inawezekana Muswada huo umekwishakutumwa kutoka Bungeni lakini haujamfikia Mheshimiwa Rais. Hivyo, kama haujamfikia, Mhe. Rais hawezi akawa ameutia saini

b) Pili, Muswada huo ukimfikia Mheshimiwa Rais, inatarajiwa kuwa atautia saini kwa sababu Muswada huo umepitia katika mchakato sahihi na halali wa Kikatiba kwa maana ya kufikishwa Bungeni na Serikali, Kujadiliwa na hatimaye kupitishwa na Bunge.

c) Tatu, kama yapo marekebisho ambayo yanaonekana yanafaa kufanywa katika Sheria hiyo, basi yatafanywa na Bunge baada ya Mhe. Rais kuwa ametimiza matakwa ya Kikatiba ya kutia saini Muswada ambao umepitishwa na Bunge kwa kufuatia mchakato sahihi na halali wa Kikatiba.

d) Nne, na wala hii haitakuwa mara ya kwanza kwa Sheria kupitishwa na Bunge, ikatiwa saini na Mhe. Rais na baadaye kufanyiwa marekebisho na Bunge baada ya kuonekana umuhimu wa kufanya marekebisho hayo. Mwishoni mwa mwaka 2012, Sheria ya Marekebisho ya Katiba ilipitia njia hiyo.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais.

Taarifa husika ililenga kukanusha jambo moja tu: kwamba Rais Jakaya Mrisho Kikwete hajasaini Muswada wa Katiba kama ilivyoripotiwa kwenye mitandao hapa nchini leo hii. Ni taarifa nzuri ili wananchi wasipotoshwe. Kurugenzi hadi hapo ilifanya kazi yake ipasavyo.

Lakini, Kurugenzi imevuka mipaka.Kwa kanusho hilo tu,hakukuwa na haja ya kuwa na aya zinazoanza na 'pili', 'tatu' na 'nne'. Aya hizi zinarejesha 'chokochoko' zisizo na msingi ambazo Rais analenga kuzimaliza. Kwenye aya hizi kuna ubabe usio na tija na ramli ya kuogofya.

Nani kaiambia Kurugenzi kuwa Rais atausaini Muswada husika ukimfikia? Wanamlazimisha Rais aendane na mazoea hata katika mambo ya maslahi kwa Taifa? Kwanini?

Nazipinga aya hizo kwa nguvu zangu zote. Na msisitizo uliowekwa katika aya inayoanza na 'Pili' ni wa kuogofya na kuupuuza. Ni msisitizo usio na tija na wenye nia ya kuvuruga mshikamano wetu juu ya Katiba mpya. Kikatiba, Rais halazimiki kusaini Muswada wowote.

Naiomba Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu iepuke 'makosa ya wazi' kama haya siku nyingine. Aya iliyoanza na 'Kwanza' ilikuwa inatosha kabisa. Kurugenzi isivuke mipaka yake. Tafadhali.

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
 
Hatuna rais,
anatumia maneno "nimeambiwa,nimesikia,nimesimuliwa" kuusemea mswada ambao hata hajausoma akajua una nini,bogus rais ever
Msiumize kichwa bure Mh Rais ameshausoma huo mswada na kujifanya kusema nimeambiwa au nimesikia ni lugha tu ,tusubiri matokeo ya kurudishwa bungeni
 
ni Rais rahisi wa watu rahisi ndiyo maana hata mambo anayachukulia kirahisi na watu wanayakubakubali kirahisi tu.
 
View attachment 115589
habari zilizo sahihi lakini zimekuja kama tetesi ni kwamba muswada wa mabadiriko ya katiba umemwagiwa wino tayari kurudi bungeni.
Nini kinakuja kwa muungano wa wapinzani na nini hatima ya tume ya warioba .

Ukidhani kuitwa ikulu ni suruhu basi amini hata kwenye javi chai ipo.
 
kwanza niweke hapa taarifa hii rasmi ya ikulu:

taarifa kwa vyombo vya habari

leo, jumatatu, oktoba 7, 2013, zimetungwa habari, zikaingizwa kwenye mitandao ya kijamii na kusambazwa sana zikidai kuwa rais wa jamhuri ya muungano wa tanzania, mheshimiwa jakaya mrisho kikwete ametia saini muswada wa sheria ya marekebisho ya sheria ya mabadiliko ya katiba ambao ulipitishwa na bunge katika kikao chake cha mwezi uliopita.

Kurugenzi ya mawasiliano ya rais, ikulu inapenda kufafanua kama ifuatavyo:

A) kwanza, ofisi ya rais, ikulu haijapokea muswada wa sheria ya marekebisho ya sheria ya mabadiliko ya katiba. Inawezekana muswada huo umekwishakutumwa kutoka bungeni lakini haujamfikia mheshimiwa rais. Hivyo, kama haujamfikia, mhe. Rais hawezi akawa ameutia saini

b) pili, muswada huo ukimfikia mheshimiwa rais, inatarajiwa kuwa atautia saini kwa sababu muswada huo umepitia katika mchakato sahihi na halali wa kikatiba kwa maana ya kufikishwa bungeni na serikali, kujadiliwa na hatimaye kupitishwa na bunge.

C) tatu, kama yapo marekebisho ambayo yanaonekana yanafaa kufanywa katika sheria hiyo, basi yatafanywa na bunge baada ya mhe. Rais kuwa ametimiza matakwa ya kikatiba ya kutia saini muswada ambao umepitishwa na bunge kwa kufuatia mchakato sahihi na halali wa kikatiba.

D) nne, na wala hii haitakuwa mara ya kwanza kwa sheria kupitishwa na bunge, ikatiwa saini na mhe. Rais na baadaye kufanyiwa marekebisho na bunge baada ya kuonekana umuhimu wa kufanya marekebisho hayo. Mwishoni mwa mwaka 2012, sheria ya marekebisho ya katiba ilipitia njia hiyo.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya mawasiliano ya rais.

Taarifa husika ililenga kukanusha jambo moja tu: Kwamba rais jakaya mrisho kikwete hajasaini muswada wa katiba kama ilivyoripotiwa kwenye mitandao hapa nchini leo hii. Ni taarifa nzuri ili wananchi wasipotoshwe. Kurugenzi hadi hapo ilifanya kazi yake ipasavyo.

Lakini, kurugenzi imevuka mipaka.kwa kanusho hilo tu,hakukuwa na haja ya kuwa na aya zinazoanza na 'pili', 'tatu' na 'nne'. Aya hizi zinarejesha 'chokochoko' zisizo na msingi ambazo rais analenga kuzimaliza. Kwenye aya hizi kuna ubabe usio na tija na ramli ya kuogofya.

Nani kaiambia kurugenzi kuwa rais atausaini muswada husika ukimfikia? Wanamlazimisha rais aendane na mazoea hata katika mambo ya maslahi kwa taifa? Kwanini?

Nazipinga aya hizo kwa nguvu zangu zote. Na msisitizo uliowekwa katika aya inayoanza na 'pili' ni wa kuogofya na kuupuuza. Ni msisitizo usio na tija na wenye nia ya kuvuruga mshikamano wetu juu ya katiba mpya. Kikatiba, rais halazimiki kusaini muswada wowote.

Naiomba kurugenzi ya mawasiliano ikulu iepuke 'makosa ya wazi' kama haya siku nyingine. Aya iliyoanza na 'kwanza' ilikuwa inatosha kabisa. Kurugenzi isivuke mipaka yake. Tafadhali.

mzee tupatupa wa lumumba, dar es salaam

nafikiri amesaini tayari. Cha kujadiri hapa ni nini cha kufanya kisheria? Ameusaini tayari!!!
 
a) Kwanza, Ofisi ya Rais, Ikulu haijapokea Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba. Inawezekana Muswada huo umekwishakutumwa kutoka Bungeni lakini haujamfikia Mheshimiwa Rais. Hivyo, kama haujamfikia, Mhe. Rais hawezi akawa ameutia saini
Eti hii ndio statement ya IKULU? Ndio maana Usalama wa Taifa unavunjwa.shame on you Ikulu guyz
 
TISS wanapima upepo, october 10 ipo pale pale...
 
View attachment 115589
habari zilizo sahihi lakini zimekuja kama tetesi ni kwamba muswada wa
mabadiriko ya katiba umemwagiwa wino tayari kurudi bungeni.
Nini kinakuja kwa muungano wa wapinzani na nini hatima ya tume ya
warioba .

Ukidhani kuitwa ikulu ni suruhu basi amini hata kwenye javi chai
ipo.

hapo ndo ninapompendea JK kama kweli kasaini. angalia lakini usije kula ban kama mwenzako alivyoshughulikiwa
 
Kama JK hataki kila basi kuwe ma katiba ya kila chama, wale wa CcM wawe na katiba yao na sehemu yao wanayoishi sisi TPP Maendeleo hivyohivyo kila mtu hivyo hivyo at the end nchi inagawanywa vipande vipande kila mtu kwake ukienda nchi nyingine eg Kigoma unaingia kwa passport vivyo hivyo wanaotoka.
 
Roho yangu inaniaminisha kwamba Kikwete alishasaini mswada

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
wale waliokuwa wanatoka povu humu JF wapo wapi?
 
Hakuna mahali popote duniani ambapo mswada wa sheria uliopitishwa kihalali bungeni watu hupita mitaani na kutembea jangwani wakinshinikza asiusaini. Nikirudi kwa kauli yake kwamba wabunge warudi bungeni wafanye marekebisho hakuamaanisha kuwa mswada hatausaini. Sana sana alichosema ambacho nataka watu fulani ambao vichwa vyao ni vigumu kuelewa waelewe kuwa Mh Rais alizungumzia kanuni za Bunge kuhusu kamati ya Bunge ya sheria na katiba kutoenda Zanzibar. Baada ya maelezo yake akasema hakuna mahali popote, narudia hakuna mahali popote ambapo kanuni za kudumu za bunge zinasema kamati (yoyote) inabidi iende Zanzibar na kama wabunge wanaona iwe hivyo basi warudi Bungeni wafanye marekebisho ya kanuni. Sasa bahati mbaya kuna watu uelewa wao ni hafifu na wako humu kijiweni; walidhani Mh KASEMA MSWADA URUDI BUNGENI, UFINYU WA FIKRA NA UDHAIFU WA KUELEWA uliwafanya hawa DUNDUNDU wadhani kihivyo na kuanza kusherehekea ufinyu wao wa kuelewa. Ndani mwao kuna wengine wanaelewa alichosema Mh Rais lakini kwa kuwa wanaona wakiwaelimisha alichosema Mh watawachukia kwa kuwa vichwa vimejaa maji tu yaani ni watu wanaoelewa kutokuelewa. Mmoja wao ni Tundu, huyu anajua alichosema Mh Rais lakini amaeacha DUNDUNDU wachemke wenyewe wakidhani yupo pamoja nao. Fikiri kabla ya kutenda, na Waingereza wana msemo mzuri tu kwa kiswahili kisicho rasmi unasema, husiseme kabla hujafanya utafiti maana utaonekana boya na kituko.:frusty:

kwani huo muswada ukisainiwa ukawa sheria ukirejeshwa bungeni haurekebishiki tena? kama ukirekebishwa si ndio yaleyale? ni bora wabunge wachumia tumbo wa magamba wasingeuchakachua muswada bkuliko jinsi wanavyopoteza muda na pesa za umma kwa maslahi ya kuchuma posho uzembe kwa ajili ya matumbo yao makubwa kama mapakacha, yasiyoshiba kamwe. hawa magamba wataiyumbisha sana nchi hii. pumbaf zao.....
 
Kumbe maneno yote yale hata muswaada wenyewe hajausoma? Sasa yale aliyosema yanajadilika kayatoa wapi? Au ndiyo yale ya NIMEAMBIWA?


Maneno ya kuambiwa hayo,yule jamaa anajielewa mwnyewe tuh
 
Kilichonishangaza mimi ni kuwa muswada haujafika kwa Rais na yet ameuzungumzia kwenye hotuba yake...

atakuwa KASIKIA au KAAMBIWA yaliyomo kwenye muswada, ndio maana akaungelea kwenye mazungumzo yake ya mila mwezi.
 
Back
Top Bottom