Ila Bashe! Nchi ina upungufu wa sukari tani 30,000; yeye anaagiza tani 400,000!

Tani 30,000 zisingeweza kusovu.Pia sio Serikali inaagiza Bali ni wafanyabiashara
 
Tena angeagiza mara tatu yake zaidi watu tununue kilo Moja Kwa buku. Haiwezekani watu tunapata shida hapa sukari bei juu wakati huko nje ipo tena ya bei nafuu kuliko hata ya ndani.

Hebu fikiria hivi viwanda vya ndani vinavyodeka;soko lipo, mashamba yapo tena na wananchi wanalima miwa Ili kuviuzia viwanda halafu sukari haipatikani kwa bei rafiki
 
You overlooked this...
 
UZURI NI KWAMBA KABURI HALICHAGUI MASKINI NA TAJIRI .CHA MUHIMU HELA ZISIIBIWE KWENDA KUFADHILI MAGAIDI
 
Kwahiyo ulitaka ziagizwe chache ili muuze 5k kwa kilo?
 
We jamaa kwa maandiko yako tunafahamu una uelewa mpana wa mambo, hebu acha kujitoa akili.

Watu hawalaumu sukari kuwepo, wanauliza kiasi kikubwa kilichozidi tofauti na kilichoidhinishwa na Bunge.

Hao waliopewa tenda wamepewa kwa kufuata sheria ipi?

Anaetakiwa kuagiza sukari kwa mujibu wa sheria ni nani na kwa kufuata taratibu zipi.

Haya yote unayajua isipokuwa umeamua tu kujifyatua mkuu.
Kwani toka sukari ya bashe iingie mbona bei ndio imeshuka, sijaelewa bado malalamiko yenu ni yapi hasa?

Maana sukari ikiwa chache bei hupanda, sasa ikizidi tatizo ni nini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…