Charlz ze son conscious
JF-Expert Member
- Aug 22, 2019
- 554
- 848
Mwaka bora uishe tu
Pole
Pole
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hawakuingiza wale matapeli ndio waliniambia kuna hela zao wanatransfer kwenye acccount yangu ili mimi nitoe niwape,. Maanake wangekua wameweka kweli salio lingeongezeka ningewatolea yao hela yangu ingebaki vilevile ( Kwa maelezo yao lakini, na mimi sijui ndio nilikua nisharukwa na akili nikaamini )Akaunti inakuwaje na laki 6 kama kuna 1.5mil. imeingia? Hiyo ndio point yangu iliyoganya nigome kukuamini
Uko sawa kabisa mkuu. Hata ukikutana na rafiki yako wa zamani mlipotezana usimuàmini hata chembe pengine kashakuwa tapeli. Tena mtu akijifanya mtu wa Mungu hapo ndio ukimbie fastaaa hàdi mguu uvunjike.Mimi hata mtu ninaemjua
Akinisimamisha huwa namsalimia juu juu
Sembuse nisie mjua
Yaani napitaga wima wima sana
Sisimamagi popote
Yaani mtu akishaanza sijui imepanda imeshuka
Ataniona yuleeee
Dar asilimia 70 watu wajanja wajanja tu
Bora uonekane sio mkarimu tu
Haya , nitakutumia milioni 2 baadae, nipe uliyonayo halafu ikiingia yangu tutakatana..Hawakuingiza wale matapeli ndio waliniambia kuna hela zao wanatransfer kwenye acccount yangu ili mimi nitoe niwape,. Maanake wangekua wameweka kweli salio lingeongezeka ningewatolea yao hela yangu ingebaki vilevile ( Kwa maelezo yao lakini, na mimi sijui ndio nilikua nisharukwa na akili nikaamini )
Wakamtajia na majina yake matatuHizo si uchawi ni mind games tu...watu wanasemaga uchawi ili wasionekane wajinga coz uchawi hauna evidence...wamecheza na psychology...me ishawahi nikuta na nilifanikiwa kusanuka last minute..me Hadi gari nilipanda so ningeweza kusema nimerogwa ila ni psychology tu ikitokea hivyo unajifunza huwezi tapeliwa kizembe... sijawahi ona mtu anatapeliwa mara mbili za hivyo barabarani
Ni vizuri kutokujibu salamu yoyote ile au kuitika ukiitwa na mtu ambae humjui.Ila dsm ni hatar,muda wote unatakiwa kukaa kimachale
Ata mimi walinikosa mtandao wa Equety Bank ulikua unasumbua nikichomeka kadi kwenye Machine ya ATM za Bank zote kadi inatemwa, kila nitia kadi mashine inaitoa nje.Hata Mimi hapo soko la Songea nilishawahi kutapeliwa 😅😅😅
Nimetoka zangu home Bombambili nikashuka kwenye daladala tu wakanidaka wakaniita mpaka majina yangu yote matatu. Story nyingi sana na enzi zile nilikuwa na miaka kama 16 tu. Aisee walinipumbaza akili wakanipeleka mpaka pale Bank ya NBC nikawapa hela 80,000 aisee.
Akili zimekuja kunirudia baadaye, wajinga huwa wanafanya namna sio bure.
Usijisumbue hao matapeli Wala hawahusiani na taasisi hizo. Wanaweza kuchora gari lolote ili waendane na uhalisia.Nawaza sijui nianzie pale st.Joseph university kampasi yao, niende kule primary school na hospitali
Lakini kweli police wetu wanashindwa kufanya uchunguzi kwa details hizo jamani🤔
Classmate wangu wa O level na A level, baba yake ni jaji alistaafu kipindi cha Kikwete. Tumemaliza shule miaka 15 iliyopita. Siku napokea simu ananikopa laki 2. Nilikuwa Sina Nina laki 1. Akasema nipe narudisha mwisho wa mwezi. Tangia 2020 hadi leo hajalipa hiyo hela. Siku nimemuelezea Classmate mwingine hiyo issue. Akaniambia kiufupi jamaa akikopa halipi na amewakopa wanadarasa zaidi ya 10 hajawalipa hadi leo.Mimi hata mtu ninaemjua
Akinisimamisha huwa namsalimia juu juu
Sembuse nisie mjua
Yaani napitaga wima wima sana
Sisimamagi popote
Yaani mtu akishaanza sijui imepanda imeshuka
Ataniona yuleeee
Dar asilimia 70 watu wajanja wajanja tu
Bora uonekane sio mkarimu tu
Nguruwe akipewa samaki inakuwajesikia sikuhizi wizi haufanywi kizembe ila kijasusi ....kingine madawa yanatumikab kile kitendo mtu kajua jina lako anakutaja ukiitika tu utafata kila unachoelekezwa ...mtego huu unaitwa samaki kwa nguruwe
ulishawahi kuona nguruwe akipewa samaki au harufu yake tu ipite maeneo yake
Aiseee pole sana mkuu, wale jamaa ni hatari sana kwa kucheza na saikolojia ya mtuHuu mwaka umekua wa hovyo mapema mnoo aisee,
Habari zenu kwanza wakuu
Mwenzenu jana nimetapeliwa, na nikiri tu kuwaambia uchawi upo wakuu, Ilikua jana kuna hela nilipatiwa nikamlipie dogo Ada, Nimeenda bank( NMB)nimelipa, ile wakati natoka nikawa naelekea ile njia ya sokoni ili nikapite vile NBC then Mtaa wa zanzibar nichukue baadhi ya vitu halafu nirudi Nyumbani.. Asa wakati natembea mbele yangu kulikua na Gari Hillux ( sijui ndio hilohilo jina, ila ni haya wanatembeleaga sana wakandarasi sikufanikiwa kukariri plate number zake) Limeandikwa St. Joseph ila sikuweza kumalizia ni St Joseph nini maana kuna mtu alikua ameegemea pale kwenye Maandishi..
Napita akaniita kwa majina yangu matatu kabisa, Dada Lee habari?,, nikaitikia salama za kwako?, akanijibu tu safi za masiku nikamwambia salama nikawa nataka kuendelea kuondoka sikuwaza kwasabu nilijua huenda mteja niliwahi kumuhudumia kunijua majina yangu sio kesi,. Kabla sijafika mbali akaniita tena Akaniambia nashida mara moja naomba nisaidie nikamuuliza shida gani?,. Akasema yuko na sister mle ndani na kweli alishusha kioo ni mama mmoja hivi kavaa mavazi yale ya masista,.
Akaniambia mwanangu nina shida naomba nisaidie,. Nilikua natoa hela pale Atm bahati mbaya nimekosea pin mara3, Kadi Yangu imemezwa nasiwezi kwenda ndani kutoa sina kitambulisho,, sasa nataka uende kuna mtu nimeongea nae akahamishie hela kwenye account yako halafu utoe unipatie,,. ( Kwanza kwa maelezo kama hayo wakuu mtu mwenye akili timamu anaona kabisa hayana mashiko, kwanza kutoa hela kwenye Account yako na kitambulisho wapi na wapi?, alijuaje nina NMB account?, na kwanini asimtume yule kijana??,,. )
Basi dada enu ndo nlikua nisharogwa nahisi nikasema sawa,. Nipe namba ya huyo mtu akasema ukienda tu atakuona akachukua karatasi akaandika kiasi Tsh. 1.5m na akaomba nimtajie namba yangu ya Account nikamtajia basi nikaingia ndani, Mwenzenu nikiri tu sikua naelewa chochote mpaka wakati huo😥 ,. Nikaenda moja kwa moja nimejaza slip ya kutoa hizo hela na ni Account namba yangu niliandika,. Nimekaa foleni mpaka nimefika dirishani yule dada ananiambia mbona Acount yako haina hilo salio dada?,. Kiukweli sikua na hiyo hela ila akili yangu ilikua inaniambia kuna hela zinaingia so itakuwa ipo,. Nikamwambia yule dada basi tutoe kwanza hiyo iliyokuwepo nikarudi kujaza slip upya nikatoa laki6 na 15,. Nikarudi kule nje nikamwambia yule sista bado hawajaingiza ipo ileile yangu akaniambia nipe hiyo kwanza sisi tumwahi mgojwa wewe kaa dakika tano nenda tena watakua washahamishia hela kwako na sisi tunakuja mda sio mrefu,. Si nikakubali nimekaa weeee Pale nje sokoni kila nikienda ndani naambiwa hakuna salio..
Baadae sana ndio napata wazo hawa watakua washanitapeli maana hawakunipa hata namba yao, na Namba yao ya Account wala chochote ile karatasi waliandika tu kiasi na namba yangu ya account niliyowatajia ( Aisee jamani nimelia jana tena sanaaa),. Nikawafata wale walinzi nikawaambia nikawaelekeza na walikokua wamepark gari wanasema kule mbali sana Cctv camera haziwezi zinaonyesha kitu ( Ni kule karibu na mlango wa kuingilia soko kuu kwa mbele kidogo kama unataka Ukunje kona uende NBC),. Polisi nako ndio vilevile jana hamna hata cha maana nilijibiwa,. Na sijui ile gari ilikua ni ya St. Joseph University, St. Joseph Primary school, Hospital au ni nini??.
Nachoshukuru ni kwamba nilifanikiwa tu kulipa Ada ya dogo maana Bila hivyo walahi mzee angenikata kichwa au yeye afe kwa Pressure,.
Ila kuna watu ni wakatili sana, mlaaniwe nyie wakujiita watumishi wa Mungu halafu kumbe ni wezi,. For real wamenitia Umasikini maana ndio ilikua hela yangu ya mwisho. Mwaka ushakua wa Hovyo huu,. Tuwe makini jamani matapeli bado wapo na ninahisi wanatumia uchawi maana sio bure🤔😭
Madam hapo wamecheza na saikolojia yako...Huu mwaka umekua wa hovyo mapema mnoo aisee,

Mkuu kiufupi kabisa hawa ni matapeli,
Hata panya ili tuwanase huwa tuna wawekea mnofu wenye sumu au unatega mtego wenye mnofu... Sasa kuna panya wajanja huwa hawanasi kwenye mitego kama hii Sasa hembu tofautisha gap kati ya akili ya panya na akili ya wanadamu... Lakini bado kunapanya wanacheza na akili ya mwanadamu😂😂😂 nitoe Wito jamani binadamu wezangu tujitahidi panya wasituzidi akili/ujanja.
Matapeli wanatumia sifa kuu nne za mwanadamu kama ni mwepesi kwenye hizo sifa basi unahatihati ya kutapeliwa.
Sifa hizo ni hizi.
1. Tamaa (usiwe na tamaa na kitu kisichokua halali yako) pia hapa usiwe mroho mroho wa vyakula na vinywaji pia usimuamini kila mtu.
2. Uaminifu (usiwe mwepesi wa kuamini jambo)
3. Huruma (ukiwa na huruma sana basi hakikisha unakuwa na hekima ya kutosha/akili kwasababu kupitia huruma yako tapeli anaweza kukuaminisha (Kwahiyo tapeli anaweza kukuingia kirahisi akikujia na gia ya kuhuzunisha ukaingia mkenge) anaweza wakaja na stori ya kuhuzunisha ukamuonea huruma pengine ukamkaribisha nyumbani, game over))
4. Shida(umasikini mbaya sana, ukiwa na shida tuliza akili vizuri usiwe na pupa wala haraka amua maamuzi yako kwa Akili timamu na kufauta talatibu za kisheria, sio kwasababu una shida ndio uchukulie poa.
Yaani kwa mwanaume hakikisha watakoa fanikisha kukuibia ni wale wanaokuja ana kwa ana na silaha/majambazi au vibaka na umezidiwa, ila sio sio kwa kutapeliwa.
Mwisho kabisa linapokuja suala la mali aidha makabidhiano/kuuziana usichukukulie poa wala usilete kujuana sijui rafiki mpenzi ama ndugu, huyu jamaa yangu... Hakikisha taratibu zote zinaenda kiuweledi zaidi /kisheria/kiprofessional kwanini ni kwasababu hari ya mtu huwa inabadilika kulingana na mazingira na jambo analopitia wakati huo, mfano: mtu akiwa nashida huwa anashuka anakuwa mkarimu mpole na kwa muda huo anachokiongea ni kweli kinatoka moyoni na yuko serious kabisa, sasa wewe chakufanya hapa pasipo kujali wanakuaga muaminifu au sio muaminifu wewe cha kuzingatia Hakikisha mnaandikishiana kisheria na mbele ya mashahidi, usije kuthubutu mkakabidhiana kienyeji,
Kwanini kwasababu baadae shida ikiisha na ile hali ya usikivu unyenyekevu inaisha, ikiisha swala lako anakuwa halichukulii uzito kama walivyokua anakuomba. usumbufu unaanzia hapo na anaweza akakudhulumu kama akijua hakuna shahidi yoyote.
Na aina hii ya utapeli huwa inafanya kazi kwa ufahasa kwa wanawake mpo weak sana kwenye ulimwengu wa kiroho pole sana walichukua akili yako kwa muda
Mkuu hii elimu ninatamani kuijua maana bi mkubwa alipigwa 14m ya vicoba, wallah ningekuwa simfahamu vizuri na ni kijana bado ningesema aliwapiga wanakikoba wenzake...yaani alitoka na wezi mwendo wa kama kilometa 15 mpaka nyumbani kwake na kuwapa wezi sanduku la pesa kwa mkono wake mwenyewe...
Sijui wanatumia nini wallahDah Acha tu
Kuna Bidada last year katembea na matapeli hadi wakapanda daladala, kufika nyumbani kawapa bag la Jewelery eti wakaliombeee
🤣🤣🤣