Ila kutapeliwa kunauma wakuu

Akaunti inakuwaje na laki 6 kama kuna 1.5mil. imeingia? Hiyo ndio point yangu iliyoganya nigome kukuamini
Hawakuingiza wale matapeli ndio waliniambia kuna hela zao wanatransfer kwenye acccount yangu ili mimi nitoe niwape,. Maanake wangekua wameweka kweli salio lingeongezeka ningewatolea yao hela yangu ingebaki vilevile ( Kwa maelezo yao lakini, na mimi sijui ndio nilikua nisharukwa na akili nikaamini )
 
Uko sawa kabisa mkuu. Hata ukikutana na rafiki yako wa zamani mlipotezana usimuàmini hata chembe pengine kashakuwa tapeli. Tena mtu akijifanya mtu wa Mungu hapo ndio ukimbie fastaaa hàdi mguu uvunjike.
 
Haya , nitakutumia milioni 2 baadae, nipe uliyonayo halafu ikiingia yangu tutakatana..

We unaona hilo jambo mtu anaweza kuamini kweli?
 
Haya , nitakutumia milioni 2 baadae, nipe uliyonayo halafu ikiingia yangu tutakatana..

We unaona hilo jambo mtu anaweza kuamini kweli?
NDio maana nikasema uchawi umehusika maana mie nakuwaga makini sana
 
Wakamtajia na majina yake matatu
 
Ata mimi walinikosa mtandao wa Equety Bank ulikua unasumbua nikichomeka kadi kwenye Machine ya ATM za Bank zote kadi inatemwa, kila nitia kadi mashine inaitoa nje.
 
Huo wizi wa kawaida sana maeneo ya Kibo complex Tegeta, mlimani city, Posta mpya. Pale Posta Kuna mzee anajiita mzee Mlawa ukimuona kavaa Pete ya ndoa na kachomekea vizur tu lakini tapeli
 
Sio mbaya ndo umepata cheti kingine,
Jamaa wamekupiga aisee Hadi unatuambia kuhusu huko sokoni as if tunajua soko gani au njia gani sijui duka la Zanzibar.
 
Nawaza sijui nianzie pale st.Joseph university kampasi yao, niende kule primary school na hospitali
Lakini kweli police wetu wanashindwa kufanya uchunguzi kwa details hizo jamani🤔
Usijisumbue hao matapeli Wala hawahusiani na taasisi hizo. Wanaweza kuchora gari lolote ili waendane na uhalisia.
Unafikiri wangekuja na Rasta na pensi chafu ungewaamini?
 
Classmate wangu wa O level na A level, baba yake ni jaji alistaafu kipindi cha Kikwete. Tumemaliza shule miaka 15 iliyopita. Siku napokea simu ananikopa laki 2. Nilikuwa Sina Nina laki 1. Akasema nipe narudisha mwisho wa mwezi. Tangia 2020 hadi leo hajalipa hiyo hela. Siku nimemuelezea Classmate mwingine hiyo issue. Akaniambia kiufupi jamaa akikopa halipi na amewakopa wanadarasa zaidi ya 10 hajawalipa hadi leo.
 
Nguruwe akipewa samaki inakuwaje
 
Aiseee pole sana mkuu, wale jamaa ni hatari sana kwa kucheza na saikolojia ya mtu
 
Madam hapo wamecheza na saikolojia yako...

Kosa lako ni kuamini yale mazingira waliokutengenezea.

Ungejiuliza hivi hii Taasisi imekosa backup kweli hadi wamvae mtu random tu.
 
Na aina hii ya utapeli huwa inafanya kazi kwa ufahasa kwa wanawake mpo weak sana kwenye ulimwengu wa kiroho pole sana walichukua akili yako kwa muda

Sio aina hiyo tu, wanawake wanatapeliwa kirahisi sana.
Wana hisia(Huruma, upole na Ukarimu) sana kuliko kutumia akili.
Tapeli ukianza kumsikiliza tu ni kosaa
 

Dah Acha tu

Kuna Bidada last year katembea na matapeli hadi wakapanda daladala, kufika nyumbani kawapa bag la Jewelery eti wakaliombeee

🤣🤣🤣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…