Ila kutapeliwa kunauma wakuu

Ila kutapeliwa kunauma wakuu

Dawa rahisi kabisa ya kudhibiti utapeli wa aina hiyo, ni hii hapa;
Ukiwa mjini, ukitoka tu benki, au ukiwa katika mishe zako! Jitahidi uwe busy tu na mambo yako! Na usikubali kamwe kumsikiliza mtu anayekuita au kukusimamisha ili akuambie shida yake.

Na kwa ule utapeli wa kwenye simu, na wenyewe ni hivyo hivyo! Usikubali kumsikiliza mtu. Wewe mwambie kwa ufupi tu uko busy, na kama atakuambia eti kuna hela sijui imetumwa kimakosa kwenye simu yako; mjibu tu kirahisi apige simu huduma kwa wateja ili arejeshewe hiyo pesa yake! Maana hilo silo jukumu lako.
 
Shukuru hata umetapeliwa hela zako safi, ukaishia kwenda kulia nyumbani kwenu.


Siku nyingine usikubali tu kuingiziwa hela kwenye akaunti yako na mtu usiyemfahamu. Ni very risky na hatari sana.

Kuna watu wanatapeliwa, na isivyo bahati njema matapeli wanatafuta njia ya kuitoa na kusafisha. Ikiwekwa tu kwenye akaunti yako, umeliwa.

Kuna hela nyingi za madili zinapigwa. Ili kuzisafisha, zinagawanywa kwenye akaunti kadhaa. Sasa baadae dili likibumba, utahenyeka mpaka ukome.

Kuna watu wanauwawa. Na matapeli wanakosa namna ya kutoa pesa isipokuwa transfer. Nani wa kumhamishia? Kanyaboya mmoja. Polisi wakifanya yao, watakukamata. Utalia na kusaga meno.

Usijaribu tena.
Kaa mbali na usiyemjua inapokuwq kwenye swala la hela.
 
Hata Mimi nikiwahi pigwa na Hawa kenge,nimetoka zangu home full pocket money naelekea zangu boarding school wale wangese walinisimamisha wakataja majina yngu yote matatu na kuongezea kubwa bibi yako ni mgonjjwa sana halafu wakanitoa manyoya mdomoni nakuja kujitambua wamesepa na kila kitu Hadi lakuchumpa langu timberland Kuna msamaria akanipa ndalana nauli narudi home kilio tu.Cha kushangaza mshua alicheka tu Wala hakuna react!
 
Dawa rahisi kabisa ya kudhibiti utapeli wa aina hiyo, ni hii hapa;
Ukiwa mjini, ukitoka tu benki, au ukiwa katika mishe zako! Jitahidi uwe busy tu na mambo yako! Na usikubali kamwe kumsikiliza mtu anayekuita au kukusimamisha ili akuambie shida yake.

Na kwa ule utapeli wa kwenye simu, na wenyewe ni hivyo hivyo! Usikubali kumsikiliza mtu. Wewe mwambie kwa ufupi tu uko busy, na kama atakuambia eti kuna hela sijui imetumwa kimakosa kwenye simu yako; mjibu tu kirahisi apige simu huduma kwa wateja ili arejeshewe hiyo pesa yake! Maana hilo silo jukumu lako.
Naunga mkono hoja, kitendo cha kuwasikiliza ni hatarishi sana.
 
Mimi nilipata mteja wa mpesa akaniambia anatoa 40K nikamwambia toa, akaomba namba ya wakala nikamtajia, akataja jina nikasema correct, si nikahesabu hela nikampa! kuangalia meseji iliyoingia sio!! alafu jamaa ameshaondoka aah acha kabisa.
 
Me nilipigwa ada ya chuo semester 1 mwaka wa kwanza ilikuwa tabata, sitasahau niilibiwa ndani ya bank CRDB Tabata magengeni.
Nilitembea kwa mguu hadi polisi kufika wakaniandikia RB then wakanambia waniunganishe na mpelelezi ili afatilie CCTV camera alitaka nilimpe laki 3. Walinizungusha sana hadi nikakata tamaa kufatilia, Ila nashukuru mungu nilifanikiwa kupata ada nyingine nikalipia na kuanza masomo.
Ile siku nilikuwa nahisi ni ndoto.
 
Pole sana kwa kupigwa tukio, nakumbuka niliwai tapeliwa na hao jamaa mwaka 2004 nikiwa form 2 bado mdogo masikini mtoto wa watu waliniibia shenzi kabsa hawa wauni. Ilikuwa mwenge pale ilipokuwa stendi ya daladala alianza kuja mmoja akaniuliza kdgo akaja mwingine kumbe walikuwa wanajuana wale dah wakuu hawa watu wanatumia dawa usithubutu kukutana na bwana pepsi
 
Pole sana, haya mambo kama hayajawahi kukutokea au kumtokea mtu wako wa karibu, unaweza hisi ni story tu!!
Mwanangu aliwahi kutapeliwa simu katika mazingira kama hayohayo. Alikuwa akikuelezea namna alivyotapeliwa yaani haiingii akilini.

Miaka ya nyuma sana nami walitaka kunifanyia mchezo huo, nashukuru account ilikuwa inasoma frequency za fm radio😅😅
 
Back
Top Bottom