Half american
JF-Expert Member
- Sep 21, 2018
- 38,283
- 97,793
Usiku ni mrefu ila ukilala na kuota ndoto za ajabu ajabu huufanya uwe mrefu zaidi. Kuna baadhi ya ndoto nikiota ni ngumu sana kuzikumbuka na hizi ndio hunipa hofu hasa nikiota ndoto mbaya.
Huwa ninapata hofu kwa sababu ndoto nyingi nisizozikumbuka huwa zina uwezekano mkubwa wa kutokea na zikishatokea huwa ndio nakumbuka tukio husika na kupata picha kuwa tukio husika niliona ndotoni kama lilivyo. Huwa nashangazwa sana na hii hali inawezekanaje nishindwe kuvuta kumbukumbu mda mfupi baada ya kuota lakini ukipita muda na nikaliona tukio nakumbuka kuwa niliwahi kuota kwenye ndoto ambayo sikuikumbuka?
Tukio la ndoto ya usiku wa kuamkia leo limenichosha, ni nafuu zaidi kwa sababu nalikumbuka, kwangu haina athari kama nisingekumbuka. Niliota hivi,
Kulikuwa na sherehe sijui ilikuwa ni yanini ila niliofanikiwa kuwaona
ndani ni baadhi ya maclass mate. Kwenye hiyo sherehe kiingilio kwa wanaume ni lazima uwe na kitambi tena kikubwa haswa na ukaguzi ulikuwa unaendelea kwenye lango la kuingia ukifika unavua saa, pete na shati unalikunja vizuri unaacha mlangoni unaingia tumbo wazi. Nikikumbuka hicho kitambi changu cha ndotoni nacheka sijui nilikipatia wapi mpaka kutembea ikawa shida, ni kile kitambi kikubwa kilichomwagikia pembeni na chini.
Baada ya kuingia ndani tulikaa kwa muda na hakukuwa na kinywaji chochote kile zaidi ya maongezi na niliowakuta, muda ulivyosogea likaanza zoezi la chakula, unanyanyuka kwa utaratibu kuelekea bufee zilipo na kupakuliwa chakula. Ilipofika zamu yangu nafika kwenye bufee hakuna sahani hata moja, mhudumu akaniomba nitafute sahani kwa waliomaliza nioshe ili niwekewe (muda huo vyakula kwenye bufee bado vimejaa).
Nilitembea kwa shida sana kutokana na kitambi changu kilichokuwa kinacheza kila nikipiga hatua na nilifanikiwa kupata sahani na kuiosha, ile nimerudi nafika kwenye bufee nanyoosha sahani niwekewe msosi naambiwa umeshachelewa chakula kimeisha (wazee wa sherehe ni chakula nadhani mnaelewa hii inavyokata), ile taarifa ya chakula kuisha ilinishtua hadi nikashtuka usingizini na ndoto ikaishia hapo.
Tukio lililotokea INAENDELEA COMMENT #1