Ila tusemeni Tu ukweli bila wivu mtu akisoma masomo ya sayansi halafu akawa Rais lazima TAIFA lipige hatua kimaendeleo

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
25,030
Reaction score
61,298
Najua hii itawaumiza ambao mmesoma masomo ya Sanaa na biashara lakini ukweli masomo yenu tofauti na sayansi hayana foundation za kutafuta majibu kwa changamoto nyie NI watu wa negotiation Tu mambo ya diplomasia.

Mifano ipo na tumeshuhudia baada ya hapo naombeni mnitajie viongozi wa sasa hasa wa CCM wabunge au mawaziri ambao wame specialize kwenye science fields kama vile engineerings, chemistry, environmental and ecology,hesabu, geology n.k niwaweke kwenye maombi maalumu RAIS ajae nakuomba mwenyeziMungu tupatie mwanasayansi please..

NB:SIJASEMA SUBJECTS NYINGINE HAZIFAI MAISHANI AU HATUZIHITAJI ZOTE NATAMBUA UMUHIMU WAKE ILA KWA LEVEL YA RAIS YAFAA MWENYE MAONO YA SAYANSI.
 

Unataka kusemaje? 😂
 
Rais wa China tangu mwaka 1990 lazima awe na digrii ya engineering na ndicho kipindi ambacho China imeendelea kwa kasi sana
 
Tupe na mifano kama kumi mkuu
 
Nadhani umemaanisha Rais ....
Nafikiri ulisoma kabla sijarekebisha ila ni kweli, nilikuwa na maana ya rais. China wanaongozwa na watu wenye digrii za engineering, halafu watu wenye digrii hizo ndio wengi sana serikaliniu; sisi tunaongozwa na watu wenye elimu za kuungaunga tu, na sasa tutakuwa na makamu wa rais ambaye alianza kwa kununua digrii alipobanwa ndipo akafanya mpango wa kuipata digrii hiyo kutoka Mzumbe ikiwa ni ya kuunganunga tu. Utaona kuwa hatuna maono kabisa bali ni nchi ya wababaishaji tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…